GE2025 Mpina kwenda ACT Wazalendo ni Plan ya Samia, hii unahitaji kuwa na extra akili kujua hii move. Mpina ni project ya Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sio Polepole wala mpina wote ni project za chura kiziwa...wangelikuwa wako really kw hayo waliofanya ...basi wangeungana na Watanganyika kudai Reforms.
Pia saa hizi wangekuwa wananyea debe, kama huyo Polepole angeshapewa kesi ya uhaini na kuvuliwa uanachama.

Maigizo tu haya. Toka ameanza kutoa matamko hakuna hatua yeyote ya maana aliyochukua ama kuchukuliwa, ni kubwabwaja.

Polepole, Mpina, Gwajima ni diversion plans.
 
Hufai kuwa mchunguzi
 
Mpina ana kura za wasukuma na kanda ya ziwa ,chaumma project kwishney huko
 
Naunga mkono hoja Mpina na gwajima wote ni project za mfumo.

Hata Polepole ni project ya mfumo kumuamsha mkubwa ajaribu kuweka mambo sawa huku ground watu hawaelewi moja wala mbili wanaona kutokuwajibika. Ufisadi. Undugunization.

Mpinzani wa kweli ni lissu anayepigania reforms maana panahitajika reforms kubwa sana ili hata ile dira ya maendeleo ifikiwe
 
Bongo sasa hivi hata ikinyesha mvua siku ya maandamano kuna watu watasema mvua hiyo ni kazi ya Samia.
 
Huo ndio ukweli
 
 
Chadema kuna wapumbavu wengi mno, Mpina angekuja chadema wangeporomosha uzi za kumsifia 😂
Sio CDM wapumbavu. Jamaa anasema hizo ni plan. Yaani tatizo kila siku mnajazwa na mnaingia ktk mfumo. Tafakari hoja yake. Ni suala la muda tu
 
Extra akili gani unahitaji hapo sasa kwa vitu vya kitoto kama hivi
 
Niliwaambia siku nyingi mpina ni project kamba ilivyokua Shibuda.
 
Mpina na samia hawaivi pamoja.Yule Kamishna wa polisi ndio project ya ccm
 
100%
 
Binafsi kwa sasa simuamini huyo Mpina kwenda huko ACT, naona ni mchezo wa kisiasa tena ambao umechorwa kwa muda mrefu tu. Uchaguzi mkuu utakapo isha baada ya muda Mpina atakuwa amekamilisha majukumu yake huko ACT na kurejea ndani ya CCM ama vinginevyo.

Wanasiasa wetu wapo kimaslahi zaidi, pale ambapo mchongo unaletwa mezani wenye maslahi mapana hata kuliko wa Ubunge lazima wanapita nao regardless heshima yao kwa jamii katika muda husika, narudia huu ni mchongo wa chama tawala katika kuhadaa umma wa Tanzania na dunia hasa nchi wahisani kuwa kuna upinzani Tanzania na demokrasia inafanya kazi vizuri, lakini ukweli ni matumizi mabaya ya Kodi za wananchi sisi.

Report ya CAG itaendelea kusema matumizi yasio na tija kwa nchi kwa bilions and billions. Hizi ni pesa za umma ndio zinampleke na kumhudumia muda wote akiwa huko, soon ataanza kuonekana na walinzi kibao, na kubadilishiwa aina ya usafiri wakati akitimiza majukumu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…