Mpenzi wangu amekiri kunisaliti, ameomba msamaha natafakari maamuzi ya kufanya

Mpenzi wangu amekiri kunisaliti, ameomba msamaha natafakari maamuzi ya kufanya

Hamekusaliti vipi wakati bado hujamuoa, ndoa ndio sehemu pekee kwenye kiapo cha kutosalitiana

Lakini kwenye mahusiano we msamehe tu maana yupo kwenye kipindi cha kuchagua yupi sahihi kwake inawezekana huyo jamaa ndio akaja kumuoa

Mapenzi usiyachukulie serious sana maana utaumia kila siku
Umemaliza kila kitu hapa. Nakazia.
 
Labda nichangie kidogo.
Inategemea mna malengo gani.
1. Ikiwa ni urafiki wa kufurahishana na kukata mihemko ya ujana msamehe maisha yaendelee

2. Ikiwa mnapanga kuoana mnajitesa bure wote mmeharibu.
Ndoa na mapenzi ya dhati msingi wake ni uaminifu na ninyi wote 2 mmeutikisa huo msingi.
Mkilazimisha mtateseka bure.

Ikiwa jibu lako ni namba 1. Msamehe muendelee kila mmoja akisubiria mwenza sahihi.
Ikiwa jibu lako ni 2.
Msamehe lakini anza kujipanga kujionfoa taratibu kwenye kifungo hicho utafute mwingine.
Uchumba hausuluhishwagi mkuu ukilazimisha mnajimaliza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawezi kukuelewa hata.
 
Nipo kwenye mahusiano na huyu dada kwa almost mwaka mmoja.

Wiki ilopita kaenda site nje ya mkoa na wafanyakazi wenzie maana nature ya hiyo kazi wengi wanaomzunguka ni wanaume, wanawake wako wawili tu kati ya watu 30.

Okay, alivyorudi niligundua alinisaliti akiwa huko site, aligoma kunambia ukweli lakini nikamwambia tuachane kama anataka turudiane aniambie ukweli, ee bana ee akafunguka ni kweli alinisaliti na mmoja wa wafanyakazi wenzie sababu akanambia alipitiwa tu.

Amelia sana nimsamehe hatorudia tena amekiri kosa na anahitaji msaada wangu. Nimempa siku nne nmefikirie namsamehe au laa!

Japo huyu dada siishi nae anakaa geto na mwenzie huyo wa kike, na kwa maelezo yake ametembea na huyo jamaa mala mbili tu,ile siku na kabla ya hapo.

Umri wa huyu dada ni miaka 22, mimi 27 mi mwenyewe pia namsaliti mara kibao na nina wanawake wengine wawili na ashanifuma mara moja akanisamehe. Nimeongea haya ili niwape picha kamili ili mtoe ushauri kulingana na yeye na mimi pia.

ASANTENI.
Kwa suala la mahusiano,wewe ndo wakuamua! Unatakiwa uskilize moyo wako tuh. Mpaka hapo huyo mwenzako anaonekana sio mtu wa kukumbushia makosa! Coz nmeona hapo umesema na wewe tayari kumsaliti Mara mbili Ila mliongea labda yakaisha easy,na wewe umemwambia kua muachane kisa amekusaliti but anaomba tuh msamaha Hilo ni sahihi pia. Kwenye suala la mahusiano ukiamua "kuingia" we "ingia" na ukiamua "kutoka" we "toka" yani shikilia msimamo wako.
 
Wewe una madem zaidi ya 3, na hakuna kati ya hao uliemuoa sasa huko kuchapiwa kunakuumaje mkuu, yani unataka uwamiliki wote 4 na uwatimizie kila kitu utaweza??

Stress za kijinga namna hiyo huwa mnajitaftia tu, ndio maana nkakwambia kama una malengo nae unaweza kuumia ila kama ni wa kupita unaumia nini sasa??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hata haelewi nn anataka.
 
Sisi wanaume kuchepuka ni kawaida hiyo ni general rule, ila mwanamke akichepuka hilo kosa kubwa sana halina exception, achana naye huyo
Kanuni hii iko ktk kifungu au ibara gan? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
dem ananisikiliza na kuniheshimu,vip apo niendelee nae?
Umejuaje Kama anakuskiliza na kukuheshimu? Unakuta Apo anang'ang'ania usimuache coz anajua vizuri kua Kuna vitu unampatia wewe na kwa mwingine hapati na Kuna anavipata kwa hiyo mwingine na kwako hapati,ko unakuta anaigiza tuh,maaana Hawa washkaji Hawa they are 5 minutes earlier.
Iko ivo ndugu. Sema kikubwa usiruhusu mwanamke aitawale akili yako katika umri huu,bado tunasafari ndefu ya kwenda kua focussed tuh.
 
Mkuu,ukichapiwa,ukijua na kuthibitishiwa na kuombwa msamaha samehe.Ila kuhusu kuendelea na uhusiano hakikisha uko tayari kukaa katika uhusiano ambao akichapwa tena na tena na tena na tena na tena na tena na tena na tena bado utakuwa jasiri wa kumasamehe.Pembeni ya hapo ama utamtesa huyo mwenzio kwa sababu ya kuanguka kwake au utateseka wewe kwa kukaa na mtu ambae humuamini.

Mpenzi kutoka nje ni jambo ambalo lipo hata hivyo kumvumilia na kukubaliana na hio hali inahitaji umpende zaidi ya unavompenda sasa hivi
 
Sasa wote ni wasaliti, na alikufuma akakusamehe kwahyo nawee umsamehe ili iwe sawa sawa,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
mwanamke akisaliti ni mbaya kuliko sie vidume,huenda anampenda huyo jamaa ndo kagoma kunipa namba ya uyo bwana wala hataki kumpigia tukiwa wote ili amwambie kuwa ana mtu anayempenda
 
Nipo kwenye mahusiano na huyu dada kwa almost mwaka mmoja.

Wiki ilopita kaenda site nje ya mkoa na wafanyakazi wenzie maana nature ya hiyo kazi wengi wanaomzunguka ni wanaume, wanawake wako wawili tu kati ya watu 30.

Okay, alivyorudi niligundua alinisaliti akiwa huko site, aligoma kunambia ukweli lakini nikamwambia tuachane kama anataka turudiane aniambie ukweli, ee bana ee akafunguka ni kweli alinisaliti na mmoja wa wafanyakazi wenzie sababu akanambia alipitiwa tu.

Amelia sana nimsamehe hatorudia tena amekiri kosa na anahitaji msaada wangu. Nimempa siku nne nmefikirie namsamehe au laa!

Japo huyu dada siishi nae anakaa geto na mwenzie huyo wa kike, na kwa maelezo yake ametembea na huyo jamaa mala mbili tu,ile siku na kabla ya hapo.

Umri wa huyu dada ni miaka 22, mimi 27 mi mwenyewe pia namsaliti mara kibao na nina wanawake wengine wawili na ashanifuma mara moja akanisamehe. Nimeongea haya ili niwape picha kamili ili mtoe ushauri kulingana na yeye na mimi pia.

ASANTENI.
Mungu uwa anakupatia unayeendana na kufanana nae.
Huwezi kuwa sokwe ukaoa ng'ombe
 
Hata kama ukimsamehe, Huyo jamaa anae fanya nae kazi ataendelea kumla tu maana mpaka saivi kashamla mara mbili.

Je,unahisi wameishia hapo?
 
Back
Top Bottom