Mpina ataka viongozi wa wizara, mashirika, mikoa na wilaya kupatikana kwa usahili!

Mpina ataka viongozi wa wizara, mashirika, mikoa na wilaya kupatikana kwa usahili!

Wazo zuri na tumechelewa sana,cabinet tu ndio president awe na uwezo wa kuteua na kutengua,judiciary ijitegemee na majaji wote waombe na kufanyiwa interviews (including CJ ),RCs na DCs futulia mbali uchafu huu,binafsi sioni umuhimu wao kabisa,fedha tutakayo okoa ikasukume maendeleo
 
Nani atasimamia uteuzi? Hivi ikiwa uteuzi utahitaji idhini kutoka bengeni, je, Mpina haoni kwamba siasa za upendeleo utashamiri? Mfano mwingine bunge liwe na wabunge wengi wa chama cha upinzani, je, haoni kwamba mfumo anaoupendekeza utachangia kwa nafasi kubakia wazi au kuwa na inefficiencies? Haoni kwamba Patron atashindwa kuwawajibisha kwa utendaji duni au wakikiuka sera? Au ndio itakuwa na maana vyama vyote vikubaliane sera za nchi? Kutakuwa na umuhimu gani wa kuwa na vyama vya upinzani?
 
Akichangia bungeni leo mbunge machachari wa CCM anasema umefika wakati sasa viongozi kama mawaziri, wakurugenzi, makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya wapatikane kwa kuomba nafasi hizo na kufanyiwa usahili.

Anasema mfumo wa sasa hauna uwazi kwani Rai hawezi kusoma CV za watu wote wanofaa kuteuliwa na kujua yupi ni sahihi pia anasema haijulikani hata ni wapi hao wateuiliwa wengine wanakotolewa na kuletwa kushika uongozi au kama hata waliomba hizo nafasi. Amemalizia kwa kusema mfumo wa vetting nao bado haugarantii kupata viongozi sahihi kwani imeelezwa kuna watu wasio raia wa Tanzania ambao wamepewa nafasi za uongozi.
Mkuu saa mbovu leo imesema kweli 🤣🤣🤣
 
Nani atasimamia uteuzi? Hivi ikiwa uteuzi utahitaji idhini kutoka bengeni, je, Mpina haoni kwamba siasa za upendeleo utashamiri? Mfano mwingine bunge liwe na wabunge wengi wa chama cha upinzani, je, haoni kwamba mfumo anaoupendekeza utachangia kwa nafasi kubakia wazi au kuwa na inefficiencies? Haoni kwamba Patron atashindwa kuwawajibisha kwa utendaji duni au wakikiuka sera? Au ndio itakuwa na maana vyama vyote vikubaliane sera za nchi? Kutakuwa na umuhimu gani wa kuwa na vyama vya upinzani?
Hujaelewa alichosema Mpina,
 
Well Said

KATIBA
Watu wanasahau kwamba katiba ndiyo inayoongoza teuzi zote hizi. Katiba ikifuliwa na kueleza kama alivyopendekeza Mpina kila kitu kinawezekana.

Bila kubadili katiba rais ateuendelea kuteua tu.
 
Pointless
Kuna point japo umevaa miwani ya mbao ndiyo maana huoni. Huyu Luhagq Mpina wakati wa Magufuli ndiyo alikuwa mmoja wa watendaji wanaoaminika. Hakuwahi kumshauri Magufuli namna bora ya kuemdesha nchi ila sasa hivi anajifanya ndiye bingwa
 
Ukiondoa chama chake, huyu mtu ni makini sana mara nyingi.
 
Binadamu hawatakiwi kubadilika kama alivyofanya mtume Paulo?
Hakuna kubadilika ni unafiki tu. Polepole aliwahi sema cheo cha DC kifutwe, cha ajabu alivyoteuliwa yeye hakujiuliza mara mbili kukubali!!

Mpina anataka interviews, cha ajabu alipokua waziri enzi za JPM alipinga katiba mpya ambayo ilitaka wabunge wasiwe mawaziri na pia wafanyiwe usaili na kamati za bunge!!! Unafiki tu
 
Yale Yale SERIKALI ZA MAJIMBO NI MUHIMU mfano tukio la mkurugenzi kibaka huko mafia ,serikali za majimbo hatuwezi kuruhusiu wahuniiiiii waongoze wilaya.
 
Yale Yale SERIKALI ZA MAJIMBO NI MUHIMU mfano tukio la mkurugenzi kibaka huko mafia ,serikali za majimbo hatuwezi kuruhusiu wahuniiiiii waongoze wilaya.
Hahahahaha haki nimecheka eti kuongozwa na wahuni
 
Watu wanasahau kwamba katiba ndiyo inayoongoza teuzi zote hizi. Katiba ikifuliwa na kueleza kama alivyopendekeza Mpina kila kitu kinawezekana.

Bila kubadili katiba rais ateuendelea kuteua tu.
Rais anaweza kuendela kuteua kwa katiba hii hii pamoja na usahili kufanyika. Inatungwa tu sheria ya bunge kusema wateuliwa watatoka katika kundi ambalo limefanyiwa usahili tayari.
Halafu mbona pia tume ya uchaguzi imefanyiwa mabadiliko pamoja na kubadilishwa jina bila kufanyika mabadiliko ya katiba?
 
Back
Top Bottom