Mpenzi wangu kagoma kuhamia imani yangu ili tufunge ndoa

Mpenzi wangu kagoma kuhamia imani yangu ili tufunge ndoa

Baada ya safari ndefu ya mahusiano tumefikia hatua ya kufunga ndoa ila binti ni mkatoliki mimi msabato mpaka sasa hatujafikia mwafaka nani amfuate nwenzie japo kisheria tumezoea mwanamke anamfata mwanaume lakini yeye hataki na hayupo tiyali kuhama roma.
Kwani wanaona wanafuata dini au mapenzi kati yao. Tutoke kwenye fikra za kizamani. Dini ni Imani yako sio yake kila moja wetu ana imani yake. Kama kwako dini ni cha kwanza basi usimfuate asiye wa imani yako au mbadili imani kwanza ndio penzi lifuate
 
Ndio maana ndoa nyingi sana za siku hizi zinavunjika ovyo ovyo tena mapema sana.
Kwanza kabisa hayo mambo ya imani mlitakiwa kuyaweka sawa sawa mwanzoni kabisa mwa uhusiano wenu na sio muda huu wa kufunga ndoa.
Zanzibar-ASP heshima kwako!

Umeongea vizuri sana hapa,kuhamishana kiimani kwa sababu ya ndoa ni mtihani sana maana wakati mwengine hufikia wale waliokubaliana mwanzo kukengeuka na hapo sasa hufikia hata kuwapoteza watoto kiimani ni vizuri kila mmoja atafute wa imani yake kama kweli anataka amani ya maisha.
 
Hebu achana na ujinga nenda kaoe, unaoa dhehebu au mke!? 😳😳😳

Baada ya safari ndefu ya mahusiano tumefikia hatua ya kufunga ndoa ila binti ni mkatoliki mimi msabato mpaka sasa hatujafikia mwafaka nani amfuate nwenzie japo kisheria tumezoea mwanamke anamfata mwanaume lakini yeye hataki na hayupo tiyali kuhama roma.
 
Ila pia si kuna ndoa za bomani kila mtu anabak na imani yake na maisha yanaendelea
 
Hello ndugu unaweza kunitajia kifungu cha sheria kinachosema mwanamke ndie humfuata mwanaume..?
Nasubiri boss nami nijifunze
Wewe na demu wa mtoa mada akili zenu zinafanana!

Acheni ujuaji
 
Mwanaume unaandika tiyali?
Hii pia huchangia demu kukugomea
 
Baada ya safari ndefu ya mahusiano tumefikia hatua ya kufunga ndoa ila binti ni mkatoliki mimi msabato mpaka sasa hatujafikia mwafaka nani amfuate nwenzie japo kisheria tumezoea mwanamke anamfata mwanaume lakini yeye hataki na hayupo tiyali kuhama roma.
Mfuate mwanamke wako Roma ndio baba wa makanisa baadae Ruther akajitenga, Anglican nao wakajitenga na mama mmoja nae akajitenga akaanzisha dhehebu la sabato

Kwa hiyo we we ukirudi Roma ni sawa maana umerudi katika asili yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna Mungu wa wasabato basi tungeishi maisha ya tofauti sana....hata pumzi, riziki, pesa, utajiri wangepewa wasabato tu kwa sababu ndo watu wa Mungu!
Issue sio Mungu tofauti ila ni vile waroma wanabadilisha maandiko kwa manufaa yao tofauti na asili ya biblia
 
Issue sio Mungu tofauti ila ni vile waroma wanabadilisha maandiko kwa manufaa yao tofauti na asili ya biblia
Hata waliaoanza kuiandika waliandika kwa manufaa yao, au umesahau ni maandiko tu yaliyoandikwa na mzungu? Kwan baada ya Catholic kubadili maneno ya biblia Mungu amewapa adhabu gan au bado wanaishi duniani tu kama wasabato
 
Kwani nyinyi wote sio wakristo? 🙄au bibilia zenu mnazosoma ni tofauti na maandiko ni tofauti??
 
Yawezekana hukusoma maandiko vyema, nini tafsiri ya mke na mume kuwa mwili mmoja?. Sara na Hajiri walikuwa wake wa baba wa imani Ibrahimu, na vipi ndoa ya bomani,kimila,na dini?. Wewe ni dhahiri unaubaguzi hata vitabu takatifu vinakukana. Hujui ndoa ni kitu gani. Angalia mwishowe utapata mke mwenye tabia Kama za mke wa Ayubu; hapo akili itakukaa sawa. Nyie ndio msio changamana na wasamaria na YESU alisha pata midhihani ya aina ya watu kama wewe pale kisimani.
 
Hello ndugu unaweza kunitajia kifungu cha sheria kinachosema mwanamke ndie humfuata mwanaume..?
Nasubiri boss nami nijifunze
Kwa tz hakuna ila India mwanamke ndie anae toa mahari kifungu hicho hata India hakuna wanacho fanya ni desturi yao Kama ilivyo tz ni desturi si sheria.
 
Acha usenge wewee nendeni mkafunge ya bomani kama nako hataki,Achana na hiyo takataka
 
Back
Top Bottom