Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Nimekuelewa mkubwa hapo katika hitimisho lako
 
Mkuu, sijui ni kwa nini hujiamini kiasi hicho na kutegemea sana akili za watu wengine? ... Tulipigania uhuru tukiwa na lengo la kujitawala ili tuweze kuendesha mambo yetu wenyewe ikiwemo bandari.

Nikufahamishe tu kuwa wapo watanzania waliosomeshwa kwa ajili ya kusimamia na kuendesha bandari tena tangu enzi za Nyerere, nawafahamu watanzania wanne tena kwa majina na nchi wanazofanya kazi hivi sasa kwenye bandari za kigeni. Mzanzibari mmoja amesomea Gdańsk degree ya kwanza hadi ya pili, hivi sasa yuko Marekani, kama hajastaafu. Kuna wabongo wawili, mmoja yuko Gothenburg-Sweden na wa pili bado yuko Gdańsk -Poland ...

Mbongo wa nne aliyesomea fani hiyo yupo hapo bandarini, bila shaka ameishaathiriwa na ubadhirifu... Hii nchi ni yetu, tuijenge wenyewe jomba. DPW hana muujiza wowote ule unaoweza kuwatoa watu makini kwenye reli!.
 
Ukweli unabakia kuwa sekta ya bandari ya nchi za afrika haina teknolojia, na hizi za kwako ni dhana za hayati JPM za kujidanganya kwamba tunaweza kujitegemea kwa nguvu kazi yetu.

Teknolojia kuwa chini ni tatizo la bandari zetu.

Rasilimali watu yenye uwezo ni tatizo katika bandari zetu

Mtaji mdogo ni tatizo la bandari zetu.

Maaskofu wamepinga uwekezaji lakini hawajaja na suluhisho la hayo matatizo matatu, kuendelea kubakia na utendaji wa bandari wa kizamani ni kuendelea kukwama kiufanisi, sina uhakika iwapo wamejiuliza baada ya kuukata uwekezaji kipi kinachofuata.
 
Mkuu labda ungenipa mifano ya bandari unazodai kuwa zina teknologia ambayo ni ngeni iliyotoka sayari nyingine ili tujadili, vinginevyo naona ni kama tunapiga soga tu.

Bandari ya Dar es salaam inahitaji uwekezaji mkubwa kama uliofanyika kwenye gati ya magari, uwekezaji kama uliofanyika kwenye hospitali ya Muhimbili, ... Taasisi ya moyo na ile ya mifupa....n.k.

Bandari inahitaji Kutengewa bajeti inayotosha kununua vifaa na teknologia, kuwekeza kwenye rasilimali watu na kuondoa mnyororo wa uswahili unaoitwa siasa wakati ni mtandao WA waharifu wa kitaasisi.
 
Brother distance yourself from the ongoing nuisance otherwise you will be stained beyond the cleansing reagent
 
Mi napendaga tu malamri yako wanyumbani!

Ni "mule mule" haiachi kitu wala kukwepesha!

Au wewe ni shushushu flani amaizing mjanja mjanja unayeyanusa mambo yakiwa jikoni kabisa yakipikwa?

Kwenye utabiri wa Ndugai na Tulia, kiukweli mimi nilistaajabu sana!

Pokea maua yako mkuu.
 
Baraza la maaskovu haliruhisiwi kutoa kauli ya kukemea au kuipinga uonevu, unyonyaji na ukandamizaji? Kanisa pia lina kazi ya kutetea haki za wananchi kwa kupaaza sauti linapoona haki zao zinakanyagwa na serikali.
Ni kweli, kanisa lina haki zote kukemea maovu, lakini hapa kwenye waraka huu, kanisa lime dictate terms!. Bunge letu Tukufu ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi, limeridhia, CCM chama tawala, kimeridhia, Mahakama imeridhia. Tamko hili linawaweka Wakatoliki wanaounga mkono DPW, unawaweke kwenye wakati mgumu kiasi gani?.
P
 
Kama Wananchi hawasikilizwi, kuna kosa gani Kanisa likasaidia kupaza sauti Mr Paskali, au wewe kubadili Sheria za Nchi ili Mwarabu afaidi Nchi yetu wewe umeridhika?
Hakuna kosa lolote kwa kanisa kusaidia kupaza sauti, ila hili tamko lina amri ndani yake!. Kuhusu kubadili sheria to accommodate DPW, this is inevitable, sisi waona mbali, hili tulilisema toka day one tulipozitunga hizi sheria za ajabu Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?
P
 
Unajuaje kama Baraza limeisaidia Serikali kwa tulipofikia?
Najua sana jinsi kanisa Katoliki livyoisaidia serikali, Wakatoliki ni raia wema, na kanisa Katoliki linasaidia sana kwenye utoaji wa huduma za jamii, afya, elimu na ujasiriamali na misaada kibao, lakini hili tamko ni too strong, badala ya ku beg, lina dictates!.
P
 
Chukua nakala ya kiingereza ndio iko kwenye level yako Learned Brother. Kingine ambacho pia unatakiwa kufanya ni kupitia sala za wakatoliki uone kama kuna inayoomba...nielewe we are not beggars.
 
Huna akili 🚮
 
Umesoma vizuri Tamko brother? Kwani Maaskofu hawana haki ya kulinda Rasilimali za Taifa hili.
Maaskofu Katoliki wana haki ya kulinda rasilimali, kama raia wengine wowote, ila tamko hili lina dictates with no option of choice!, ni kama amri fulani hivi!. Huwezi kumuamrisha rais wa JMT!
Tunasubiri na Bakwata nao waunge mkono.
Leo ELCT leo wameunga mkono, CCT wanafuatia, at the end of the day TEC itapuuzwa!.
Bikira Maria ndiyo mlinzi wa Taifa letu.
Unajua baada ya kumzaa Yesu, hiyo B ilitolewa na alizaa watoto wengine na mumewe Yosefu?. Whats a point kuendelea kumuita B?
Kanisa Moja Takatifu la mitume
Hapa tuko pamoja,
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
Mwumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu,mwana wa pekee wa Mungu.
Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu,mwanga kwa mwanga,Mungu kweli kwa Mungu kweli
Nasadiki kwa Kanisa moja,Takatifu Katoliki la mitume
Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.
Na uzima wa milele ijayo.

Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…