Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Kaka Kama umefuatilia kwa making kuhusu sakata la DP world utagundua wanaopinga hawana shida na uwezo wa Dp world ila shida yao kuwa ni vifungu vya mkataba ambapo kikawaida mkataba unatakiwa uwe win win katika haki na wajibu wa pande zote zinazohusika na huo mkataba Sasa huu mkataba hauko na usawa kwamba Tanganyika inapewa wajibu zaidi huku Dp world akipewa haki zaidi pia mkataba hauweki wazi kikomo cha uhai wake lakini zaidi hauonyeshi ni namna mwekezaji amepatikanaje, atawekeza kiasi gani n.k
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Tokea lini waislam hitaji lao lilikua shule na hospital
 
Kama hiyo ndio thinking na matarajio yako kutoka DPW, basi maaskofu wako sahihi.
Matarajio yangu toka dp world ni mapato bandarini kuwa zaidi ya Mara mbili,na kuchangia bajeti zaidi ya 60%,hicho nilichoandika ni matarajio ya kanisa,kile wanachoona kinakuja na dp world,wao hawajali mapato ya nchi,ukizingatia wanakula Bure kupitia sadaka na fungu la kumi na michango mingine,wanapitisha Bure mizigo bandarini na ruzuku toka hazina kwenda kwenye miradi yao,wanachohofia wao ni yule adui yao mkuu,kuona atapata pumzi
 
Je BANDARI ya Dar es salaam ina chapa ya nani…? TANZANIAAAA na je hao maaskofu ni raia wa nchi gani TANZANIAA? Na DP WORLD nao ni kina nani Waarabu … Basi vya watanzania waachieni WATANZANIA na vya waarabu wapeni WAARABU’
 
Duh!....
 

Ma O level na A level waliosomeshwa na kanisa si ndio hawa wanaotia mikataba ambayo kanisa inakuja kupinga ??

Mahospitali haya tuliyonayo ya kanisa , mbona akina X Speaker, Ndungai bado walipelekwa India kutibiwa ?? hata Jiwe tuliambiwa dakika za mwisho alipelekwa nje pia ?? kuna nini huko Kanisani ??
 
Andaa andiko lingine la kuomba radhi mkuu muungwana akivuliwa nguo huchuntama sasa chuntama omba radhi, 'who the hell is....' unaelewa maana yake omba radhi umewakosea wazee wa baraza

Wazee wa Baraza ndio wa kumwomba radhi Pascal sio pascal wa kuomba radhi
 
TEC wakati wa Magufuli ilifurukuta mara moja tu mwaka 2017 ikiwa chini ya Askofu Ngalelikumtwa wa Jimbo la Iringa. Mimi ni Mkatoliki, nasali kila J2 nikiweza na natoa Zaka na sadaka. Lakini Baraza la Maaskofu wangu ni WANAFIKI.

Mbona hawakuandika kitu wakati Magufuli anaendesha nchi kama familia yake na kuua watu. Hata shambulizi la Tundu Lissu la wazi kabisa hakuna mahali walilisemea
 
Acha kujieleza sana kama mgonjwa wa akili
 
Tokea lini waislam hitaji lao lilikua shule na hospital
Hili ni tatizo la mtu asiyejua mbele wala nyuma.

Unafahamu kuwa waislamu Tanzania walilazimishwa kutoka katika jumuia ya waislamu (OIC)? unajua kwanini? na bado hapohapo wakatoliki wakachimbiwa mizizi kwa mikataba mizito mizito kati yao na Serikali na huku wakipewa haki ya kupokea funds za kuwasaidia kujenga hayo mahospitali na mashule!

Wewe ni kama mtoto anayeaminishwa kuwa yeye ana akili kuliko mwenzake, na kutokana na udogo wa akili yake na yeye anaamini hivo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…