Mpenzi wangu kagoma kuhamia imani yangu ili tufunge ndoa

Pole sana mkuu
Muweke wazi failure to join you na ndoa hakuna!

Komaa wewe mwanaume, usikubali eti mfunge ndoa geresha then kila mtu afuate dini yake..USIKUBALI
 
Kwanza tafuta msabato mwenzako.

Pili mhubiri au mfundishe mwenzako ajifunze imani yako amjue Mungu na si kwasababu yako maana unamtaka akugeuze mungu.

Tatu: jiandae kuishi na huyo mwanamke maana anaonesha anamsimamo gharama zao ni kubwa.

Nne; fungeni ndoa bomani mbele mcha Mungu wa kweli atamvuta mwenzake.
 
Haya mambo mimi pia sikujua kama mpka wakristu huwa tunabaguana.. mpka majuzi hapa nilipokutana na mwanamke wa kisabato..
Akaanza kuniletea blah blah nyingi sijui imani.. nikaona hapa hamna kitu kama mapema hivi masharti yashaanza.
 
Aliye-propose ndoa ndiyo abadilike.
Kama yeye binti alikuvisha pete akaomba umuoe, basi itabidi abadilishe dini. Kama ni wewe ndiye ulimvalisha pete na kuomba umuoe, basi badilisha dini.
Unapanda basi halafu unamuomba konda atoe nauli?
Mweeh!
 
Mkuu! Kama umeshakula tunda na anazngua, piga chini'
 
Muwe mnawekana wazi mapema kuliko kufika mbali huko afu mnaanza kuhangaishana
 
Kwani wewe unasemaje
 
With all due Respect Wasabato vs Madhehebu mengine always huwa kuna utata linapokuja swala la ndoa....
Wasabato wala hawana tatizo lolote maana wamesimama kwenye misingi ya imani yao inayowakataza kuoa au kuolewa na mtu wa imani nyingine, tatizo ni watu wa madhehebu mengine kutaka kulazimisha kuoa au kuolewa na msabato bila kuwa wasabato.

Kwa uchunguzi wangu mdogo niligundua yapo madhehebu mengi tu yenye msimamo kama huo (ndoa ni kwa watu wa imani moja tu), lakini wahusika wanaamua kupuuzia (wanakiuka kimakusudi imani zao) hivyo wanaoana na kuozeshwa. Na huu ndio upuuzi mkubwa.
 
Na ndio maana nmesema Wasabato vs Madhehebu mengine kwa maana haya mengime hizi changamoto ni ndogo ama chache kabisa huwa hakuna shida linapokuja swala la ndoa...

Wasabato wana misimamo yao reason why ni ngumu kuchangamana na madhehebu mengne ambayo hayana shida kwenye kuchangamana
 
Kwahyo by that logic mwenye msimamo Na Imani yake Na asiye Na msimamo Na Imani yake,,who is better?
 
Kwahyo by that logic mwenye msimamo Na Imani yake Na asiye Na msimamo Na Imani yake,,who is better?
Am not here to judge who is better than the other Mkuu...

Nmezungumzia uhalisia wa mahusiano baina ya pande hzi mbili za madhehebu.
 
Wewe Mnyakyusa mapenzi yanakusumbua sana,

Embu achana nayo ufanyr mengine
 
Sabato-Wana amini katika asiku-jumamosi
Katoliki-wana amini bikira Maria na siyo siku wala Yesu.
Hamuwezi kuwa kitu kimoja, nakushauri mfunge ya kiserikalai muendelee kulana mzigo kihalali.
 
Naomba uje nyumbani kwetu kwa ajili ya kula pilau nililopika mwenyewe. Kuna juice isiyotiwa maji wala sukari. Karibu sana.
 
Reactions: BAK
Acha ujinga,mapenzi ni mambo ya moyoni,oa kila mtu abaki na dini yake,haya mambo ya kubadilisha dini,ni ushamba,na ufinyu wa uelewa
 
Kwamba amhubiri amjue Mungu, kwaivo Catholic hawamjui Mungu?
 
Sjawai kuona kama imani ya mtu inaweza kuwa kikwazo eti mshiishi kama wanandoa, mfano hai wa familia yangu (baba na mama) walioana dhehebu tofauti wana miaka 40+ kwenye ndoa sasa sioni shida, dada angu mkristo shemeji muislam miaka 15 sasa wanaishi vizuri, mimi na mume wangu dhehebu tofauti msabato+Catholic hatujawai gombana kisa dhehebu, mna complicate mambo utafikiri kupitia dini mtaishi uzima wa milele.....na akati maisha ya mwanadamu ni miaka 70woooiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…