Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

bunge unalosema limejadili, ni bunge la akili za musukuma na kibajaji na wengine, bunge ambalo halina maslahi ya wananchi, pamoja na bunge kupitisha, wale wa mtaani waliowapeleka pale hawajakubaliana nao, wananchi wamekataa hivyo walichokublai bunge sicho kile walichokitaka wananchi wao. ukisema who the hell is TEC, hilo ni kundi la maaskofu wanaowawakilisha na kuwaabudisha wakatoliki zaidi ya milion 10 hapa Tanzania ambao ni wapiga kura, wakiona uozo wewe ni nani kuwazuia wasiwasemee waumini wao? serikali yetu ni ya kiimla kwamba chochote inachoamua ni sahihi kisipingwe? kwani ni mangapi yamepingwa wakalazimisha tukaishia kulipa mamia ya mabilioni kama fidia hapo mbeleni? unatafuta cheo?
 
Tanzania yetu ni Secular Democracy tukemee kwa nguvu zote Agenda za siri zitakazotugawanya.

Tukiichoma hii Tanzania kuna watu watakimbilia Vatican na wengine Saudia sisi akina yakhe tutaenda wapi yarabi?
 

Paschal Mayalla,

1. Taasisi zote za kijamii (social institutions) unazozifahamu kama vile elimu, tiba, familia, dini, dola, na uchumi, ni kwa ajili ya kumhudummia binadamu.

2. Hivyo, masuala ya elimu, tiba, familia, dini, dola, na uchumi yanaunda "both/and senario" na sio "either/or senario."

3. Hili kosa lako linaitwa "Either-Or fallacy" au "False dilemma fallacy" au "bifurcation fallacy" au "black-or-white fallacy" au "the excluded middle fallacy" au "false dichotomy fallacy."

4. Pia nashauri tujadili maudhui ya tamko badala ya kujadili waleta tamko.

5. Wewe ni mwanasheria na hivyo unaelewa umuhimu wa ukuta unaotenganisha ujumbe na mjumbe.

6. Kwa kisukuma unachofanya kinaitwa ARGUMMENTUM AD HOMINEM.

7. Acha kudhalilisha taaluma. Sio poa.

Dawati la Mama Amon,
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga.
 
watake wasitake maoni yameshatolewa na huo ndo msimamo wa wananchi walio wengi. imeenda hiyo.
 
Mkuu Paskali.

Vatican ni dola, inatawala kupitia mfumo usioonekana kwa macho.

Waraka wao ni red alert. Just skip to the next page
 
Sijui kbs mambo ya dp world lakini naomba nichangie kwenye hili suala la dini na siasa.Si kwa waislamu wala kwa wakristo wala budha au nani: ni hivi Mungu anatakiwa kutukuzwa katika eneo lolote la maisha iwe binafsi au kijamii.Kamwe usitenge kwamba hili ni la Mungu hili sio.
 
Haya mambo ya kuchanganya vitu CCM muanze kuwa mfano kuyakataa.

Mfano jana huyo mama yenu anafanya mkutano wa CCM kwenye ikulu iliyojengwa kwa kodi za wananchi totally absurd.

Hapo unakuta gharama za kuandaa mkutano kulipana posho zinatokana na kodi za wananchi.

Pili issue ya hao maaskofu kutoa msimamo wao sio kama kuna tatizo kanisani mbali ya kuwepo dini hata wanasiasa wapo na ndio maana hata najua unafahamu serikali ina shughuli zake na watu wake kwenye hizo nyumba zote za ibada.
 
icho kibandiko kwamba tusichanganye dini na siasa ndio uchochoro wa kutafunia pesa wanaccm, hawataki kusemwa. kwenye majukwaa wanawaalika wawaombee, mashule yao wanayataka, mahospitali wanayataka, ila wakikosea hawataki kusemwa ati unachanganya dini na siasa, msiwe mnawaalika basi hata kwenye hizo hafla zenu, ninyi ndio wa kwanza kuchanganya dini na siasa.
 
Ehee! Tujadili hoja au tujadili watu?
 
Kuna jipya gani unaposema wasichanganye dini na Siasa?

Mara ngapi JPM alifanyia Siasa Msikitini ama Kanisani

Hujaona ile kauli ya kuhusu Corona hayati aliitoa akiwa Kanisani.

Hujaona Mama Samia anafanya Siasa Kanisani ama Msikitini wakati ule wa kufutarisha?

Kanisa lina wakilisha Wananchi vile vile Msikiti.

Kwahiyo kutoa maoni yao kama Jumuiya inayowakilisha Mamilioni ya Watanzania sidhani kama ni dhambi.

Kumbuka Kanisa/Msikiti imara huzalisha Viongozi Imara.
 
Pascal Naamini wewe ni Mkristo na umesoma biblia, unajua vyema kazi walizofanya manabii kwa kusaidia jamiii kuishi vizuri na pia unafaham namna mitume na manabii kama akina elisha, elia walivyofanya kazi na watawala enzi hizo kwa maani waliwatia moyo watawala kupigana vita ilipobidi na pia waliwakosoa waziwazi pia pale walipoona mambo hayako sawa , sasa napata shida kama ufahamu wako kwa HAKI umekutuma kuwaza hivyo ulivyoandika ukiwa huru kabisa kifikra. Naukumbuke Tanzania inaamini katika MUNGU refere viapo vyetu na mombu yetu Bungeni, hivyo hutuwezi kujitenga na Nguvu za Mungu katika kujenga jamii bora ki utawala, Iweje sasa tushangae walioamiwa na Mungu wakituasa jambo?

Kwanini tuwashakie watuonya juu ya mienendo yetu ya kiutawala, kwani mtu akiiba au akafanya udanyifu mahali hiyo sio dhambi?. Tusiwafunge mikono watumishi wa Mungu kwa kuwapa mipaka, sisi ni jamii yao na wanahaki tudurudi hasa pale wanapofanya kwa haki.
 
Who the he'll are TEC!?? Wewe kweli mkatoliki kobe. Unaifahamu Canon law of infallibility? Kwa ufahamisho tu hizi ni sauti za watanzania milioni 20 wakatoliki. Hili tamko tutalikuta kigangoni jumapili. Ni utii tu.
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Acha uzwazwa kwa mkataba kama ule wa kissenge acha waseme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…