Bado haijajulikana mpira ni nini
Huenda tukasema kuna vitu vinavyoweza kuchangia katika mchezo huu wa mpira ambavyo vinaweza vikakuza na kuufanya mpira uwe mchezo mzuri.
Kitu cha kwanza ni wachezaji wenyewe wa mpira, hawa lazima wajengwe na wapatikane wachezaji wenye vipaji, afya njema, stamina, flexibility, nidhamu na passion.
Kitu cha pili wakufunzi wazuri wenye kujua mbinu mbalimbali za mpira kutokana na wachezaji wake, ambaye ataweza kufundisha mpira wa kisasa wenye ushindani.
Cha tatu ni viwanja na vifaa vya mchezo, lazima tuwe na viwanja vizuri vya kuchezea mpira kuanzia ngazi za mashule hadi kwenye vyuo vya kufundishia mpira wenyewe na wachezaji wawe na vifaa muhimu vya kuchezea ili waweze kuzoea kuvitumia pindi watakapo weza kucheza mpira wa kulipwa na pia ili waweze kujihifadhi na madhara yatokanayo na mchezo huo.
Ili haya mambo yote yafanikiwe lazima fedha itumike.
Mambo ambayo ya kuyapiga vita katika michezo yetu ni:-
1-Ushirikina
2-Roho mbaya
3-Utovu wa nidhamu.
Tukizingatia mambo haya basi mpira kwetu utakuwa:-
1-Ajira
2-Burudani
3-Mazoezi ya kujenga mwili.
4-Njia ya kuwaunganisha wana jamii.
5-Kusaidia baadhi ya jamii katika michezo ya hisani.
6-Matangazo ya biashara
7-Kuwaepusha vijana na kujiingiza katika mambo ya wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi wa pombe, uasharati.
Haya ni mawazo yangu ambayo yanaweza kuchangia katika mada hii.