Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Nadhani kama mpira ungetegemea pesa basi waarabu wangekuwa wanachukua kombe la dunia mara kwa mara, kwani wana invest pesa nyingi sana katika mpira lakini hawana timu nzuri.
Bado haijajulikana mpira ni nini
 
Bado haijajulikana mpira ni nini
Huenda tukasema kuna vitu vinavyoweza kuchangia katika mchezo huu wa mpira ambavyo vinaweza vikakuza na kuufanya mpira uwe mchezo mzuri.
Kitu cha kwanza ni wachezaji wenyewe wa mpira, hawa lazima wajengwe na wapatikane wachezaji wenye vipaji, afya njema, stamina, flexibility, nidhamu na passion.
Kitu cha pili wakufunzi wazuri wenye kujua mbinu mbalimbali za mpira kutokana na wachezaji wake, ambaye ataweza kufundisha mpira wa kisasa wenye ushindani.
Cha tatu ni viwanja na vifaa vya mchezo, lazima tuwe na viwanja vizuri vya kuchezea mpira kuanzia ngazi za mashule hadi kwenye vyuo vya kufundishia mpira wenyewe na wachezaji wawe na vifaa muhimu vya kuchezea ili waweze kuzoea kuvitumia pindi watakapo weza kucheza mpira wa kulipwa na pia ili waweze kujihifadhi na madhara yatokanayo na mchezo huo.
Ili haya mambo yote yafanikiwe lazima fedha itumike.
Mambo ambayo ya kuyapiga vita katika michezo yetu ni:-
1-Ushirikina
2-Roho mbaya
3-Utovu wa nidhamu.

Tukizingatia mambo haya basi mpira kwetu utakuwa:-
1-Ajira
2-Burudani
3-Mazoezi ya kujenga mwili.
4-Njia ya kuwaunganisha wana jamii.
5-Kusaidia baadhi ya jamii katika michezo ya hisani.
6-Matangazo ya biashara
7-Kuwaepusha vijana na kujiingiza katika mambo ya wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi wa pombe, uasharati.
Haya ni mawazo yangu ambayo yanaweza kuchangia katika mada hii.
 
Lazima fedha itumike, fedha ambazo ata USA, China na Russia wanazo lakini soccer la wanaume limewashinda...
 
Badala ya kunijibu swali langu na wewe pia unanitwanga swali...!!! Daaah, sisi waafrika bhana.
Jib la hilo swali ndo jibu lako.
Yesu alikuwa muafrika?
2 wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

3 Akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali. 4 Je, mamlaka ya Yohana ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa wanadamu? ”
 
Unaona sasa namna unavyozidi kujichanganya mkuu. Ninaongea na wewe unaaanza kuleta masuala ya Yesu matokeo yake wakija wafia dini hapa wataugeuzi mjadala huu kuwa wa kidini badala ya soccer.

Unatoka nje kabisa ya mada boss.
 
Basi ngoja nirudie
Kwanini sio Marekani wala Nigeria waliowahi kuonesha ushindani na kutwaa kombe la dunia?
Marekani na Nigeria hawana ushindani wa kisoka nchini mwao
 
Huenda tukasema kuna vitu vinavyoweza kuchangia katika mchezo huu wa mpira ambavyo vinaweza vikakuza na kuufanya mpira uwe mchezo mzuri.
Kitu cha kwanza ni wachezaji wenyewe wa mpira, hawa lazima wajengwe na wapatikane wachezaji wenye vipaji, afya njema, stamina, flexibility, nidhamu na passion.
Kitu cha pili wakufunzi wazuri wenye kujua mbinu mbalimbali za mpira kutokana na wachezaji wake, ambaye ataweza kufundisha mpira wa kisasa wenye ushindani.
Cha tatu ni viwanja na vifaa vya mchezo, lazima tuwe na viwanja vizuri vya kuchezea mpira kuanzia ngazi za mashule hadi kwenye vyuo vya kufundishia mpira wenyewe na wachezaji wawe na vifaa muhimu vya kuchezea ili waweze kuzoea kuvitumia pindi watakapo weza kucheza mpira wa kulipwa na pia ili waweze kujihifadhi na madhara yatokanayo na mchezo huo.
Ili haya mambo yote yafanikiwe lazima fedha itumike.
Mambo ambayo ya kuyapiga vita katika michezo yetu ni:-
1-Ushirikina
2-Roho mbaya
3-Utovu wa nidhamu.

Tukizingatia mambo haya basi mpira kwetu utakuwa:-
1-Ajira
2-Burudani
3-Mazoezi ya kujenga mwili.
4-Njia ya kuwaunganisha wana jamii.
5-Kusaidia baadhi ya jamii katika michezo ya hisani.
6-Matangazo ya biashara
7-Kuwaepusha vijana na kujiingiza katika mambo ya wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi wa pombe, uasharati.
Haya ni mawazo yangu ambayo yanaweza kuchangia katika mada hii.
Mpira una faida sana kwa taifa kama wenyewe utakupenda na sio wewe kuupenda alafu unakukataa. Tazama nchi kama Spain, Italy na nchi za South America jinsi vijana wanavyokula pesa ya soccer.
 
Marekani na mipesa yake yote yu wapi katika ramani ya soka

Azam yu wapi pia

Mo na mipesa yake aliinunua Ashanti iliishia wapi?
MO sio mtu wa mpira ila anataka kuutumia mpira kwenye mambo yake
 
Marekani hawako serious na mpira kwanza wanauita Soccer, alafu Kuna American Football huu kwao ndo mpira... jamaa hawako serious

Zaman tulikuwa tunamjua Tim Howard, Clint Dempsey na London Donovan tu But now kidgo wameanza ku invest kwa vijana Kama Dest wa Barca, Pulisic, na wengine wengi wapo German League naamini baada ya 10 year wanaweza fanikiwa kidgo..

Note: mpira = kipaji + process + investment + management + time
 
Utamaduni wa Africa ni ngoma
Mpira ni utamaduni lazima uwe damuni na kuwa sehemu ya maisha hapo ndo utaona matokeo chanya......... Cricket ni sehemu ya maisha na utamaduni wa India, Pakistan, England, South Afrika na Zimbabwe kama ilivyo Basketball Marekani vivyo hivyo kama uchawi ulivyo sehemu ya maisha yetu kwa hiyo mkuu mpira sio hela kama unavyodhani angalia mchina anavyohustle kutengeneza huo utamaduni hadi ananunua wachezaji kwa bei za kutupwa
 
Ni nchi nane tu duniani zilizowahi kutwaa kombe la dunia, tatu za Amerika ya Kusini na tano za Ulaya.

Kwa nini umeikomalia Marekani wakati kuna nchi nyingine nyingi tajiri zaidi ya Marekani ambazo hazijawahi kuonyesha mafanikio yoyote ya maana katika kombe la dunia?

Unaweza kusema Messi na mafanikio yake yote sio mchezaji bora kuwahi kutokea katika mchezo kwa sababu tu hajawahi kushinda kombe la dunia na Argentina?

Back
Top Bottom