Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Hiyo pesa waliyoichukua 5billion + na kuihamishia bot ni pesa waliyotapeliwa watu.inaonekana watu wengi wamepigwa sana hapa.
Kifupi watz wengi wanapenda mteremko kitonga.akitokea mjanja mwingine lazima wapigwe maboya wengine.kweli wajinga hawaishi.
Investment funding, hakuna aliyetapeliwa alikuwa anakusanya anawekeza faida ikipatikana anagawa, tatizo hakufuata sheria za nchi zinavyotaka
 
Ni kweli amefanya makosa au wamechungulia kwenye account wanatafuta jinsi ya kuzipunguza kidogo
 
Hapana. Sio rahisi kuuza hivyo vitu vingine kimyakimya bila kujulisha mahakama. Alichonyang'anywa ni huo mpunga tu. Kama kuna kingine mahakama ingesema.
Oky kama nikweli unachosema, basi serikali imeamua wagawane mabilioni, wenyewe wachukue cash. Mr kuku abaki na asset maana kigamboni jamaa anaekari zaidi ya 34 ,Godown za kufugia zaidi ya 15 tena za kisasa, mabasi, na vigari vidogo vidogo zaidi ya 10 vyakusambazia bidhaa. Ile investment aliyoifanya ni zaidi ya 1.5 billion

Tena hapo serikali itakuwa imemsaidia sana maana, hakuna wa kumshataki tena hukumu imeshatolewa walioumia ni raia wawekezaji.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si kwenye akaunti kuna iyo Billion 5.4 sasa iyo 5 itumike kama Fidia hafu iyo pont 4 (Mil 400) jamaa awape Mahakama Mil 5 yao hafu ibaki Mil 395.


Mil 100 hivi aende vacation viwanja vya mbele kama week 2 hivi hafu arudi kuanza upya.

Atawapata wajinga wengine tu.
Nyamaza tu sasa kwani inaonekana wewe ni mzito sana kuelewa! si usome taratibu ili uelewe?
 
Someni muelewe vizuri ni kwamba ameshakubaliana na DPP. Kwa mfumo mpya wa Plea Bargain

Wameshaangalia kwenye akaunti ana 5.4billion wamekubaliana unakiri kosa tunazichukua hizi halafu tunapunguza mashtaka

So 5.4 ya FIDIA washachukua
Halafu wanakupa adhabu ndogo ya FAINI ya million 5 au Jela miaka mi5

So wameshampukutisha kila kitu dogo hadi hiyo mil5 kashindwa kulipa kaenda rumande
Duh! Dogo ana talent ya mambo ya biashara , serikali ingetafuta namna ya Kudili nae bila kuathiri biashara yake.

So far sikuskia km kuna MTU ametapeliwa halafu isitoshe alikuwa anatengeneza ajira na chain ndefu ya kusupply kuku Hadi ubalozi wa marekani
 
Hiyo pesa waliyoichukua 5billion + na kuihamishia bot ni pesa waliyotapeliwa watu.inaonekana watu wengi wamepigwa sana hapa.
Kifupi watz wengi wanapenda mteremko kitonga.akitokea mjanja mwingine lazima wapigwe maboya wengine.kweli wajinga hawaishi.
Crowd funding sio utapeli usimsingizie dogo! Wawekezaji wote walikuwa wanalipwa hela zao kwa wakati sasa utapeli hpo uko wapi?
 
Hakuna lolote ni wivu na kuona watu wamebuni namna ya kuendesha miradi huku wakisaka wawekezaji wadogo
True mkuu! Mabenki yenyewe kutoa mikopo yenye riba nafuu ni ishu!

Dogo kajiongeza kwa kutafuta wawekezaji kwa njia isiyo rasmi anaonekana mwizi

Ndiyo maana Africa ni vigumu Sana kuwa tajiri ungali kijana, sababu gape zote za kutusua zimewekewa Sheria Kali makusudi ili vijana tuendelee kusota.
 
Kuweka hela benki za Tanzania ni risk.

Muda wowote wakizitaka wanazichukua.

Bila mjadala mrefu.
Mkuu, nadhani hata Ulaya kuna kuzuia na kunyang'anya mali na maslahi, interest and asset seizure and forfeiture.

Na pia haijasemwa kama walipokaa Mr. Kuku na DPP mjadala ulikuwa mrefu au mfupi.
 
Hizi kesi sa kukubali mashitaka na kulipa fine ni mbinu za kuibia watu pesa.

Binafsi mpaka leo sijaelewa kosa la mr kuku. Maana kama mradi ulikuwa active na watu wanawekeza kwa free consent sasa kosa lipo wapi?
Aliuza hisa bila kusajiliwa soko la hisa!!!@
 
Yaani sijui tunaishi nchi gani. Baada ya jamaa kuzinguliwa soko la kuku liliyumba sana. Yaani wameua mradi mkubwa ambao huko mbele huenda ungekua na manufaa. Tatizo wivu watanzania tukiona mtu katoboa bila sugu mikononi tunaanza kuita wizi na majina mengine yasiyofaa
Jamaa alikuwa alishapata tenda za kusupply kuku kwenye balozi , mahotel na international school .

Kwa serikali inayojielewa baada ya kuona tatizo ingekaa na mhusika na kumuelekeza namna sahihi ya kufanya mradi wake bila kuathiri biashara na ajira alizotengeneza.
 
Pamoja na hivyo dogo alitumia akili nyingi sana kuweza rubuni watu wote hao
Sio kurubuni ni kushawishi, ukisema kurubuni maana yake jamaa alikuwa tapeli wakati ukweli ni kuwa kila aliwekeza alipewa mgao wake kwa mujibu wa makubaliano.
 
IQ yako kiduchu sana. Mtu akikwapua fedha ya mwingine kwa udanganyifu jua ingeweza kutumika kwa mambo muhimu ikiwemo kuokoa maisha. Fikiria out of the box. Akili yako ibamue kidogo.
Amemdanganya Nani wakati kila mwekezaji alikuwa akipata gawio lake km kawaida?

Tatizo jamaa aliintoduce kitu kipya kbsa nchini na watu km wewe kwa kutoelewa mnamuita tapeli wakati huko Nigeria kitu alichofanya dogo ni kitu kilichozoelekakwa miaka mingi wanaita crowd. Funding.
 
Ukisoma maandiko yameandikwa vizuri na kuelezea kuwa kila mtuu atakula kwa jasho lake sema walimwengu wamebadilisha badala ya kula kwa jasho wanataka mteremko.

Mr kuku kashaa asiwa na hali yake na walio taka ule mteremkoo wakee wanalia na kusag meno hawakusikia na walakusoma maandiko hakika kuku kaliwa na mchele
 
Hazitatosha, inabidi BOT wakae nazo wakati tathmini ya waliotapeliwa ikiendelea ili kuhakiki nani katapeliwa kiasi gani, na kila mtu apate asilimia ngapi ya alichotapeliwa, maana kamwe haziwezi tosha
Hivi hizi habari za kutapeliwa mnazitoa wapi?

Maana hta mashtaka yake hayahusiani na yeye kuwatapeli watu!
 
Back
Top Bottom