Mpira wa "Anao anao" wa Fiston Mayele unamkosesha soko

Lakini timu zote walizocheza nazo wakiwemo USM Alger walikandwa hapohapo bila kuwa na mashabiki, hoja yako hapa ni nini?
 
Uwongo siyo kitu kizuri, nimeishi South Africa nazijuwa vizuri hizo timu, Simba ilicheza na hizo timu kipindi cha Corona usidanganye watu.

Kama unafungwa goli 4 kipindi cha corona watu wamejifungia majumbani ukikutana na vibe lao la full house mngekufa hata hao 10 na ukumbuke wao ndio waanzilishi wa hizi vuvuzela mlizoiga, kule vuvuzela ndio Nyumbani kwake na vuvuzela ni jina la kizulu.

Unachopaswa kujuwa South Africa wanapenda timu na siyo mpira.

Mamelodi Sundowns kwa sasa ndio Giant lakini hawana vibe lolote South Africa ndio maana wanaweza kukupiga nje ndani hawategemei mashabiki maana ile ni timu ya mtu haina historia ndefu South Africa lakini imetawala soka kwa sasa.
 
Basi tufunge mjadala unavyotaka wewe. Marumo kafungwa na Yanga kwasababu hakuwa na mashabiki. Haya ridhika sasa, maana una reasoning za vihande mno.
 
Hapa sasa unapotosha unasemaje Mayele hana mchango kwa lile goli la Musonda?

Ile ndio ilikua njia rahisi ya kumtoka yule mchezaji wa Marumo manake Mayele alipiga hesabu na kuona udhaifu wa yule mchezaji kua ni speed na yeye anayo speed sasa icho alichofanya ndio kilikua sahihi kwa asilimia mia moja.

Tumpeni uraia huyu kijana kwa Kibu Denis tuliongeza idadi ya mizigo tu kwa taifa.
 
Nilikuwa nasema magoli mengine ambayo Mayele hakushangilia na Musonda, Mayele hakuwa na mchango mkubwa katika upatikanaji wa yale magoli kwa hiyo kisingizio cha juzi ni dhaifu.

Mayele hata akipewa uraia hana msaada maana tayari amechezea timu ya taifa ya DRC, ila mbona hizo mbio zake za kuku hatuzioni akichezea Chui? Kibu Mkandaji lazima ajumuishwe katika gemu zilizobaki za AFCON kama tuko serious na masuala ya kufuzu.
 
Lakini timu zote walizocheza nazo wakiwemo USM Alger walikandwa hapohapo bila kuwa na mashabiki, hoja yako hapa ni nini?
Basi tufunge mjadala unavyotaka wewe. Marumo kafungwa na Yanga kwasababu hakuwa na mashabiki. Haya ridhika sasa, maana una reasoning za vihande mno.
Hoja siyo kwamba Marumo amefungwa kwa kuwa haina mashabiki, ni kuwa ile ni timu changa. Na kama nilivyowahi kusema kuhusu Rivers na Bamako tena ukanibishia, ndiyo nimekiona kwa Marumo, timu zote hizi tatu ni mzuri na zina beki na middle nzuri sana zinazojua kucheza na mpira ila zinakosa safu nzuri ya washambuliaji ndiyo maana tuliona magoli ya wazi wote waliyokuwa wanakosa. Kwa hiyo credit kwa beki ya Yanga nimependa utulivu wao ila hamjakutana na timu dhaifu bali washambuliaji butu wasioweza kutumia nafasi vizuri.
 
Hapo unajikangaja mwenyewe, kama Simba alicheza na hizo timu kipindi cha corona na bado mashabiki wao wakaja viwanjani, hii Marumo inakuwaje inacheza kipindi hakuna corona na inashindwa kushawishi watu waje kuisapoti? Pia sina uhakika kama vuvuzela bado zina vibe huko South, ni sisi tu tumechelewa na tunang'ang'ania haya mambo ya miaka 15 iliyopita.
 
Acha uongo
 
Timu zenye mashabik nimbili tu kule South Orlando na kaizer hata mamelodi bado sana nikama azam tu
 
ndo kilichobaki hicho
 
Katika haya maelezo yako yote, pointi iko kwenye pongezi tu. Huko kwingine kote umeandika porojo tu.
 
Katika haya maelezo yako yote, pointi iko kwenye pongezi tu. Huko kwingine kote umeandika porojo tu.
Njooni Klabu Bingwa tupambanie heshima ya kweli, acheni kupoteza muda wenu huko. Ukitaka kujua mashindano ya shirikisho hayana hadhi, angalia hao kina Mayele, Kisinda sijui Nabi wote tayari wana medali za ubingwa ila hawana hadhi Afrika.
 
Msimu ujao siyo mbali. Najua kwa upande wenu mtakuwa busy kwa mara nyingine tena kukifumua kikosi chenu, na hivyo kukisuka upya.
 
Kilomita Moja mbele.... eeeeh...
 
Msimu ujao siyo mbali. Najua kwa upande wenu mtakuwa busy kwa mara nyingine tena kukifumua kikosi chenu, na hivyo kukisuka upya.
Najua na nyie mtarudi huko huko shirikisho, mmeshaona raha kucheza na vilaza wameshawalemaza.
 
Eeeeh, au zilikuwa kilomita 2 zile? Ila Mayele dah....
Unaijua kilomita au unajitoa ufahamu...kutoka goli mpaka goli ni umbali gani .... Uwana Gani huo wenye hata MITA 500!!?? Ficha ujinga wako
 
Ndio star wa timu na wiki ijayo wanashinda goli 3 na kuweka rekodi sasa ya kuwa timu ya kwanza tz kutwaa kikombe Afrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…