Tetesi: Mpina: Hata wakitaka na Ubunge nitawaachia lakini sitonyamaza

"....tatizo jamaa wanadhani mimi nitababaishwa na mbinu yao chafu ya kutumia chombo cha habari kunitweza hahahaha!"

"....brother, kwa akili yako eneo lile lingekuwa na tabu mwamba ( JPM) angeniacha salama?!"

"....yule kijana ( Mwandishi wa TBC )aliitwa Dar es Salaam usiku na alifuatwa na V8 akapangwa cha kwenda kureport including wale Viongozi wa kijiji walitumiwa fungi la kutosha ili pamoja na wao wawatafute wakina mama wenye shombo pale kijiji kile wakatengeneza sinema nzuri ya kuropoka!"

"...acha wapige kelele na hata wakitaka hilo eneo acha wachukue muhimu watambue sitonyamaza abadani!"

Mpina.
Wala hatutaki unyamaze, endelea kuropoka tu kwani ni haki yako kikatiba na ndiyo Tanzania yetu tuliyoizoea.

Siyo ile ya 2015-21 iliyokuwa chini ya Kichaa mwenzio Dikteta Magufuli ambapo watu wote waliomkosoa alikuwa anawawinda awaue kama alivyomuua Ben Saanane na Azory Gwanda au kama alivyomshambulia Tundu Lissu kwa risasi..
 
Hapa ishu sio mpina,ishu wanaomtuma mpina kuibua uozo huo wanna malengo GANI HASA!!?

Check and Balance KWA awamu hii inafanywa kupitia mpina!!

Ngoja tuone!
 
Hili la shamba la Mpina ukiangalia waongeaji unajua kabisa kwamba ni movie imepangwa. Na hapa jf kuna wapambe wa kujibu mapigo ili jamaa aache kuwachachafya bungeni.
Makamba, Bashe, Nape, Mwigulu, Ummy ni watu hatari sn
 
"....tatizo jamaa wanadhani mimi nitababaishwa na mbinu yao chafu ya kutumia chombo cha habari kunitweza hahahaha!"

"....brother, kwa akili yako eneo lile lingekuwa na tabu mwamba ( JPM) angeniacha salama?!"

"....yule kijana ( Mwandishi wa TBC )aliitwa Dar es Salaam usiku na alifuatwa na V8 akapangwa cha kwenda kureport including wale Viongozi wa kijiji walitumiwa fungi la kutosha ili pamoja na wao wawatafute wakina mama wenye shombo pale kijiji kile wakatengeneza sinema nzuri ya kuropoka!"

"...acha wapige kelele na hata wakitaka hilo eneo acha wachukue muhimu watambue sitonyamaza abadani!"

Mpina.
Hii nchi sijui ni sababu gani inayopelekea watu ambao wamejitolea kwa dhati kukemea na kufichua vitendo vya kifisadi, na pia kukemea dhuluma wanayofanyiwa wananchi huwa wanapigwa sana vita. Ni lazima sote tutambue kuwa kama Mungu wetu angalituhesabia makosa tuyafanyayo kila iitwapo leo hakika hakuna hata mtu mmoja miongoni mwetu ambaye angestahili.

Ni vyema tuwaunge mkono wale wote wanaopaza sauti zao na kukemea bila woga ubadhirifu wa mali za umma. Kuwa na watu wasiokuwa na uthubutu wa kuweza kuhoji, hata pale madudu yanapifanyika, basi hapo ni sawa na mtu kupata hasara na kufilisika moja kwa moja.
 
mpina punguza kinyongo......sidhani kama una uchungu na maumivu kufikia aliyonayo muhitimu wa kozi ya ualimu mwenye shahada aliemaliza chuo toka mwaka 2015 na mpaka leo hajapata ajira na umri unakwenda bila ramani yoyote
Mwenye makosa ni huyo mhitimu ambaye umri Unakwenda yeye amebaki amebung'aa tu akisubiri ajira yenye malipo kiduchu
 
Huu ni upuuzi Kama kweli kasema haya basi Mpina ni mjinga.

State ikitaka kukushughulikia haitahitaji yote hayo. Ni chap Kwa haraka unabaki masikin
Hizo sio kazi za State, ni vichawa vya kujipendekeza kwa Dola. Ndio hao kipindi cha JPM mlisema wanatumwa nae.

Hao ni wapuuzi wadodgowadogo kabisa. Shida ya State ni kuwanyamazia kwani who cares? Acha wapopoane.
 
Hii nchi sijui ni sababu gani inayopelekea watu ambao wamejitolea kwa dhati kukemea na kufichua vitendo vya kifisadi, na pia kukemea dhuluma wanayofanyiwa wananchi huwa wanapigwa sana vita. Ni lazima sote tutambue kuwa kama Mungu wetu angalituhesabia makosa tuyafanyayo kila iitwapo leo hakika hakuna hata mtu mmoja miongoni mwetu ambaye angestahili.

Ni vyema tuwaunge mkono wale wote wanaopaza sauti zao na kukemea bila woga ubadhirifu wa mali za umma. Kuwa na watu wasiokuwa na uthubutu wa kuweza kuhoji, hata pale madudu yanapifanyika, basi hapo ni sawa na mtu kupata hasara na kufilisika moja kwa moja.
Alikuwa wapi kukemea toka kipindi kile cha ukiukwaji mkubwa wa haki kipindi cha jiwe.
 
Back
Top Bottom