Mpira wa "Anao anao" wa Fiston Mayele unamkosesha soko

Kuna siku isiyo na jina mtakuja kuleta hii mada nyie wenyewe na mimi nitakachofanya nitalink tu uzi huu.

Juzi niliwaambia ile Marumo ni timu changa na haina mashabiki kabisa, kuna watu wakaleta ubishi na walitegemea eti uwanja ungekuwa full house kisa kiingilio ni bure, wote tuliona jinsi juzi Marumo haikuwa na mshabiki hata mmoja wa kusakizia pale uwanjani.

Siku hizi situmii nguvu kutoa hoja, naongea halafu nakaa pembeni.
Lakini timu zote walizocheza nazo wakiwemo USM Alger walikandwa hapohapo bila kuwa na mashabiki, hoja yako hapa ni nini?
 
O

South Afrika wana mzuka wa kutosha kwenye mpira ni kwamba Marumo ndiyo haina mashabiki.

Derby ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates inajaza uwanja wa 70,000, Simba alipocheza na Chiefs, tuliona mashabiki wao wa kutosha, Simba vs Pirates, tuliona mashabiki wa kutosha wa Pirates, ila juzi hatukuona hata mashabiki 5 wa kusingizia wa Marumo kwenye mechi ya nusu fainali na kiingilio ni bure.

Acha kukaza fuvu hilo bwashee.
Uwongo siyo kitu kizuri, nimeishi South Africa nazijuwa vizuri hizo timu, Simba ilicheza na hizo timu kipindi cha Corona usidanganye watu.

Kama unafungwa goli 4 kipindi cha corona watu wamejifungia majumbani ukikutana na vibe lao la full house mngekufa hata hao 10 na ukumbuke wao ndio waanzilishi wa hizi vuvuzela mlizoiga, kule vuvuzela ndio Nyumbani kwake na vuvuzela ni jina la kizulu.

Unachopaswa kujuwa South Africa wanapenda timu na siyo mpira.

Mamelodi Sundowns kwa sasa ndio Giant lakini hawana vibe lolote South Africa ndio maana wanaweza kukupiga nje ndani hawategemei mashabiki maana ile ni timu ya mtu haina historia ndefu South Africa lakini imetawala soka kwa sasa.
 
Basi tufunge mjadala unavyotaka wewe. Marumo kafungwa na Yanga kwasababu hakuwa na mashabiki. Haya ridhika sasa, maana una reasoning za vihande mno.
 
Najua ninachokiongea na naamini wengi mmeshakiona. Hii ilianza toka goli la kwanza Musonda amefunga kwa Yanga pale kwa Mkapa. Alienda akalala chini, nakumbuka alivyonyanyuka akageuka akakuta mchezaji mmoja tu amemfuata. Kuna magoli kadhaa hilo lilitokea na sijasema magoli yote Musonda aliyofunga Mayele alikausha ila ni idadi ya kutosha kuona kuna jambo ukizingatia ni partner wake pale mbele.
Hapa sasa unapotosha unasemaje Mayele hana mchango kwa lile goli la Musonda?

Ile ndio ilikua njia rahisi ya kumtoka yule mchezaji wa Marumo manake Mayele alipiga hesabu na kuona udhaifu wa yule mchezaji kua ni speed na yeye anayo speed sasa icho alichofanya ndio kilikua sahihi kwa asilimia mia moja.

Tumpeni uraia huyu kijana kwa Kibu Denis tuliongeza idadi ya mizigo tu kwa taifa.
 
Nilikuwa nasema magoli mengine ambayo Mayele hakushangilia na Musonda, Mayele hakuwa na mchango mkubwa katika upatikanaji wa yale magoli kwa hiyo kisingizio cha juzi ni dhaifu.

Mayele hata akipewa uraia hana msaada maana tayari amechezea timu ya taifa ya DRC, ila mbona hizo mbio zake za kuku hatuzioni akichezea Chui? Kibu Mkandaji lazima ajumuishwe katika gemu zilizobaki za AFCON kama tuko serious na masuala ya kufuzu.
 
Lakini timu zote walizocheza nazo wakiwemo USM Alger walikandwa hapohapo bila kuwa na mashabiki, hoja yako hapa ni nini?
Basi tufunge mjadala unavyotaka wewe. Marumo kafungwa na Yanga kwasababu hakuwa na mashabiki. Haya ridhika sasa, maana una reasoning za vihande mno.
Hoja siyo kwamba Marumo amefungwa kwa kuwa haina mashabiki, ni kuwa ile ni timu changa. Na kama nilivyowahi kusema kuhusu Rivers na Bamako tena ukanibishia, ndiyo nimekiona kwa Marumo, timu zote hizi tatu ni mzuri na zina beki na middle nzuri sana zinazojua kucheza na mpira ila zinakosa safu nzuri ya washambuliaji ndiyo maana tuliona magoli ya wazi wote waliyokuwa wanakosa. Kwa hiyo credit kwa beki ya Yanga nimependa utulivu wao ila hamjakutana na timu dhaifu bali washambuliaji butu wasioweza kutumia nafasi vizuri.
 
Uwongo siyo kitu kizuri, nimeishi South Africa nazijuwa vizuri hizo timu, Simba ilicheza na hizo timu kipindi cha Corona usidanganye watu.

Kama unafungwa goli 4 kipindi cha corona watu wamejifungia majumbani ukikutana na vibe lao la full house mngekufa hata hao 10 na ukumbuke wao ndio waanzilishi wa hizi vuvuzela mlizoiga, kule vuvuzela ndio Nyumbani kwake na vuvuzela ni jina la kizulu.

Unachopaswa kujuwa South Africa wanapenda timu na siyo mpira.

Mamelodi Sundowns kwa sasa ndio Giant lakini hawana vibe lolote South Africa ndio maana wanaweza kukupiga nje ndani hawategemei mashabiki maana ile ni timu ya mtu haina historia ndefu South Africa lakini imetawala soka kwa sasa.
Hapo unajikangaja mwenyewe, kama Simba alicheza na hizo timu kipindi cha corona na bado mashabiki wao wakaja viwanjani, hii Marumo inakuwaje inacheza kipindi hakuna corona na inashindwa kushawishi watu waje kuisapoti? Pia sina uhakika kama vuvuzela bado zina vibe huko South, ni sisi tu tumechelewa na tunang'ang'ania haya mambo ya miaka 15 iliyopita.
 
Mkuu ingia YouTube tafuta goli la adebayor alipewa assist na Lennon, Lennon alichenga 'kijiji' kizima akampa adebayor akamalizia, adebayor akakimbia kushangilia, kilichotokea wachezaji wote wa spurs walimfata Lennon kushangilia nae, nadhani utapata jibu hapo
Acha uongo
 
O

South Afrika wana mzuka wa kutosha kwenye mpira ni kwamba Marumo ndiyo haina mashabiki.

Derby ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates inajaza uwanja wa 70,000, Simba alipocheza na Chiefs, tuliona mashabiki wao wa kutosha, Simba vs Pirates, tuliona mashabiki wa kutosha wa Pirates, ila juzi hatukuona hata mashabiki 5 wa kusingizia wa Marumo kwenye mechi ya nusu fainali na kiingilio ni bure.

Acha kukaza fuvu hilo bwashee.
Timu zenye mashabik nimbili tu kule South Orlando na kaizer hata mamelodi bado sana nikama azam tu
 
Kwanza niwapongeze Yanga kwa kufika Fainali. Huyo mganga wenu msimuache na akifa endeleeni na atakayemrithisha matunguli yake.

Leo nazungumzia goli la pili alilofunga Mayele. Nimpongeze kwa kuwa mshambuliaji mwenye kasi ya ajabu. Ananikumbusha wachezaji wa zamani kina Lunyamila na hata Ronaldo de Lima. Kilichonishangaza katika goli lile ni alivyouvuta ule mpira, dah kweli kasi anayo ila style hii ya kucheza hapana aisee, ule ni mpira wa kizamani sana.

Pia kwa nini toka Kennedy Musonda amekuja pale Yanga, Mayele anaonekana kama hajamkubali? Mara nyingi Musonda akifunga, Mayele huwa hamfuati kushangilia naye, najua mashabiki wa utopolo wanaliona ila wanakausha kwa kuwa timu inashinda. Kuna wakati Musonda anafunga goli anaenda kushangilia anajikuta yuko mwenyewe, hii haijakaa poa wanangu.

Namalizia kwa kuwapongeza tena kwa kuwa timu ya pili ya Tanzania kufika fainali za mashindano ya CAF.
ndo kilichobaki hicho
 
Katika haya maelezo yako yote, pointi iko kwenye pongezi tu. Huko kwingine kote umeandika porojo tu.
 
Njooni Klabu Bingwa tupambanie heshima ya kweli, acheni kupoteza muda wenu huko. Ukitaka kujua mashindano ya shirikisho hayana hadhi, angalia hao kina Mayele, Kisinda sijui Nabi wote tayari wana medali za ubingwa ila hawana hadhi Afrika.
 
Msimu ujao siyo mbali. Najua kwa upande wenu mtakuwa busy kwa mara nyingine tena kukifumua kikosi chenu, na hivyo kukisuka upya.
 
Elewa nimachosema, siongelei kukimbia tu na mpira maana washambuliaji wengi wanafanya pale inapobidi na nimewahi kusema moja ya mapungufu ya Baleke ni kutokuwa na uwezo wa kukimbia na mpira. Hapa naongelea kitendo cha Mayele kuupiga mpira kilomita moja mbele na kuanza kuukimbilia. Usijifanye hamnazo.
Kilomita Moja mbele.... eeeeh...
 
Msimu ujao siyo mbali. Najua kwa upande wenu mtakuwa busy kwa mara nyingine tena kukifumua kikosi chenu, na hivyo kukisuka upya.
Najua na nyie mtarudi huko huko shirikisho, mmeshaona raha kucheza na vilaza wameshawalemaza.
 
Eeeeh, au zilikuwa kilomita 2 zile? Ila Mayele dah....
Unaijua kilomita au unajitoa ufahamu...kutoka goli mpaka goli ni umbali gani .... Uwana Gani huo wenye hata MITA 500!!?? Ficha ujinga wako
 
Kwanza niwapongeze Yanga kwa kufika Fainali. Huyo mganga wenu msimuache na akifa endeleeni na atakayemrithisha matunguli yake.

Leo nazungumzia goli la pili alilofunga Mayele. Nimpongeze kwa kuwa mshambuliaji mwenye kasi ya ajabu. Ananikumbusha wachezaji wa zamani kina Lunyamila na hata Ronaldo de Lima. Kilichonishangaza katika goli lile ni alivyouvuta ule mpira, dah kweli kasi anayo ila style hii ya kucheza hapana aisee, ule ni mpira wa kizamani sana.

Pia kwa nini toka Kennedy Musonda amekuja pale Yanga, Mayele anaonekana kama hajamkubali? Mara nyingi Musonda akifunga, Mayele huwa hamfuati kushangilia naye, najua mashabiki wa utopolo wanaliona ila wanakausha kwa kuwa timu inashinda. Kuna wakati Musonda anafunga goli anaenda kushangilia anajikuta yuko mwenyewe, hii haijakaa poa wanangu.

Namalizia kwa kuwapongeza tena kwa kuwa timu ya pili ya Tanzania kufika fainali za mashindano ya CAF.
Ndio star wa timu na wiki ijayo wanashinda goli 3 na kuweka rekodi sasa ya kuwa timu ya kwanza tz kutwaa kikombe Afrika
 
Back
Top Bottom