Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Haya maswali ya Mpina kuna dalili yakazimwa nyie subirini mtaona.
 
Hapa ndipo pakudiscuss. Wanakwepa hapa tu
 
Hapa ndipo pakudiscuss. Wanakwepa hapa tu.
Ni hilo tu. Asante mheshimiwa jaji
 
Sema wewe unataka nini?? Usitujumuishi kwenye upumbavu wako.
 
Mhe Mwigulu Nchemba Waziri wa fedha wa Tanzania, leo akijibu maswali bungeni ameshindwa kufafanua tofauti ya TRAT &TRAB kwenye uchumi, jambo lilomfanya spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania kuingilia Kati na kumtaka atolee ufafanuzi, ghafla Waziri wa fedha (PhD) akashikwa na kigugumizi na kushindwa kufafanua vizuri, hali iliyoibua shamra shamra za hapa na pale Bungeni.

Ikumbukwe Waziri wa fedha ana PhD ya Uchumi.

Your browser is not able to display this video.
 
Hata mfanyabiashara wa Kariakoo aliyewahi kukadiriwa vibaya kodi anazijua na anaweza kueleza vizuri kuliko Daktari wa Uchumi. Wakili msomi anashindwa kueleza tofauti ya Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya.
 
Kosa la mwigulu ni nn?
Hapendi ushauri, anajifanya anajua kila kitu, kama utakumbuka kabla la hili alishauriwa, yeye akajibu watanzania kwa sasa hawata muelewa na ataonekana waziri wa ovyo, ila kwa maendeleo atakayo leta andandikwa kwenye historia. Ila sasa imekuwa kinyume chake.
 
 
PhD ya kusaga na kukoboa mashudu ya nguruwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…