GE2025 Mpina ahamia rasmi ACT Wazalendo, kumvaa Rais Samia Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3432229

DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.

Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.

Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.

Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.

Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.

Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.

“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma >> Pre GE2025 - 2025 CHADEMA kumsimamisha Luhanga Mpina?
Ila CCM wahuni sana
 
Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!
Hilo halina ukweli, John Cheyo aliwahi kuwa na ndoto kama hiyo, ameishia wapi?
Wasukuma si watu wa kukulupuka na ukabila kama ilivyo kwa baadhi ya makabila.
 
Cheyo kipindi kipi!!?

Kwa Sasa Kanda ya ziwa hasa jpm inakitaka kiti kuliko nyakati zote zile!
 
Jicho la tofauti!

The state wameanza kutengeneza matishio ya KITI Cha urais ndani ya ccm kupitia Kanda pendwa!

Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!

Ni hatari sana!

Tena kama watafanya coalition ya kisiasa kwamba ACT isimamishe mgombea urais Chadema isimamishe wagombea wengi ubunge halafu kina Lisu na heche wamsapoti mpina plus kina josephat Gwajima!!!

Wasukuma na wanyamwezinwapo Hadi Zanzibar!!

Hesabu kali!!

KAZI na utu tunasongambele!
SHIDA ya wasukuma huwa awapigi kula MTU huwa ni ccm TU man inaonekana BADO huja wajua HAO WATU

Kwishaaaaaa
 
Angegombea Ubunge ingekuwa realistic kuweza kushinda anyway kama anachotaka ni kuweza kupata uhalali wa kuongea sio mbaya; sababu nchi hii unaweza ukashindwa kuongea lolote eti sababu sio mwanachama wa Chama fulani au Chama chako kukufukuza sababu tu una fikra tofauti....
 
Mpina ana kura zote za Kanda ya ziwa na kati.maana huko Samia hawamtaki kabisa hata kidogo
 
Zitto kamnunua Mpina, ili apate ruzuku iliyonona inayotolewa kulinga na idadi ya kura za uraisi...

Kafanya alichofanya mbowe 2015....MPINA AMEKWISHA KISIASA!...MAANA AMEHARAMISHA MAGEUZI YA KWELI ALIYOKUWA AKIYAPAMBANIA AKIWA CCM...

ZITTO TARGET YAKE NI RUZUKU TU!... Na anajua mpina atapewa kura nyingi mno! Hasa kanda ya ziwa......ILA HAWEZI KUTANGAZWA NA TUME!
Ona akili zilizojaa MAVI kama hizi...leo ndio mmejua alikua anapambania mageuzi ya kweli? By the way kwni saivi baada ya kuondolewa kimabavu kisesa, hivi Sasa anapambania akiwa na cheo Gani hapo ccm?
 
Cheyo kipindi kipi!!?

Kwa Sasa Kanda ya ziwa hasa jpm inakitaka kiti kuliko nyakati zote zile! we unaelewa wapigakura hupigia mtu na chama pia.
Si rahisi kwa chama ambacho hakijajijenga, kuimarika na kukubalika kishinde kirahisi hivyo.
Na pia ushindi ni zaidi ya urais.
Unaweza kushinda urais na wabunge 30, kwa Katiba tuliyonayo rais wa aina hiyo hatomaliza hata mwezi mmoja madarakani.
 
Jicho la tofauti!

The state wameanza kutengeneza matishio ya KITI Cha urais ndani ya ccm kupitia Kanda pendwa!

Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!

Ni hatari sana!

Tena kama watafanya coalition ya kisiasa kwamba ACT isimamishe mgombea urais Chadema isimamishe wagombea wengi ubunge halafu kina Lisu na heche wamsapoti mpina plus kina josephat Gwajima!!!

Wasukuma na wanyamwezinwapo Hadi Zanzibar!!

Hesabu kali!!

KAZI na utu tunasongambele!
Unaona visivyoonekana.
 
na hapa ndipo ccm wanatuweza watanzania, hype ya 'no reform no election' imejifia sasa wametupa track 2 tuhangaike nazo i.e mpina + polepole.
 
View attachment 3432229

DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.

Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.

Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.

Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.

Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.

Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.

“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma >> Pre GE2025 - 2025 CHADEMA kumsimamisha Luhanga Mpina?
 
Attachments

  • 1749448169920.jpg
    1749448169920.jpg
    235.5 KB · Views: 31
Huyo hawezi na isitoshe Dorothy Temu tayari alikwisha pitishwa na kugombea Urais kupitia ACT!
Upinzani kwa maigizo ndio wenyewe

Wazungu kuelewa siasa za Tanzania watasubiri sana tu

Maigizo ya Siasa watanzania tunashika nafasi ya kwanza duniani
 
Back
Top Bottom