Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Sio liliwashinda bali hawalipendi,
Mkuu, kama kitu haukipendi si unaachana nacho. Sasa mbona wao hawalipendi soccer lakini bado ni wanachama wa FIFA? Mbona hawajitoi kama Burundi walivyojitoa ICC?...
 
Mkuu, soccer liliwashindwa wanaume wa Marekani ndio maana wakaamua kuanzisha michezo yao wenyewe?...
Wamarekani wamekufanya nini wewe?

Walikunyima visa?

Maana si bure.

Nishakueleza Wamarekqni hawapendi mifumo ya Waingereza.

Hawapendi chai, wanapenda kahawa.

Hawaendeshi gari kushoto, wanaendesha kulia.

Hata tai za Wamarekani stripes zake zinaenda tofauti na za Waingereza.

Hawapendi soccer, wanapenda American Football na Basketball.

Sasa unataka kuwalazimisha wapende kitu wasichopenda?

Idea nzima ya watu kuhama huko ikd world, Ulaya, Asia na Africa, na kuja Marekani, ilikuwa kuachana na mambo ya hiyo dunia ya zamani ya kuanzisha mambo mapya ya dunia mpya.

Ndiyo maana Marekani imeleta umeme, imeleta internet etc, na hata kwenye michezo imeanzisha michezo mioya kama basketball.

Sasa kama hujui historia, ni vigumu kuelewa hayo.
 
Kama hawapendi soccer mbona bado wanachama wa FIFA mkuu? Burundi hawakuipenda ICC wakajitoa. Wao USA bado wanafanya nini FIFA?...

Kwani lazima soka iwe ni mchezo wako pendwa ili uwe FIFA?

Cricket ni mchezo number 1 India ila bado ipo FIFA. Nao unataka watoke?

Inadhuru nini kuwa FIFA hata kama wanaume wenu hawapendi soka let alone nchi nzima kama India.

Basi tuseme USA ipo FIFA sababu ya USWNT if that makes you happy.
 
Mpira ni kitu Fulani chenye umbo la duara hutumika Katika mchezo ambao hufanyika kwnye uwanja mkubwa na kuwa na watu 11 kwa kila pande mbili ambapo lengo ni kuukokota huo mpira uingie kwnye nyavu iliofungwa katika nguzo nne kwa kuzunguza hizo nguzo.

....atakae ingiza mpira humo kwnye nyavu Basi timu take inakua imeshinda..
Kama hamna nyavu je?[emoji1]
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimeja sana Afrika na hatufanyi maajabu?

View attachment 1645695

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Marekani imecheza fainali kadhaa za Kombe la Dunia.

Matokeo yao mazuri yalitokea wakati wa kuibuka kwao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1930, wakati Marekani ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Baada ya Kombe la Dunia la mwaka 1950, ambapo Marekani iliivuruga timu ya Uingereza katika mechi ya makundi kwa ushindi wa 1-0.

Marekani haikuwepo kwenye mashindano hayo mpaka mwaka 1990. Marekani ilishiriki kila Kombe la Dunia tangu mwaka 1990 hadi mwaka 2014, lakini hawakufuzu mashindano ya 2018 kwa mara ya kwanza tangu 1986 baada ya kupoteza kwa Trinidad na Tobago.

HAYA NDIO MAFANIKIO YA KANDANDA KWA NCHI ZA AFRIKA

(1) Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010) ndio timu pekee kutoka katika bara la Afrika kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya kombe la dunia la FIFA.

(2) Cameroon imecheza mechi nyingi kama team ya Afrika katika historia ya kombe la dunia. Imecheza mechi 23.

View attachment 1645697

(3) Nigeria ndio team iliyoshinda mechi nyingi katika kombe la dunia la FIFA kwa kushinda jumla ya mechi 6.

(4) Hao hao Nigeria (The Super Eagles) pia wanashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi (Magoli 23) kwa timu za bara la afrika.

(5) Mchezaji Abdul Rahman Fawzi ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka Afrika kushida katika mashindano haya ya kombe la dunia dhidi ya nchi ya Hungary mwaka 1934.

(6)Morocco ndio timu ya kwanza ya Afrika kupata "point" baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi na Bulgaria mwaka 1970.

(7) Tunisia ndio nchi ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya kombe la dunia baada ya kuwafunga Mexico 3-1 mwaka 1978.

(8) Morocco ndio timu ya kwanza kutoka Afrika kuvuka raundi ya kwanza na kufika raundi ya 16 bora mnamo mwaka 1978.

Je, mpira ni pesa au kipaji? Mbona umewashinda wote matajiri (U.S.A) pamoja na masikini (Afrika)?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mpira si kipaumbele kwao, kama ambavyo HAKI si kipaumbele cha CCM.
 
Mkuu, kama kitu haukipendi si unaachana nacho. Sasa mbona wao hawalipendi soccer lakini bado ni wanachama wa FIFA? Mbona hawajitoi kama Burundi walivyojitoa ICC?...
Yaani unafananisha uanachama wa FIFA na ICC?!
Tambua kwamba nchi kuwa mwanachama wa mchezo fulani ngazi ya dunia haimaanishi kwamba hiyo nchi inaupenda mno huo mchezo. Nchi Kama Argentina, England, Brazil, nk raia wake wanapenda sana soccer kuliko mchezo wowote ule, na wachezaji wa timu ya taifa wanatokana na raia haohao, so vijana hujiingiza katika huo mchezo wao pendwa na hivyo kufanikisha kuwa na timu ya taifa bora. Kwa US wananchi hawapendi sana soccer Kama wanavyopenda basket, swimming, Boxing, Music, Movies,nk hivyo vijana wengi wa kimarekani huchagua michezo yao pendwa ya basket, nk.
 
Imagine gwiji Maradona kuna watu hawamjui[emoji1]
Screenshot_20201211-171757_1607698392445.jpg
 
Timu za MLS zinajitahidi sana kuchukua malegend wa soka ili kushawishi wamarekani kufatilia mpira lakini bado impact ni ndogo, Zlatan kidogo alipokuwa huko alileta amshaamsha kama unavyoona dongo alilowapiga hapo alipomaliza muda wake[emoji23][emoji23]
Screenshot_20201211-175123_1607698336470.jpg
 
Kwa watasha huwa wana vipaumbele vyao kitu kama kwao hakitakuwa na faida pamoja na upekee basi huwa wanakitupa mbali na kuhusu afrika tatizo ni vipaumbele na kutokuwa na uwezo wa kutosha wa kushughulikia jambo husika na sababu za kushindwa huko zinajulikana dhahiri
 
Kuna siku nilimuuliza mmoja kwanini wanasema football is boring, anasema kwenye football timu zinaweza kucheza dakika 90 na kusipatikane goli, lakini kwenye basketball ni amshaamsha mwanzo mwisho atleast kwenye kila dakika 1 lazima washangilie goli, anasema kwenye 'soccer' hizo raha hazipo[emoji1][emoji1]
 
Kuna siku nilimuuliza mmoja kwanini wanasema football is boring, anasema kwenye football timu zinaweza kucheza dakika 90 na kusipatikane goli, lakini kwenye basketball ni amshaamsha mwanzo mwisho atleast kwenye kila dakika 1 lazima washangilie goli, anasema kwenye 'soccer' hizo raha hazipo[emoji1][emoji1]
Daaah jibu la huyo mwamba kweli ni kiboko mkuu wakati mimi hapa sijui hata sheria moja ya basketball
 
Kwa watasha huwa wana vipaumbele vyao kitu kama kwao hakitakuwa na faida pamoja na upekee basi huwa wanakitupa mbali
Siku watakayojitoa uanachama wa FIFA ndio nitajua kuwa ni kweli hao USA hawana interest na soccer...
 
Namba moja duniani lakini si namba moja Marekani.

Sasa unalazimisha mtu awe mahiri katika mchezo asioupenda?

Unavyokwenda unaweza kuingia shughuli ya Waislamu Msikitini halafu ukawauliza kwa nini pilau lao halina nyama ya kitimoto.

Kwa sababu nyama ya kitimoto inapendwa sana duniani.

Marekani ni nchi tofauti. Wanaoenda kuwa tofauti. Wana kitu wanakiita "Anerican Exceptionalism".Wamekataa kutumia metric system mpaka leo. Si kqzima wafuqte mfumo unaofuatwa na dunia yote.

Dunia yote karibu wanatumia kilometers na meters, Marekani wanatumia miles na inches.

Wamarekani walitaka kupingana na wakoloni wao Waingereza.

Wakoloni wao Waingereza wanakunywa chai, Wamarekani wamekataa kunywa chai, wanakunywa kahawa.

Wakoloni wao Waingereza wanaendesha gari kushoto, Wamarekani wanaendesha kulia.

Wakoloni wao Waingereza tai zao stripes zake zinaenda upande mmoja, tai za Wamarekani stripes zinaenda upande tofauti.

Wakoloni wao Waingereza wanapenda Soccer, Wamarekani wanapenda American Football na Basketball.

Sasa usipoelewa haya mambo kihistoria unaweza kuhoji kama Wamarekani hawawezi Soccer, kumbe wenzako wamekataa mchezo wa Wakoloni wao, wameanzisha michezo yao tofauti.

Wewe usiyeweza kuanzisha michezo yako na kuifanya ipendwe na watu wako, endelea tu kuwa koloni la Muingereza kiutamaduni.
Hii maelezo imekaa sawa jombaa hongera, tukomae na bao letu na rede
 
Back
Top Bottom