Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Kaka Kama umefuatilia kwa making kuhusu sakata la DP world utagundua wanaopinga hawana shida na uwezo wa Dp world ila shida yao kuwa ni vifungu vya mkataba ambapo kikawaida mkataba unatakiwa uwe win win katika haki na wajibu wa pande zote zinazohusika na huo mkataba Sasa huu mkataba hauko na usawa kwamba Tanganyika inapewa wajibu zaidi huku Dp world akipewa haki zaidi pia mkataba hauweki wazi kikomo cha uhai wake lakini zaidi hauonyeshi ni namna mwekezaji amepatikanaje, atawekeza kiasi gani n.k
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Tokea lini waislam hitaji lao lilikua shule na hospital
 
Kama hiyo ndio thinking na matarajio yako kutoka DPW, basi maaskofu wako sahihi.
Matarajio yangu toka dp world ni mapato bandarini kuwa zaidi ya Mara mbili,na kuchangia bajeti zaidi ya 60%,hicho nilichoandika ni matarajio ya kanisa,kile wanachoona kinakuja na dp world,wao hawajali mapato ya nchi,ukizingatia wanakula Bure kupitia sadaka na fungu la kumi na michango mingine,wanapitisha Bure mizigo bandarini na ruzuku toka hazina kwenda kwenye miradi yao,wanachohofia wao ni yule adui yao mkuu,kuona atapata pumzi
 
Je BANDARI ya Dar es salaam ina chapa ya nani…? TANZANIAAAA na je hao maaskofu ni raia wa nchi gani TANZANIAA? Na DP WORLD nao ni kina nani Waarabu … Basi vya watanzania waachieni WATANZANIA na vya waarabu wapeni WAARABU’
 
Nimesoma tamko la TEC

Kwanza tamko limesomwana mtu mmoja bila kuwepo na askofu mwingine yeyote.

Aliesoma na kuandika tamko amekuwa miongoni mwa watu wanaopinga mkataba wa bandari kwa nyakati tofauti hata kabla ya tamko la leo.
TEC imetumika kama Jukwaa lilisaidia slaa na kitima kufikisha hoja zao.

Rejea mjadala mdaharo uliowashirikisha Rostam,Kitila mkumbo,Zitto,Lema,Shekh Ponda,Balile na Dr Kitima mwenyewe.

Kwenye madaharo watu wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa uwekezaji,Kitima pekee ndie alikuwa na hoja tofauti, akasema haoni sababu ya kukabidhi uhuru wetu kwa waarabu,akapinga uwekezaji na kutaka mkataba tuachane nao,tuwaachie vijana wa kitanzania waendeshe,akaongeza kuwa hata wakiiba watatumia pesa hizo humuhumu nchini(ingia youtube andika mdaharo wa bandari utaona ninachokisema)

Leo ameibuka kama katibu wa TEC nafasi iliyowahi kushikwa na Dr.Slaa.

Anatoa tamko kwamba TEC inapinga uwekezaji na wanamuamuru Rais Ufute mkataba.
Kwenye andiko lake ametoa hoja kubwa tatu.

1.Kwenye andiko lake anadai Mihimili iheshimiane,isiingiliwe hapa alimaanisha Kesi ya mwabukusi ambayo kwa vyovyote Kitima alihusika kuifungua .

Kushindwa kwa Mwabukusi ni sawa na kushindwa kwa Kitima,lazima Kitima atafute plan B.

Kitima kwenye andiko lake anasema mihimili isiingiliane,kila muhimili uwe huru.

Kwake anaamini walishindwa kesi kwakuwa mahakama haikuwa na uhuru wa kufanya maamuzi,Kitima ni kama anasema mahakama ilishinikizwa kutoa yale maamuzi.

Halafu anafanya makosa kwenye andiko hilohilo kuhusu hoja hiyo kwa mushinikiza Rais Samia kutengua maamuzi ya bunge ambao ni muhimili mwingine wa dola ambao awali amesema mihimili isiingiliwe.

Hapa anahalalisha kuingiliwa kwa munimili wa Bunge ili kufanikisha malengo yake.

Rais akiingilia bunge atakuwa naendelea kuvunja katiba, kukosea kwa kufanya kile ambacho Kitima anapinga kwenye Tamko lake.

2.Kuhusu hoja ya kutaka Bandari iendeshwe na wazawa,kwamba haijawahi kuendeshwa na wageni,amesahau kuwa Bandari imeendeshwa na TICS kwa miaka 22 hakulisema hili kwa makusudi,huenda anatamani TICS ndio iendelee badala ya DP-World ili kulinda maslahi binafsi aliyonayo bandarini.

Hapa Kitima ni kama ana msalahi binafsi anayoyapigania kwa kutumia mwamvuli wa TEC,hoja yake inamashaka.kumbukeni sakata la ESCROW kuna hadi viongozi wa dini ambao walinufaika na wizi wa ESCROW sio wasafi kwa kiwango hicho.

3.Kitima na Dr.Slaa ni watu wenye Itikadi kali ya ukristo(Udini)

Kuna Wakristo wasiokuwa na ubaguzi halafu kuna Slaa na Kitima waliopea kwenye Udini.

Sio utamaduni wetu Watanzania kunadiliana habari za udini ma Ukabila,lakini kwa muktadha huu nitalisemea ili muwajue vizuri.

kwa nyakati tofauti Kitima ameonesha ni mtu mwenye chuki ya kidini na mdini sana tangu akiwa Makamu mkuu wa chuo cha St Augustine Mwanza.

Nakumbuka wakati wa utawala wa Rais Kikwete kwenye kipindi cha star TV chini ya Dotto Bulendu kitima aliilaumu serikali ya Rais kikwete kwa kuruhusu waarabu wenye ndevu hadi kifuani kuzagaa Kariakoo,alisema kwamba wale wenye ndevu ndio magaidi.kwamba serikali inawatazama haiwachukulii hatua.

Yaani kwenye ule mjadala, kitima akaona ndevu ni tishio kwake.
Ndio maana Tangu utawala uchukuliwe na Rais Magufuli,Mkatoliki mwenzake Kitima hajawahi kujitokeza hadharani kuipinga serikalinya magufulipamoja na chamgamoto zote za Utawala wa Magufuli.

Kadhalika Dr.Slaa,kwenye utawala wa Magufuli hakuwahi kuishambulia serikali kwa lolote hata pale palipokuwa na makosa ya wazi,baadae Slaa alipewa zawadi ya cheo kuwa balozi wa tanzania kwa kazi nzuri ya Kuhujumu demokrasia yetu.

Baadae alirudishwa nyumbani baada ya kumaliza muda wake wakati wa utawala wa Rais samia,hadi hivi karibuni kwenye sakata la mbowe,Slaa alisema mbowe anaweza kuwa gaidi kwamba mashtaka aliyoshtakiwa nayo yalikuwa halali,hapa alitoa kauli ya kumfurahisha Rais samia kwa lengo la kuwinda zawadi ya cheo kipya.
Rais Samia amejipambanua kuwa hataki wapambe,ni kiongozi anaetembea kwenye 4R,msisitizo ukiwa mwafaka wa kitaifa.

Watu kama slaa ambao wanashangilia mauaji na uonevu Rais samia aliona hawawezi kumsaidia.

Pia Rais Samia anaamini katika uongozi wa vijana.Slaa ana zaidi miaka 78.

Baada ya Slaa kukiridhisha kuwa utawala wa Rais Samia hauna mpango wa kumtumia,ndipo akaamua kuungana na Dr.Charles Kitima kuishambukia serikali

Kama Slaa angepewa cheo,muda huu angekuwa anatetea Mkataba wa DP World.

Huu ni uthibitisho kuwa Kitima na Slaa ni wadini sana ambao Kuingia kwa Rais Samia madarakani kwao waliona ni suprise.

Hawakujiadaa kuongozwa na Rais Samia ndio maana Wamekuwa mbogo sio kwenye mkataba wa bandari tu bali kwenye utawala wa Rais Samia kwa ujumla.

Rejea mahojiano ya Slaa na star tv baada ya Rais samia kuapishwa,Slaa aliishambulia serikali na kuituhumu kuhusu kifo cha Rais Magufuli,Slaa akamalizia kwa kusema kama wanataka wanikamate,siogopi kukamatwa.,alionekana ni mtu mwwnye hasira ya kukosa cheo.

Kwa msingi huo,huu ni uthibitisho kuwa Tamko lililoitwa la TEC lina msukumo wa kidini kuliko msukumo wa kisheria na kisiasa.

Nchi yetu ina dini kubwa Mbili,Wakristo na waislaam,tujaalie hilo ni tamko la wakatoliki.

Je na waislaam nao wakitoa tamko lao linalopingana na tamko la TEC?

Vipi walokole nao wakiunga mkono uwekezaji,serikali itafuata msimamo wa dini gani?

Ndio msingi uliosababisha serikali kutamka kuwa haina dini,lengo nikuepuka misuguano inayoweza kuliingiza taifa kwenye machafuko.

Tumeshatoa maoni,serikali imeyasikia na ndani ya serikali kuna watu wa dini zote na wasiokuwa na dini.,kuna wanasheria kuna vyombo mbalimbali vya dola.

Ni imani yangu kuwa Swala la uwekezaji wa Bandari watalifanyia kazi kwa kulinda maslahi ya taifa.

Viongozi wa dini wasiingile utendaji wa serikali ambayo kila mmoja anatambua haina dini.
Tuwapuuze Slaa na kitima,wanataka kutuingiza kwwnye vita yao ya maslahi binafsi kwa Kisingizio cha kulinda rasilimali ,tuulinde umoja wetu uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.
Tujifunze Burundi na Rwanda,mauaji ya kimbali yalihamasishwa na viongozi wa dini.
Duh!....
 
Mkuu Pascal Mayalla ameandika andiko lililoyumba. Maana analysis yake ameponda tamko la Maaskofu. Hitimisho ameshauri Mh Rais Samia akubaliane na Maaskofu. Huku ni kuyumba kiuandishi!

Kimsingi mchango wa Kanisa kijamii hapa Tanzania haupimiki. Ukitizama shule za msingi za kanisa, o level na a level schools, vyuo na vyuo vikuu ambavyo vipo affiliated na kanisa, hapo hatujagusa idadi ya hospital na vituo vya afya, na mipango kedekede ya kanisa kwa Kaya masikini kupitia shirika lake la Caritas. Hivyo ni ngumu sana kutenganisha kanisa na jamii na siasa za Tanzania.

Zaidi ikumbukwe Watumishi wengi (sio wote) wa ngazi za juu Serikalini wamefaidika na mifumo hii ya kanisa. Ndiposa taasisi hii ya kanisa katoliki ina-exert special threat kwa Serikali yoyote iliyopo madarakani.

Itoshe kusema, matawi ya filosofia - Epistemolojia na Ontolojia - ni silaha hatari sana ambazo ndio msingi wa kanisa.

Mkuu Pascal Mayalla amefanya haraka sana kukosoa tamko la Maaskofu. Sio kawaida kwa Pascal Mayalla kuandika ima kukosoa ima kupongeza pasina tafakari ya kina.

Unfortunately, this time around mwandamizi Mayalla ameloa.

Ma O level na A level waliosomeshwa na kanisa si ndio hawa wanaotia mikataba ambayo kanisa inakuja kupinga ??

Mahospitali haya tuliyonayo ya kanisa , mbona akina X Speaker, Ndungai bado walipelekwa India kutibiwa ?? hata Jiwe tuliambiwa dakika za mwisho alipelekwa nje pia ?? kuna nini huko Kanisani ??
 
Andaa andiko lingine la kuomba radhi mkuu muungwana akivuliwa nguo huchuntama sasa chuntama omba radhi, 'who the hell is....' unaelewa maana yake omba radhi umewakosea wazee wa baraza

Wazee wa Baraza ndio wa kumwomba radhi Pascal sio pascal wa kuomba radhi
 
Mbona hukusema neno wakati TEC walipomshutumu Magufuli na serikali yake kwa kuminya haki za binadamu, na uhuru wa vyombo vya habari? au unataka mpaka Magufuli nae atoe bure bandari zetu?

Hakutoa ndio maana wakakaa kimya, lakini alipokosea, walimpinga.
TEC wakati wa Magufuli ilifurukuta mara moja tu mwaka 2017 ikiwa chini ya Askofu Ngalelikumtwa wa Jimbo la Iringa. Mimi ni Mkatoliki, nasali kila J2 nikiweza na natoa Zaka na sadaka. Lakini Baraza la Maaskofu wangu ni WANAFIKI.

Mbona hawakuandika kitu wakati Magufuli anaendesha nchi kama familia yake na kuua watu. Hata shambulizi la Tundu Lissu la wazi kabisa hakuna mahali walilisemea
 
Acha kujieleza sana kama mgonjwa wa akili
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, tena sio Mkatoliki mlei tuu, ni miongoni mwa Wakatoliki wacheche waliokwenda kuhiji Israel, na waliofika St. Peter's Basilica, Rome, Italy, nikiwa mdogo nimehudunu utumishi kanisani chini ya Muadhama Laurian, Cardinal Rugambwa, na nimemhudumia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu in disbelief, hili kweli ni tamko la TEC, au tamko la Fr. Kitima?. Naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, na kuridhia ile IGA ya DPW, CCM ndio chama tawala na chama pekee cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, kwa kuipiga chini kesi ya kupinga DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?!.

Katika uendeshaji wa nchi yetu, kumewahi kuwepo tuhuma za kitu kinachoitwa "Mfumo Kristo", hata uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, uliwahi kutuhumiwa kujaza Wakatoliki!. Mwalimu Nyerere akamtuma msaidizi wake Bi. Wickens amuhesabie idadi ya mawaziri Wakatoliki kwenye cabinet yake, akawakuta wawili, mmoja wao ni Sir George Kahama, wakati huo Sir George ameisha endelea, ana wake 2!.

Japo Tanzania ni secular state, nchi yetu haina dini na serikali haina dini, ila watu wake wana dini, na dini Kuu mbili ni Wakristo na Waislamu. Ukiangalia development index ya maendeleo na personal development ya watu hawa wawili ni tofauti, kuna mmoja ni more influential kuliko mwingine, hivyo akisema kitu kinasikilizwa na kisipo sikilizwa...

Tukubali tukatae, Kanisa Katoliki lina upper hand kwenye siasa za nchi hii!, si wengi wanajua kuwa kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, na atakaye mfuatia Mama Samia baada muda wake, ni lazima awe Mkatoliki!, je kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.

Zanzibar ilipojiunga na OIC na kwa vile Zanzibar sio nchi, hivyo Tanzania ndio ikahesabika kujiunga na OIC, ni TEC ndio wa kwanza kupiga kelele, Tanzania tukajitoa!, lakini tupo Wakristo Wakatoliki, tuliisupport Zanzibar na kuitaka JMT ijiunge na OIC OIC - Zanzibar kujiunga kivyake vyake

Waislamu walipotaka Mahakama ya Kadhi, na CCM chini ya rais Muislamu, ikawakubalia na kuuingiza hoja ya Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, ni TEC walipiga kelele, Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na ilani ya CCM iliyofuata ya 2015 ambapo ni zamu ya rais Mkristo, hoja ya Mahakama ya Kadhi ikaondolewa kwenye ilani ya CCM!. Tupo baadhi yetu tena ni Wakristo Wakatoliki, tuliwaunga mkono ndugu zetu Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali? na mpaka tukapendekeza Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

Tuambiane ukweli, jiulize, rais angekuwa ni MkatolikinMagufuli ndio ameileta hii DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.

Bwana wetu Yesu Kristo alituasa tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Ki Mungu, jee waraka mzito kama huu, haujachanganya ya Ki Mungu na ya Kaizari?.

Pia Bwana wetu Yesu Kristo alituusia tuwe makini sana na manabii wa uongo, niliwahi kuandika hivi humu Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

Sipingi uhuru wa Maaskofu Katoliki kutoa kutoa maoni yao binafsi kuhusu jambo lolote, lakini maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, kitu ambacho kitawakwaza Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.

Sina tatizo kiongozi yoyote wa dini akihubiri amani, mimi mwenyewe ile 2010, JK alipokuwa na hali mbaya, nimezunguka nchi nzima na Askofu Moses Kulola kuokoa jahazi Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Niliwahi kuuliza maswali haya kuhusu viongozi hawa wa dini
Hitimisho
Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Sauti ya Mungu mwenyewe, kumaanisha Vox Populi is Vox Dei, hii maana yake waraka huu ni sauti ya Mungu wa kweli, na kama hawa Maaskofu Katoliki sio manabii wa uongo, ushauri wangu wa bure kwa Rais Mama Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu wa kweli, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe, Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo tangu Membe alipoupuuza ushauri huu,... (naomba nisimalizie), ila hakuchukua round!.

Hivyo mimi nikiwa ni mmoja wa wana jf wenye kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Nakushauri tuu Mama, pamoja na mema yote DPW waliokutendea during Expo Dubai, and after, kubaliana tuu na ushauri wa TEC, huu ni ushauri Mungu, hili jambo la DPW achana nalo kwa sasa, kisha anzisha upya mchakato wa kumpata a strategic investor wa Bandari yetu kwa kufuata a due process, hakuna strategic investor mwekezaji wa Bandari wa kushindana na DPW!, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, and very honourably.

Paskali.
Rejea za Mwandishi kuhusu DPW na Bandari zetu
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
  8. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  9. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  10. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  11. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  12. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!.
  13. Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
  14. IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
  15. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  16. IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
  17. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
  18. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
  19. Na kufuatia baadhi ya watu wenye akili fupi humu kudhani mimi ni chawa, nawahakikishia mimi sio chawa Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
  20. Chawa hawezi kupandisha bandiko kama hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
 
Tokea lini waislam hitaji lao lilikua shule na hospital
Hili ni tatizo la mtu asiyejua mbele wala nyuma.

Unafahamu kuwa waislamu Tanzania walilazimishwa kutoka katika jumuia ya waislamu (OIC)? unajua kwanini? na bado hapohapo wakatoliki wakachimbiwa mizizi kwa mikataba mizito mizito kati yao na Serikali na huku wakipewa haki ya kupokea funds za kuwasaidia kujenga hayo mahospitali na mashule!

Wewe ni kama mtoto anayeaminishwa kuwa yeye ana akili kuliko mwenzake, na kutokana na udogo wa akili yake na yeye anaamini hivo!
 
Back
Top Bottom