Hii nchi sijui ni sababu gani inayopelekea watu ambao wamejitolea kwa dhati kukemea na kufichua vitendo vya kifisadi, na pia kukemea dhuluma wanayofanyiwa wananchi huwa wanapigwa sana vita. Ni lazima sote tutambue kuwa kama Mungu wetu angalituhesabia makosa tuyafanyayo kila iitwapo leo hakika hakuna hata mtu mmoja miongoni mwetu ambaye angestahili.
Ni vyema tuwaunge mkono wale wote wanaopaza sauti zao na kukemea bila woga ubadhirifu wa mali za umma. Kuwa na watu wasiokuwa na uthubutu wa kuweza kuhoji, hata pale madudu yanapifanyika, basi hapo ni sawa na mtu kupata hasara na kufilisika moja kwa moja.