Mpango wowote wa TRA kukamata wasiodai risiti hautofanikiwa hadi pale Wamachinga watakapoondolewa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
FB_IMG_1610015199147.jpg

Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.

Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.

Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?

Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.

Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.
 
Wapiga kura wa Rais hawatakiwi kulipa kodi ya biashara, ukitaka nawe hamia huko.
Ni sawa kabisa na sijabisha hilo mkuu, hoja iko kwa wateja wao wanapokutwa na bidhaa bila risiti.
 
Hapa kuna haja kwa Serikali kuangalia upya suala la vitambulisho vya machinga interms mtaji/aina ya biashara.
Lakini pia TRA wanaweza kubuni app ya risiti ili kila machinga mwenye biashara atoe risiti ya kielectronic.
 
Ni Kweli ulichosema,watakamata wanaotoka Petrol station na sehemu tunaponunua vitu ambapo hakuna bidhaa zilizobebwa na wamachinga.Kuna siku nimenunua kitu dukani kariakoo nikasahau kuchukua receipt nikiwa njiani nikampigia mwenye duka nikamwambia anitumie receipt yangu nimesahau wasije wakanikamata akanijibu waambie umenunua kwa wamachinga nilicheka sana (kama mazuri) kwani tunaikosesha nchi kodi ujue
 
itakuwa ni ujinga mtupu kumkamata mtu ilhari vitu hivyo vinauzwa barabara, kuna redio kubwa kabisa, hata ukienda posta watu wanauza suti kali na viatu hai vya laki moja na nusu sasa serikali imerikologa kwa kuendekeza wapiga kura hacha waliwe
 
Inabidi tu ibuniwe mifumo ya kodi kulingana na mazingira yetu. Kuna shughuli nyingi sana zinazofanywa na watu hazilipiwi kodi kutokana na sheria zilizowekwa za usajiri wa shughuli hizo zinazosabababisha zisitambulike rasmi, kule kukosa urasmi ndiko kunakosababisha serikali ikose mapato.

USHAURI WANGU KWA WATUMUSHI SERIKALI
Ebu tuache ubabe kwa kuwafokea watu kwamba kwa nini wanaanzisha shughuli Fulani bila kufuata utaratibu na kufunga, ebu tuwasaidie watu namna ya kufuata au kukamilisha taratibu hizo ili wawe walipa kodi wazuri.
Watumishi wengi wa serikali wanapenda kuonyesha mamlaka waliyonayo badala ya kusaidie watu.
 
Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.

Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.

Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?

Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.

Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.
Dhuluma ndio maisha ya sasa kama hayaja kukuta basi kazi unayo.
 
Back
Top Bottom