Mpira wa Ulaya umekuwa wa kizembe sana nowdays kuliko Afrika

Kiukweli kwa mtu aliyezoea kuangalia mpira kuanzia miaka ya 2000 mpaka kuja 2015 lazima akubaliane na wewe. Mpira umepoteza thamani wachezaji wamekua lonya lonya sheria zimekua nyingi. Lakini sasa kinachotuumiza wengi wetu timu tulizokua tunazishabikia kipindi icho hazifanyi vizuri kwa sasa.

Kama ukiwa shabiki wa mpira hili halitakuumiza sana na huyo ndio mimi. Kwangu ni kawaida kabisa kukuta naangalia game ya Ipswich na Leicester au Verona dhidi ya Venezia sio tu game kubwa. Kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa kwa mshabiki wa mpira.
 
Mkuu, na wewe unaamini Halaand sio bora ni takataka kulinganisha na kina Nunez?
Waongee waongeavyo EPL haitokuja kushuka ubora kwenye hii dunia kwani hamna logo kama EPL na ndio inavilabu tishio duniani Sasa hivi arsenal man city na Liverpool hamna timu inapoenda kukutana na hizi timu Sasa hivi duniani
 
Niliwahi kuuliza kuwa, hivi kuna Striker wa sasahivi angeweza kabwa na hawa mabeki na kupita? Angalia tu aina ya mabeki...akina Paolo Maldini au Genaro Gatuso halafu eti Striker ni Ganacho au Gabriel Jesus
Kumbe unaangalia wachezaji dhaifu ndio unawashindanisha na hao mastaa wa zamani hivi nikuulize swali hiyo zamani kulikua hamna mabeki uchwara na washambuliaji uchwara
 
Majitu kazi ,majitu mwitu , mapafu ya mbwa mbavu kama William Gallas ,Claude Makelele ,Michael Essien
Ila aisee wachezaji wa miaka ile walikuwa wametimia , majitu yana ubavu ,kasi , unyumbufu , pumzi
Ukiambiwa kiungo ni kiungo kweli kweli
 
Hakika watu kama wewe mpo wachache sana na ndiyo mnaojua mpira halisi uliokuwepo ulaya na sasa hivi total different kabisa.

Lakini walioanza kuangalia majuzi wanaona kwamba ni soka Zuri kumbe ushubwada mtupu

Kwa sasa hakuna vipaji eti Halaand ni kipaji wajameni hata kwa Samuel Etoo alipokuwa prime huyo hafiki
 
Majitu kazi ,majitu mwitu , mapafu ya mbwa mbavu kama William Gallas ,Claude Makelele ,Michael Essien
Ila aisee wachezaji wa miaka ile walikuwa wametimia , majitu yana ubavu ,kasi , unyumbufu , pumzi
Uliambiwa kiungo ni kiungo kweli kweli
Hamna kitu hapo wote nimewashuhudia ni wachezaji wa kawaida sana
 
Majitu kazi ,majitu mwitu , mapafu ya mbwa mbavu kama William Gallas ,Claude Makelele ,Michael Essien
Ila aisee wachezaji wa miaka ile walikuwa wametimia , majitu yana ubavu ,kasi , unyumbufu , pumzi
Uliambiwa kiungo ni kiungo kweli kweli
Safi ssna na ule ndiyo ulikuwa mpira wa ukweli kabisa kabisa unaenjoy sana

Ngumi mkononi na mpira majitu yanaujua
 
Sasa hivi watu wanataka magoli
Ile anao anao tokea kati unafika golini unafinya na kipa kama enzi za kina Van Bursten hamna akina Maguire lazima wakupige kiatu
Mpaka kwa namba ngumu ngumu zile kama namba sita anayecheza shimoni bado watataka magoli eti
 
Nimegundua halaand unachukia kwakua ni kijana mdogo mwenye MAFANIKIO ikiwemo pesa akiwa na miaka 22 wewe u
Safi ssna na ule ndiyo ulikuwa mpira wa ukweli kabisa kabisa unaenjoy sana

Ngumi mkononi na mpira majitu yanaujua
Hapa Sasa ndio nimeona kumbe hujui mpira eti ngumi mkononi Sasa mpira na ngumi wapi na wapi si wakawe mabondia aisee kumbe kunawatu akili hawana kabisa jitu Zima kabisa eti ngumi mkononi🤣🤣🤣🤣
 
Hujui mpira bwanamdogo kizazi cha PlayStation ulishuhudia wapi wewe?

Hebu kalale hapa wanajadili wanaojua mpira hatukuzingatii
We ndio hujui mpira hao wachezaji ni wakawaida sana na wote nimewashuhudia hamna kitu chochote Cha ziada
 
Kumbe unaangalia wachezaji dhaifu ndio unawashindanisha na hao mastaa wa zamani hivi nikuulize swali hiyo zamani kulikua hamna mabeki uchwara na washambuliaji uchwara
Walikuwepo ila sijui kama umeelewa nilichomaanisha, Wachezaji wa sshv wengi wapo kisharo zaidi na wapo soft kulinganisha na wa zamani au wa miaka michache nyuma
 
Kiufupi hatukuzingatii huna hoja wengine wameelewa wehye akili

Bye
 
Mpaka kwa namba ngumu ngumu zile kama namba sita anayecheza shimoni bado watataka magoli eti
Mpira ume badilika una kasi watu wanataka matokeo masuala ya kupiga kanzu matobo bila uelekeo watu wamehama uko
 
We ndio hujui mpira hao wachezaji ni wakawaida sana na wote nimewashuhudia hamna kitu chochote Cha ziada
Kwahiyo watu wote hao wanaokwambia hawajui wewe mtoto wa "afu mbili" ndiyo unajua?

Maajabu hatautaki OK?
 
Mimi nimemiss ule mpira jihad , enzi zile ukisikia ni Chelsea vs Real Madrid ,au Barca Vs AC Milan ,Au Inter Vs Manu
Hutamani kubanduka kwenye screen yako , maana ilikuwa mbio na skills mwanzo mwisho
Majitu yalikuwa yanapiga kazi si mchezo ,ila kwa sasa kilichopunguza ladha ya soka ni mifumo ya sasa ya soka na nguvu walizopewa makocha tofauti na kipindi kile , hizi techniques za walimu kuongoza timu uwanjani zinawaforce wachezaji waende mule mule na hawatakiwi kuongeza au kuleta manjonjo yao tofauti na miaka ile ya nyuma ,ni kweli kiasi kikubwa wachezaji wanakuwa robots wa mfumo wa kocha kwa sasa
 
Walikuwepo ila sijui kama umeelewa nilichomaanisha, Wachezaji wa sshv wengi wapo kisharo zaidi na wapo soft kulinganisha na wa zamani au wa miaka michache nyuma
Kwamba Jude au vincus ni masharo sio
 
Mchambuzi nguli The MoNA
Captain Marvelous
lembu
hamis77
Mnasemaje kuhusu hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…