Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ni vigumu sana kujua nani kanunua bidhaa zake wapi, hii ni kwa sababu Wamachinga wanauza kila kitu kinachouzwa madukani tena bila kikwazo chochote.
Wamachinga wanauza nguo, simu, vifaa vya simu, vifaa vya mahospitalini, vifaa vya shule, TV , vifaa vya majumbani na maofisini, ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu, dawa za meno na dawa za magonjwa mengine zinapangwa barabarani kuanzia Kariakoo, Manzese hadi Mbagala huku zikipigwa jua kutwa nzima.
Wamachinga hawana machine za EFD na wala hawabughuziwi kwenye hilo huku wakifanya biashara kubwa kuliko wenye maduka na taarifa za sasa za Kariakoo zinaonyesha kwamba Wamachinga ni almost 70% ya wafanyabiashara wote, sasa kwa hali hii unawezaje kumuuliza mtu risiti ya alichonunua?
Labda TRA iseme kwamba imelenga kuwakomoa wauzaji wa jumla ambao ndio unaweza kuwatofautisha na wengine, Vinginevyo TRA yaweza kushitakiwa mahakamani kwa kumkamata aliyenunua kwa wamachinga ambao wanauza kila kitu kuliko hata maduka halali, maana hakuna duka lolote la halali linaloweza kuuza kandambili, chupi za watoto na humo humo likauza na dawa za binadamu pamoja na sumu za panya.
Ikumbukwe pia kwamba Watanzania hawajui lolote kuhusu sheria za uuzaji wa baadhi ya bidhaa , wanachoangalia ni bei rahisi pekee , kwahiyo kumkamata huku akiwa kanunua kihalali kwa muuzaji aliyevaa kitambulisho halali cha Mmachinga utakuwa uonevu wa kutisha.