GE2025 Mpina ahamia rasmi ACT Wazalendo, kumvaa Rais Samia Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT

Sioni kosa lolote, mana ACT hawana focus ya uraisi kwa sasa ni tofauti na Chadema mana wao walikuwa wapo kwenye position ya ku challenge uraisi.
 
Mpina kitambo kageuka Mhuni, kuna Uzi humu WA jinsi aliyokuwa anatumiwa na wenye viwanda vya sukari kwenye sakata la vibali vya uigizaji sukari nje....
Anatembea na price tag, mwenye dau kubwa anajichukulia kivyake, hapo kuna sinema imetengenezwa!
 
Upinzani wao si wanaona kuwa yeye ndie jabali la siasa kama Membe na Lowassa?

Wamchukue tu Upinzani

CCM hatumhitaji

Ruksa wamchukue

Haki yake ya kidemokrasia kwenda ACT wazalendo kugombea cheo chochote hata ujumbe wa nyumba kumi
 
Chadema hawamo mwanabodi, walikataa kushiriki
Sisi ccm wenye akili timamu kama Mzee wasira hatuwezi ingia kwenye uchaguzi bila chadema ili kuepuka sarakasi za COVID -19 ambacho ni kirusi kilichoondoa uhalali wa Mama mkubwa kugombea Hadi akalazimisha!!

KAZI na utu tunasonga mbele!
 
Hata hivyo ACT ilikosa mgombea doroth na kithemi chake mdomoni kile angeweza kweli na hakubalic kitaa
 
Amekurupuka
Mpina ni Bernad membe wa 2020 hapo ACT mkuu!!

Ni code iliyotengenezwa!na watakaomfuata ni wale waliokatwa kwenye ubunge na wenye hasira na mtia Nia wa CCM!

Uso wa January makamba unasema mengi kama akimuunga mkono Mpina aiseh anaweza shusha pdf za hatari Kwa mtia Nia wa kijani fc!!

KAZI na utu tunasonga mbele!
 
Eti atamvaa Samia kwenye uchaguzi mkuu, kwa tume ipi ya uchaguzi?. Achezi kutufanya ss watoto..NRNE nyie mamluki ya ccm
 
Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT
Akigombea Urais huyo naenda kuifuata Kadi yangu ya kupiga kura Dodoma napiga kura ikifika October
 
reforms ndio kitu cha msingi kukabiliana na chama tawala .Kama ni kweli mpina anataka aingie ikulu mapema asubuhi ahimize reforms alafu CHADEMA nayo iridhie wafanye collision ,I tell you, saa sita mchana CCM inakalishwa chini . Sasa kwa mazingira ya uchaguzi jinsi yalivyo kuwa kwa chaguzi zilizo pita huku kitaa hakuna hata mwenye vibes labda kwa makada kindaki ndaki wa CCM ,nje ya hapo wengi no reforms no election hili somo limeeleweka vizuri .
 
Jicho la tofauti!

The state wameanza kutengeneza matishio ya KITI Cha urais ndani ya ccm kupitia Kanda pendwa!

Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!

Ni hatari sana!

Tena kama watafanya coalition ya kisiasa kwamba ACT isimamishe mgombea urais Chadema isimamishe wagombea wengi ubunge halafu kina Lisu na heche wamsapoti mpina plus kina josephat Gwajima!!!

Wasukuma na wanyamwezinwapo Hadi Zanzibar!!

Hesabu kali!!

KAZI na utu tunasongambele!
chadema imefungiwa kufanya siasa wewe unaishi wapi
 
Angegombea ubunge kule kule kwao angepata Ubunge asubuhi tu ila kwa ishu ya Urais atapata upinzani mkubwa sana..
 
View attachment 3432229

DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.

Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.

Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.

Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.

Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.

Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.

“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma >> Pre GE2025 - 2025 CHADEMA kumsimamisha Luhanga Mpina?
Jamaa anaonekana ana upwilu knoma 😄
 
Amefanya Maamuzi ya kukurupuka.
 
Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT
Sio chadema peke yake!.
Mwaka 2020 Bernard Membe aliingia ACT Wazalendo na kugombea urais na baadae alirudi CCM.
 
Back
Top Bottom