Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Jamaa hawa wanatumika kwa propagations nyingi
 
My insticts says tunapewa kingi tule ili tuliwe vizuri.
Chinese people are still interested on Bagamoyo Project, kitachotokea sasa ni fast tracking ya mazungumzo ya huo mradi, yani wanatuingiza kingi, then ndio waturarue.
 
Sina taarifa kamili juu ya bandari ya Lamu,

Ila kama hicho ulichoadika ni sahihi, basi wale walio hofu kuwa bandari ya Dar itakufa kwa uwepo wa bandari ya Bagamoyo basi hawakufikiria vyema, uwezekano wa bandari ya Dar kuuwawa na bandari za Kenya
 
Zitto, kwa taarifa yako bandari za Dar na Mombasa zipo ''underutilized'', pia kujenda au kupanua bandari sawa ila kuwe na mikataba iliyo na maslahi kwa nchi
 
Hili suala la Bandari ya Bagamoyo serikali iliangalie vizuri, lina faida kubwa sana, nashangaa kwa nini tunapoteza muda kunegotiate miaka nenda rudi, Zitto kwa hili ana point sana
 

Watu wamelipwa fidia kitambo iweje ashindwe kupitia mkataba arekebishe haraka na kuweka mapendekezo yake? Magufuli hautaki huo mradi yupo na Rwanda na kenya na Zito hawezi kushuka hadhi heshima kwa hoja hii kwani watanzania siyo wajinga wanamjua magufuli akiwa anakipenda kitu huwa na kasi sana lakini kwa Bandari ya Bagamoyo hana haraka wala hajali chochote kile hata pesa iliyolipwa fidia hajali kaamua kupotezea mazima.
 
Propaganda hao Kenya maisha yao magumu wana lala kwenye vibanda hela ina ishia kwa wakubwa kila mwaka ni vilio vya njaa nadhani unge zungumzia haya

Hata Tanzania hasa Tanganyika maisha ni magumu zaidi umasikini unazidi kushamiri kila kukicha
 
Kina cha maji ya Bandari ya Dsm ni kifupi meli kubwa haziwezi kuja hata zinazokuja hulalamika injini kuvuta tope uchafu chini.
We tambua kwamba bandari ya Dar ipo kwenye upanuzi wenye gharama ya zaidi ya trillion 1 kwa sasa na tayari mradi upo zaidi ya 60% usikariri
 
Zitto achana na siasa kabla hujaendelea kuaibika

hujui unachokipigania ktk siasa zako,yani upo kama pikipiki unaweza ipanda kwa upande wowote

achana na siasa ndugu yangu uzeeke na heshima kidogo uliyobaki nayo maana tyr heshima yako

ishaanza kuondoka na itapotea yote kama utaendelea kuongea/kuandika mashudu ya namna hiii

Nisikilize mzeeee ifike wakati mambo mengine unyamaze "pia ni jawabu la mtu genius" kukaa kimya

ila kuendelea kuropoka ropoka kwako kutaishia kukufanya uonekane takataka hata usiwekwe ktk historia

ya wana siasa waliojaribu kuwa na u "uthubutu" ktk hii nchi
 
Unajua hasara gani imepatikan kwenye makinikia?
 
Hawa huwa ni wepesi tu wa kuongea mkuu! Ila JPM angeamua kweli huo mradi uendelee hungemuona Zito akiunga mkono
 
Hakuna majasusi wa kiuchumi Tanzania,Tungekuwa NAO tusingeshindwa angalau kujua soko la mahindi tukaingia kichwa kichwa eti tunataka kuuza unga ilihali wenzetu wanauza mahindi karibu dunia nzima,wakulima wa mahindi wamehangaika na kupoteza mitaji na nguvu 2016-2018 ,tutawezaje kuyajua yaliyo magumu na yenye kuhitaji akili.Tunachoweza sisi ni kujua intelijensia ya mkutano wa Msigwa,Mbowe na kutafuta wamiliki wa akaunti za Twiter,Facebook,au Jamiiforum tu.
 
CCM wanachojua ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kwenye chaguzi mbalimbali tu vinginevyo vya kiuchumi hawataki kushiriki wamekariri zidumu fikra binafsi za mwenyekiti wa CCM Taifa
 
Hawa huwa ni wepesi tu wa kuongea mkuu! Ila JPM angeamua kweli huo mradi uendelee hungemuona Zito akiunga mkono

Miradi mingi hupigiwa kelele kwa sababu hakuna miradi ya CCM isiyo na mapungufu, lakini kumbuka mradi wa Bagamoyo ni China na Oman wanajenga kwa pesa zao hakuna senti ya Tanzania ufisadi wa kuchomeka kampuni zao binafsi kama wafanyavyo kwenye miradi mingine hakuna ndiyo maana magufuli kawakwamisha apate kuangalia ni wapi watapata chochote kwanza.
 
Kibandari hicho cha Dar es salaam kilichojengwa na mkoloni eti ndo kitufanye tusijenge libandari likubwa la kuwezesha mimeli mikubwa mikubwa kushusha mzigo!- Jiwe na serikali yake wana vision fupi kwelikweli

Siku hizi kuna mimeli inabeba mafuta tani Milioni 4, Hii bandari ya Dar inaweza kuhudumia dude kama hilo?

Siku nchi ikiwa vitani na ikawa inahitaji mafuta ya kutosha kwa ajili ya mavyombo ya kijeshi huko msitari wa mbele na mengine kutumika nchini, tuna uwezo wa kuagiza mimeli mikubwa ikaweza kutia nanga kwenye kibandari cha Dar?

Population ya nchi yetu inazidi kuongezeka , leo tuko watu milion 50,miaka 99 ijayo tunaweza kuwa watu milion 200, sasa kama hatuna vision ya kuwa na Libandari lenye kuweza kubeba ma Super Tankers itakuwaje?.

Ukitaka kula lazima uliwe, Miaka 99 kwa nchi ni kitu gani?, Hongkong si hiyo hapo walipewa waingereza waiendeshe miaka 100,mbona imerudi kwa wachina, na wachina wakaamua waiongezee miaka mingine 50 ijiendeshee mambo ya ndani, sasa miaka 50 si inaisha keshokutwa tu?

Mambo ya nchi yanahitaji long vision, siyo sifa sifa tu
Sasa Bandari ya LAMU hiyo hapo, na inajengwa na wachina hao hao, sisi tumembwelambwela.

Hiyo SGR tunayojenga kama haitakuwa na mzigo mkubwa wa kutosha wa kubeba itakuwa Underutilized!

Kwa taarifa zenu, Mchina anataka kufungua front ya kibaishara na Afrika, Alitaka Tanzania iwe gateway ya kuingilia kwa sababu ya historia nzuri na uhusiano wetu mzuri na wao na pia kwa sababu wana reli ya TAZARA waliyotusaidia kujenga miaka 50 iliyopita. Sasa kwa kuwa sisi tunajivutavuta watakwenda kuangusha kitu cha maana hapo LAMU, Then Kenya wataiongezea urefu SGR yao ifike Uganda na South Sudan, Ikshafika Uganda naamina Kagame atataka link ya SGR ya Uganda pia iende kwake na wakati huohuo atakuwa na Link ya SGR kutoka Tanzania.

Kagame akifanikiwa kuwa na SGR mbili moja kutoka Kenya na nyingine kutoka Tanzania atakuwa na leverage kubwa mno katika east Afrika, kwa sababu akikosana na nchi moja atatishia kupitishia mzigo wake nchi nyingine, kwa hiyo atakuwa na bargaining chip kubwa ndani ya East Africa.

Mradi wa Bagamoyo ulikuwa unaandamana na viwanda kibao kwenye Economic Zone hiyo, sasa hivyo vitu vimeyeyuka!
 
Zito hata ukiongea vya maana unaonekana BWEGE siku hizi

Watanzania siyo wajinga hata magufuli alishasema, watanzania wa sasa wanajua kuchambua kila kitu wanajua sinema zote zinavyokwenda hawawezi kumpuuza Zito watapokea na kulifanyia kazi bara-bara vyema kabsa.
 
Wakenya wa wapi? Acha uzushi wako kuuza Nchi kivipi? Zumbukuku ni wewe uliyekula pesa za kenya kuja kutengeneza propaganda za kishamba toka kolomije.
We jamaa huwa una koment kama una stress sana! Hivi Magufuli ale pesa za Kenya kisa nini hasa?

Urais ni taasisi kijana, unaposikia neno rais inabidi utoke nje ya box na kuacha kumuona JPM pekee
 
Sidhani kama uko vzr kichwani, kwani ulichoandika hakina uhusinao hata kdg na hoja ya mwandishi. Ni vzr ukawa unatulia na kusoma kilichoandikwa badala ya kukurupuka kama kile kitu'.
 
Wewe Mh. Zitto ni mbunge, sasa ulishindwa kuishawishi serikali ukiwa bungeni? Unaleta habari hii JF ili iweje! Unania ya kuona wananchi wanaichukia serikali yao kwa uongo wako? Una platform kubwa (Bungeni) ya kutoa maoni yako kuliko hii ndogo isiyo na meno. Na kama unarudisha maoni yako JF, ubunge wa nini?
 
Kwani na sisi ni MASOCIALIST au CAPITALISTS?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…