KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Sasa nimemaliza kuisoma mada ya Mh Zitto.
Kuna mambo magumu ambayo sio rahisi kuyaamini, lakini yanashawishi yaaminiwe. Kwa mfano hili la rafiki yetu Amollo Odinga.
Kuna vimeelea vinavyofanya pawe na shaka shaka katika jambo la Odinga kutuhujumu bila sisi wenyewe kujua?
Baadhi ya dalili ni maamuzi kuhusu usafiri katika ziwa Victoria, na mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye Bandari ya Kisumu (nyumbani kwa Odinga) Anayefuatilia mambo haya atajua ni kiasi gani cha kazi kimeelekezwa katika kuifufua Bandari ya Kisumu ili kiwe kitovu cha kusambazia mizigo ikitokea kwenye 'Northen Corridor', na hasa kwa vile ujenzi wa SGR umekwamia Naivasha.
Inavyoonekana, Bandari ya Mwanza haina tena kipaumbele kikubwa kwetu, mbali ya kupokea mizigo inayotoka huko juu, ikishirikiana na Bukoba na hata Chato (Bandari inajengwa?) Kwa hiyo Bandari ya Mombasa, baada ya kupokea mizigo katika meli ndogo kupitia Lamu, Mombasa inaweza kuwa ndiye msambazaji mkuu kwenye eneo lote la Kaskazini mwa Tanzania, kuanzia sehemu zote za Moshi, Arusha, Manyara, Shinyanga, Mwanza, Geita, na wakati huo huo sehemu hizi zikiwa njia ya kupitishia bidhaa za Rwanda, Burundi na DRC.
Dhana hii sio ya kubezwa hata kidogo. Ikumbuke vizuri ile ziara ya Uhuru Kenyatta Chato. Ukarabati wa Bandari ya Kisumu ilikuwa imekwishaanza, na siku hiyo anarudi nyumbani kwake, ilibidi ageuzie njia yake Kisumu kuhakikisha kazi inaendelea vizuri.
Ukarabati wa hiyo Bandari ulikwisha kamilika, na ilitegemewa izinduliwe mapema miezi kadhaa iliyopita ikiwahusisha viongozi wakuu wa nchi hizi, akiwemo na Tshsekedi wa Congo, Magufuli, Kaguta na nadhani hata yule wa Sudan Kusini. Huu ni mpango mahsusi.
Inawezekana Rais Magufuli kishastuka kuingizwa choo cha wanawake?
Kuhusu yaliyoelezwa kuhusu Lamu kuwa "a Trasshipment Hub", mimi nadhani wazo hili limewaijia kama 'an after thought,' baada ya kuhangaika sana kutafuta wawekezaji bila ya mafanikio yoyote na washirika waliotegemewa kushiriki kutoonyesha nia ya kufanya hivyo.
LAPSSET ulikuwa ni mradi mkubwa ukihusisha Bandari ya Lamu, Ujenzi wa miundo mbinu kama SGR na barabara, viwanja vya ndege, 'Resort Cities' n.k. katika ukanda wote wa Kaskazini mwa nchi ya Kenya. Bandari ilipangwa kuwa na ghati 32.
Baada ya kuona mwitikio wa washirika haupo, na hakuna mwekezaji yeyote aliyeonyesha nia juu ya mradi huo, serikali ikaamua yenyewe ianze na ujenzi wa ghati tatu za mwanzo huku ikiendelea kuwavutia wawekezaji. Ghati ya Kwanza imekamilika na inazinduliwa Novemba 7, (nadhani). Hili wazo la kuwa Bandari ya kusambazia mizigo kwenda bandari ndogo ndogo kama Dar es Salaam limepata nguvu sana hivi karibuni baada ya kushindwa kuifanya Bandari hiyo kuwa bandari ya kupitishia mizigo ya Ethiopia, Sudan Kusini Uganda na DRC; hili ndilo lilikuwa wazo kuu mwanzoni mwa kuubuni mradi huo, toka siku nyingi (1975) na kuja kukaziwa kwenye dira yao ya maendeleo ya 2030.
Ili bandari iweze kufanya kazi hizo inahitaji pawepo na miundombinu, barabara, reli nakadhalika, mambo ambayo hadi sasa hayapo. Kwa hiyo wazo la 'Transshipment Hub' likawadondokea kama Sir Isaac Newton alivyodondokewa (hapana, sio yeye, nimemsahau jina - miongo mingi imepita baada ya mambo haya kuyakumbuka vizuri).
Haya,sasa tumelizwa na Bagamoyo yetu?
Kwanza ni lazima tukumbuke pia kwamba, huenda hata sisi wazo la Bagamoyo tulilidaka tu, halikuwa wazo letu la asili! Ni nani asiyeikumbuka Bandari ya Mwambani Tanga... iliishia wapi?
Ni nani anayeweza kusema hapa kwamba SGR yetu hatukudandia kwenye mawazo ya wengine, tena hao hao tunaolia nao!
Je, Bandari ya Lamu kuwa "Transshipment Hub" ni tatizo kubwa kwetu? Hili ndilo ninalotaka kujua toka kwa wajuvi wa mambo haya. Je, Bandari ya Bagamoyo haiwezi ikajengwa kwa sababu ya uwepo wa Lamu? Na kumbuka, miradi hii sio bandari tu - kuna viwanda na makorokoro mengi mengine.
Djibouti wamejenga bandari zao kubwa tu na za kimkakati bila kujali uwepo wa hiyo "Transshipment Hub" ya Salasalah iliyopo hapo Oman.
Nasi tukisema, potelea mbali, tunajenga "Hub" yetu hapa Bagamoyo kwa sababu jiografia inaturuhusu vizuri zaidi, kuna yeyote atakayetuzuia, si ni biashara bwana? Mnunuzi atatafuta penye nafuu au sio?
Tuache kulialia sana jameni. Tanzania yetu hii ina kila kitu cha kutuwezesha kwenda mbele.
Hawa wenzetu huko Kaskazini ukisikia kelele zao nyingiiii, ujue wanalia na maumivu kimyakimya.
Wkifungua tu kamradi fulani kama SGR toka Mombasa kwenda Nairobi utadhani wamemaliza kila kitu. Ndege yao ilipoanza safari kwenda New York ukiwasoma utadhani hakuna ndege zingine zinazokwenda huko, huku Ethiopia wana miaka!
Ukiwakamata na udanganyifu wao katika mambo ya biashara, kama zile biskuti za sukari iliyoingizwa bila ushuru watakulalamikia kama wewe ndio mhalifu!
Lakini nitashangaa sana Rais Magufuli akiwa amehadaiwa kuihujumu nchi anayoiongoza kwa sababu za urafiki tu. Nitamshangaa saaana. Ni kwa kweli hata sitaki kabisa kuamini hilo kuwa linawezekana.