Kibandari hicho cha Dar es salaam kilichojengwa na mkoloni eti ndo kitufanye tusijenge libandari likubwa la kuwezesha mimeli mikubwa mikubwa kushusha mzigo!- Jiwe na serikali yake wana vision fupi kwelikweli
Siku hizi kuna mimeli inabeba mafuta tani Milioni 4, Hii bandari ya Dar inaweza kuhudumia dude kama hilo?
Siku nchi ikiwa vitani na ikawa inahitaji mafuta ya kutosha kwa ajili ya mavyombo ya kijeshi huko msitari wa mbele na mengine kutumika nchini, tuna uwezo wa kuagiza mimeli mikubwa ikaweza kutia nanga kwenye kibandari cha Dar?
Population ya nchi yetu inazidi kuongezeka , leo tuko watu milion 50,miaka 99 ijayo tunaweza kuwa watu milion 200, sasa kama hatuna vision ya kuwa na Libandari lenye kuweza kubeba ma Super Tankers itakuwaje?.
Ukitaka kula lazima uliwe, Miaka 99 kwa nchi ni kitu gani?, Hongkong si hiyo hapo walipewa waingereza waiendeshe miaka 100,mbona imerudi kwa wachina, na wachina wakaamua waiongezee miaka mingine 50 ijiendeshee mambo ya ndani, sasa miaka 50 si inaisha keshokutwa tu?
Mambo ya nchi yanahitaji long vision, siyo sifa sifa tu
Sasa Bandari ya LAMU hiyo hapo, na inajengwa na wachina hao hao, sisi tumembwelambwela.
Hiyo SGR tunayojenga kama haitakuwa na mzigo mkubwa wa kutosha wa kubeba itakuwa Underutilized!
Kwa taarifa zenu, Mchina anataka kufungua front ya kibaishara na Afrika, Alitaka Tanzania iwe gateway ya kuingilia kwa sababu ya historia nzuri na uhusiano wetu mzuri na wao na pia kwa sababu wana reli ya TAZARA waliyotusaidia kujenga miaka 50 iliyopita. Sasa kwa kuwa sisi tunajivutavuta watakwenda kuangusha kitu cha maana hapo LAMU, Then Kenya wataiongezea urefu SGR yao ifike Uganda na South Sudan, Ikshafika Uganda naamina Kagame atataka link ya SGR ya Uganda pia iende kwake na wakati huohuo atakuwa na Link ya SGR kutoka Tanzania.
Kagame akifanikiwa kuwa na SGR mbili moja kutoka Kenya na nyingine kutoka Tanzania atakuwa na leverage kubwa mno katika east Afrika, kwa sababu akikosana na nchi moja atatishia kupitishia mzigo wake nchi nyingine, kwa hiyo atakuwa na bargaining chip kubwa ndani ya East Africa.
Mradi wa Bagamoyo ulikuwa unaandamana na viwanda kibao kwenye Economic Zone hiyo, sasa hivyo vitu vimeyeyuka!