Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT
Upinzani wao si wanaona kuwa yeye ndie jabali la siasa kama Membe na Lowassa?Mpina kitambo kageuka Mhuni, kuna Uzi humu WA jinsi aliyokuwa anatumiwa na wenye viwanda vya sukari kwenye sakata la vibali vya uigizaji sukari nje....
Anatembea na price tag, mwenye dau kubwa anajichukulia kivyake, hapo kuna sinema imetengenezwa!
Sisi ccm wenye akili timamu kama Mzee wasira hatuwezi ingia kwenye uchaguzi bila chadema ili kuepuka sarakasi za COVID -19 ambacho ni kirusi kilichoondoa uhalali wa Mama mkubwa kugombea Hadi akalazimisha!!Chadema hawamo mwanabodi, walikataa kushiriki
Mpina ni Bernad membe wa 2020 hapo ACT mkuu!!Amekurupuka
Daah hii nchi na wanasiasa mmhh
Akigombea Urais huyo naenda kuifuata Kadi yangu ya kupiga kura Dodoma napiga kura ikifika OctoberKosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT
Halafu ushindi wake utatangazwa na tume gani?Akigombea Urais huyo naenda kuifuata Kadi yangu ya kupiga kura Dodoma napiga kura ikifika October
Ya Chura kiziwi na boss wake Mr. BORN TOWN unaweza ukamuita Vito Corleone, the Godfather himselfHzapafu ushindi wake utatangazwa na tume gani?
chadema imefungiwa kufanya siasa wewe unaishi wapiJicho la tofauti!
The state wameanza kutengeneza matishio ya KITI Cha urais ndani ya ccm kupitia Kanda pendwa!
Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!
Ni hatari sana!
Tena kama watafanya coalition ya kisiasa kwamba ACT isimamishe mgombea urais Chadema isimamishe wagombea wengi ubunge halafu kina Lisu na heche wamsapoti mpina plus kina josephat Gwajima!!!
Wasukuma na wanyamwezinwapo Hadi Zanzibar!!
Hesabu kali!!
KAZI na utu tunasongambele!
Reforms zitafanyika na watarudi mzigoni!wanaccm makini wanajua umuhimu was mpinzani makini kushiriki uchaguzi!chadema imefungiwa kufanya siasa wewe unaishi wapi
Jamaa anaonekana ana upwilu knoma 😄View attachment 3432229
DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.
Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.
Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.
Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.
Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.
Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.
Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.
“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.
Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.
Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma >> Pre GE2025 - 2025 CHADEMA kumsimamisha Luhanga Mpina?
Nini ambacho hakiwezekani?Huyo hawezi na isitoshe Dorothy Temu tayari alikwisha pitishwa na kugombea Urais kupitia ACT!
Amefanya Maamuzi ya kukurupuka.View attachment 3432229

Sio chadema peke yake!.Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT