Tetesi: Mpina: Hata wakitaka na Ubunge nitawaachia lakini sitonyamaza

Wala hatutaki unyamaze, endelea kuropoka tu kwani ni haki yako kikatiba na ndiyo Tanzania yetu tuliyoizoea.

Siyo ile ya 2015-21 iliyokuwa chini ya Kichaa mwenzio Dikteta Magufuli ambapo watu wote waliomkosoa alikuwa anawawinda awaue kama alivyomuua Ben Saanane na Azory Gwanda au kama alivyomshambulia Tundu Lissu kwa risasi..
 
Hapa ishu sio mpina,ishu wanaomtuma mpina kuibua uozo huo wanna malengo GANI HASA!!?

Check and Balance KWA awamu hii inafanywa kupitia mpina!!

Ngoja tuone!
 
Hili la shamba la Mpina ukiangalia waongeaji unajua kabisa kwamba ni movie imepangwa. Na hapa jf kuna wapambe wa kujibu mapigo ili jamaa aache kuwachachafya bungeni.
Makamba, Bashe, Nape, Mwigulu, Ummy ni watu hatari sn
 
Hii nchi sijui ni sababu gani inayopelekea watu ambao wamejitolea kwa dhati kukemea na kufichua vitendo vya kifisadi, na pia kukemea dhuluma wanayofanyiwa wananchi huwa wanapigwa sana vita. Ni lazima sote tutambue kuwa kama Mungu wetu angalituhesabia makosa tuyafanyayo kila iitwapo leo hakika hakuna hata mtu mmoja miongoni mwetu ambaye angestahili.

Ni vyema tuwaunge mkono wale wote wanaopaza sauti zao na kukemea bila woga ubadhirifu wa mali za umma. Kuwa na watu wasiokuwa na uthubutu wa kuweza kuhoji, hata pale madudu yanapifanyika, basi hapo ni sawa na mtu kupata hasara na kufilisika moja kwa moja.
 
mpina punguza kinyongo......sidhani kama una uchungu na maumivu kufikia aliyonayo muhitimu wa kozi ya ualimu mwenye shahada aliemaliza chuo toka mwaka 2015 na mpaka leo hajapata ajira na umri unakwenda bila ramani yoyote
Mwenye makosa ni huyo mhitimu ambaye umri Unakwenda yeye amebaki amebung'aa tu akisubiri ajira yenye malipo kiduchu
 
Huu ni upuuzi Kama kweli kasema haya basi Mpina ni mjinga.

State ikitaka kukushughulikia haitahitaji yote hayo. Ni chap Kwa haraka unabaki masikin
Hizo sio kazi za State, ni vichawa vya kujipendekeza kwa Dola. Ndio hao kipindi cha JPM mlisema wanatumwa nae.

Hao ni wapuuzi wadodgowadogo kabisa. Shida ya State ni kuwanyamazia kwani who cares? Acha wapopoane.
 
Alikuwa wapi kukemea toka kipindi kile cha ukiukwaji mkubwa wa haki kipindi cha jiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…