Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Sasa nimemaliza kuisoma mada ya Mh Zitto.

Kuna mambo magumu ambayo sio rahisi kuyaamini, lakini yanashawishi yaaminiwe. Kwa mfano hili la rafiki yetu Amollo Odinga.
Kuna vimeelea vinavyofanya pawe na shaka shaka katika jambo la Odinga kutuhujumu bila sisi wenyewe kujua?

Baadhi ya dalili ni maamuzi kuhusu usafiri katika ziwa Victoria, na mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye Bandari ya Kisumu (nyumbani kwa Odinga) Anayefuatilia mambo haya atajua ni kiasi gani cha kazi kimeelekezwa katika kuifufua Bandari ya Kisumu ili kiwe kitovu cha kusambazia mizigo ikitokea kwenye 'Northen Corridor', na hasa kwa vile ujenzi wa SGR umekwamia Naivasha.

Inavyoonekana, Bandari ya Mwanza haina tena kipaumbele kikubwa kwetu, mbali ya kupokea mizigo inayotoka huko juu, ikishirikiana na Bukoba na hata Chato (Bandari inajengwa?) Kwa hiyo Bandari ya Mombasa, baada ya kupokea mizigo katika meli ndogo kupitia Lamu, Mombasa inaweza kuwa ndiye msambazaji mkuu kwenye eneo lote la Kaskazini mwa Tanzania, kuanzia sehemu zote za Moshi, Arusha, Manyara, Shinyanga, Mwanza, Geita, na wakati huo huo sehemu hizi zikiwa njia ya kupitishia bidhaa za Rwanda, Burundi na DRC.

Dhana hii sio ya kubezwa hata kidogo. Ikumbuke vizuri ile ziara ya Uhuru Kenyatta Chato. Ukarabati wa Bandari ya Kisumu ilikuwa imekwishaanza, na siku hiyo anarudi nyumbani kwake, ilibidi ageuzie njia yake Kisumu kuhakikisha kazi inaendelea vizuri.

Ukarabati wa hiyo Bandari ulikwisha kamilika, na ilitegemewa izinduliwe mapema miezi kadhaa iliyopita ikiwahusisha viongozi wakuu wa nchi hizi, akiwemo na Tshsekedi wa Congo, Magufuli, Kaguta na nadhani hata yule wa Sudan Kusini. Huu ni mpango mahsusi.

Inawezekana Rais Magufuli kishastuka kuingizwa choo cha wanawake?

Kuhusu yaliyoelezwa kuhusu Lamu kuwa "a Trasshipment Hub", mimi nadhani wazo hili limewaijia kama 'an after thought,' baada ya kuhangaika sana kutafuta wawekezaji bila ya mafanikio yoyote na washirika waliotegemewa kushiriki kutoonyesha nia ya kufanya hivyo.

LAPSSET ulikuwa ni mradi mkubwa ukihusisha Bandari ya Lamu, Ujenzi wa miundo mbinu kama SGR na barabara, viwanja vya ndege, 'Resort Cities' n.k. katika ukanda wote wa Kaskazini mwa nchi ya Kenya. Bandari ilipangwa kuwa na ghati 32.

Baada ya kuona mwitikio wa washirika haupo, na hakuna mwekezaji yeyote aliyeonyesha nia juu ya mradi huo, serikali ikaamua yenyewe ianze na ujenzi wa ghati tatu za mwanzo huku ikiendelea kuwavutia wawekezaji. Ghati ya Kwanza imekamilika na inazinduliwa Novemba 7, (nadhani). Hili wazo la kuwa Bandari ya kusambazia mizigo kwenda bandari ndogo ndogo kama Dar es Salaam limepata nguvu sana hivi karibuni baada ya kushindwa kuifanya Bandari hiyo kuwa bandari ya kupitishia mizigo ya Ethiopia, Sudan Kusini Uganda na DRC; hili ndilo lilikuwa wazo kuu mwanzoni mwa kuubuni mradi huo, toka siku nyingi (1975) na kuja kukaziwa kwenye dira yao ya maendeleo ya 2030.
Ili bandari iweze kufanya kazi hizo inahitaji pawepo na miundombinu, barabara, reli nakadhalika, mambo ambayo hadi sasa hayapo. Kwa hiyo wazo la 'Transshipment Hub' likawadondokea kama Sir Isaac Newton alivyodondokewa (hapana, sio yeye, nimemsahau jina - miongo mingi imepita baada ya mambo haya kuyakumbuka vizuri).

Haya,sasa tumelizwa na Bagamoyo yetu?
Kwanza ni lazima tukumbuke pia kwamba, huenda hata sisi wazo la Bagamoyo tulilidaka tu, halikuwa wazo letu la asili! Ni nani asiyeikumbuka Bandari ya Mwambani Tanga... iliishia wapi?

Ni nani anayeweza kusema hapa kwamba SGR yetu hatukudandia kwenye mawazo ya wengine, tena hao hao tunaolia nao!

Je, Bandari ya Lamu kuwa "Transshipment Hub" ni tatizo kubwa kwetu? Hili ndilo ninalotaka kujua toka kwa wajuvi wa mambo haya. Je, Bandari ya Bagamoyo haiwezi ikajengwa kwa sababu ya uwepo wa Lamu? Na kumbuka, miradi hii sio bandari tu - kuna viwanda na makorokoro mengi mengine.

Djibouti wamejenga bandari zao kubwa tu na za kimkakati bila kujali uwepo wa hiyo "Transshipment Hub" ya Salasalah iliyopo hapo Oman.

Nasi tukisema, potelea mbali, tunajenga "Hub" yetu hapa Bagamoyo kwa sababu jiografia inaturuhusu vizuri zaidi, kuna yeyote atakayetuzuia, si ni biashara bwana? Mnunuzi atatafuta penye nafuu au sio?

Tuache kulialia sana jameni. Tanzania yetu hii ina kila kitu cha kutuwezesha kwenda mbele.
Hawa wenzetu huko Kaskazini ukisikia kelele zao nyingiiii, ujue wanalia na maumivu kimyakimya.

Wkifungua tu kamradi fulani kama SGR toka Mombasa kwenda Nairobi utadhani wamemaliza kila kitu. Ndege yao ilipoanza safari kwenda New York ukiwasoma utadhani hakuna ndege zingine zinazokwenda huko, huku Ethiopia wana miaka!

Ukiwakamata na udanganyifu wao katika mambo ya biashara, kama zile biskuti za sukari iliyoingizwa bila ushuru watakulalamikia kama wewe ndio mhalifu!

Lakini nitashangaa sana Rais Magufuli akiwa amehadaiwa kuihujumu nchi anayoiongoza kwa sababu za urafiki tu. Nitamshangaa saaana. Ni kwa kweli hata sitaki kabisa kuamini hilo kuwa linawezekana.
 
Zitto ni kinara wa "STATE CAPTURE"

AMetumika na akina ACACIA, akatumika na akina SCBHK -STANDARD CHARTERED BANK HONGKONG na sasa WACHINA WA BANDARI YA BAGAMOYO (ambao ndio haohao wa mradi wa makaa ya mawe mchuchuma na liganga)

"Mr. STATE CAPTURE "
 
Nilichoelewa ni Kwamba Odinga amechangia kukwamisha mradi wa bandari ya Bagamoyo.

Kwamba zile tripu Za Odinga Dar na Chato alikuwa anatumwa na nchi yake kumlisha sumu Rais wetu kuhusu mradi wa Bagamoyo.

Kama kweli Odinga alipewa na tuzo kwa kazi hiyo, kama nchi inabidi tujitathimini.

Kifupi Odinga alikuwa jasusi wa kiuchumi kwa nchi yake kwa mjibu wa Zitto.
Hii ni ngumu sana kuimeza.
Nashindwa kabisa kuelewa Mh Zitto kapata wapi ujasiri wa kulizungumzia hili.

Lakini pamoja na ugumu wa kuliamini hili, kuna viashairia vinavyoonyesha uwezekano wa maajabu haya yakawa na ukweli wake.

Sasa ije iwe kweli, sijui historia ya nchi hii itaandikwa vipi?

Rais aliyelihujumu Taifa lake? Nadhani huu ndio utakuwa mfano wa kipekee kabisa kuwahi kutokea duniani.
Na dunia itatushangaa sana.
 
Ujenzi wa Bandari yenye kina kirefu ya Lamu sasa kuzinduliwa rasmi Novemba, 2019. Sasa Lamu itapokea Meli kubwa za 4th Generation kama vile Suezmax, Neo-Panamax na Chinamax. Mizigo kutoka Meli kubwa itashushwa Lamu na kupakiwa kwenye Meli ndogo kuja Bandari ya Dar es Salaam na kwenda Bandari nyengine za Afrika kama Beira na Durban. Hii ndio kazi ilikuwa ifanywe na Bandari ya Bagamoyo - Mradi ambao umehujumiwa. Pia Kenya wameamua kuchukua mpango mzima wa Bagamoyo na kuutekeleza Lamu kwa kuanzisha Eneo Maalumu la Uchumi. Hapo kabla ilikuwa iwe Lamu Port Pekee.
Kuna mambo ambayo yapo bayana zaidi, ambayo sio kweli katika mada ya Mh Zitto.
Moja wapo ni hili la Bandari ya Lamu "Hapo kabla ilikuwa iwe Lamu Port Pekee." Hili sio kweli.

Zaidi ya hivyo, inafaa pia ikumbukwe kwamba Bandari ya Lamu haijampata mwekezaji hata mmoja, mbali ya serikali yenyewe kuamua kuanza na ujenzi wa ghati tatu, moja ya hizo tatu ndiyo imekamilika na itazinduliwa Nov. 7, mwaka huu. Ghati ya pili hata ujenzi haujaanza; ya tatu imetengwa kwa maksudi kuhudumia bomba la mafuta toka Turkana, na pengine ya Sudan Kusini (siamini), na tusisahau, uwezekano wa Uganda kupitisha mafuta yao huko, wazo hilo hawajaliondoa akilini mwao jamaa zetu hao. Bado wanajipa matumaini ya hilo kutokea. Kama Odinga anaweza kufanya vile...itakuwa M7?

Pili, hii habari ya Odinga na rafiki yake inapasua kichwa. Ni ngumu sana kuiamini.
Lakini ikitokea iwe kweli, yeye mwenyewe Odinga ashukuru kuipata hiyo tuzo ya "Maritime Champion of the Indian Ocean."
Nasema ashukuru kuipata hiyo tuzo, kwa sababu kama alikuwa bado anayo matumaini ya ahadi nyingine, kama ile ya URais, ..., hapo hatakuwa tofauti na rafiki yake. Wote watakuwa wameingizwa chakani. Mwenye kutaka kujua, asome alama za nyakati kuanzia sasa, baada ya ile Tume ya BBI kumaliza kazi yao. Odinga kwisha kazi.

Tatu. Rwanda kuwa na Kigali Logistics Platform na Bandari Huru ya Masaka itakayoendeshwa na Dubai World isitutishe kitu.
Mizigo yao watapitishia wapi? Wakongo watakubali kulipia gharama za Bandari mbili tofauti? Mbona gharama zitakuwa kubwa sana?

Hata hivyo Tanzania inafaa iwe na mwingiliano wa moja kwa moja na DRC, bila ya kutegemea kupitia nchi jirani, Burundi/Rwanda?Zambia/Uganda.
Pakiwepo Bandari Ziwa Tanganyika, itatusaidia sana kulishika soko kubwa la Congo.
 
Ndugu ZZK ukiweka bandiko na watu wakaja na maswali tokeza kujibu la sivyo hakuwepo maana ya kuandika
1. Uje na numerical analysis ya jinsi tungefaidika na mradi huo
2. Utuambie kwa kusema Uongo au Ukweli kwa uthibitisho kuwa
A. Serkali ilidanganya kuwa mkataba ulitaka tusipate kodi kwa muda kadhaa
B. Kuwa masharti yaliyosemwa na serkali kuwa moja ya kigezo ni kutoendeleza bandari zetu pwani ya bahari ya hindi ni UONGO
C. Useme kwanini kwa muda wote Jk akiwa madarakani haukusaini je kuna vitu vilikuwa si sawa hivyo kuhitaji marekwbisho na tayari yalifanyika?

Kama hujibu tutajumuisha kuwa ni ule upinzani ambao hata ungetekelezwa leo ungeponda kwahiyo ni mtaka sifa na elinu yako ni ya makaratasi au ile white serving education .
Na kwa mlengo huo wale wengine hatuoni shida kuita mamuluki
.
Umesema reli kwenda kigali itafanya Rwanda tusiipate. Je mizigo itashuka wapi na kusafiri kwa usafiri upi to kigali?

Rejea ya Barrick inawaondolea sifa maana mungekuwa viongizi hamkuwa tayari kuishinikiza Bareick , bora hata anayekosea ila anapambana kupata haki. Nyie mnaimani na mahakama za kinataifa tu, je mnajua zile mahakama zipo kumsaidia nani?

Naunga mkono hoja

Zitto rudi jukwaani hapa ujibu maswali ya watu
 
Sasa nimemaliza kuisoma mada ya Mh Zitto.

Kuna mambo magumu ambayo sio rahisi kuyaamini, lakini yanashawishi yaaminiwe. Kwa mfano hili la rafiki yetu Amollo Odinga.
Kuna vimeelea vinavyofanya pawe na shaka shaka katika jambo la Odinga kutuhujumu bila sisi wenyewe kujua?

Baadhi ya dalili ni maamuzi kuhusu usafiri katika ziwa Victoria, na mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye Bandari ya Kisumu (nyumbani kwa Odinga) Anayefuatilia mambo haya atajua ni kiasi gani cha kazi kimeelekezwa katika kuifufua Bandari ya Kisumu ili kiwe kitovu cha kusambazia mizigo ikitokea kwenye 'Northen Corridor', na hasa kwa vile ujenzi wa SGR umekwamia Naivasha.

Inavyoonekana, Bandari ya Mwanza haina tena kipaumbele kikubwa kwetu, mbali ya kupokea mizigo inayotoka huko juu, ikishirikiana na Bukoba na hata Chato (Bandari inajengwa?) Kwa hiyo Bandari ya Mombasa, baada ya kupokea mizigo katika meli ndogo kupitia Lamu, Mombasa inaweza kuwa ndiye msambazaji mkuu kwenye eneo lote la Kaskazini mwa Tanzania, kuanzia sehemu zote za Moshi, Arusha, Manyara, Shinyanga, Mwanza, Geita, na wakati huo huo sehemu hizi zikiwa njia ya kupitishia bidhaa za Rwanda, Burundi na DRC.

Dhana hii sio ya kubezwa hata kidogo. Ikumbuke vizuri ile ziara ya Uhuru Kenyatta Chato. Ukarabati wa Bandari ya Kisumu ilikuwa imekwishaanza, na siku hiyo anarudi nyumbani kwake, ilibidi ageuzie njia yake Kisumu kuhakikisha kazi inaendelea vizuri.

Ukarabati wa hiyo Bandari ulikwisha kamilika, na ilitegemewa izinduliwe mapema miezi kadhaa iliyopita ikiwahusisha viongozi wakuu wa nchi hizi, akiwemo na Tshsekedi wa Congo, Magufuli, Kaguta na nadhani hata yule wa Sudan Kusini. Huu ni mpango mahsusi.

Inawezekana Rais Magufuli kishastuka kuingizwa choo cha wanawake?

Kuhusu yaliyoelezwa kuhusu Lamu kuwa "a Trasshipment Hub", mimi nadhani wazo hili limewaijia kama 'an after thought,' baada ya kuhangaika sana kutafuta wawekezaji bila ya mafanikio yoyote na washirika waliotegemewa kushiriki kutoonyesha nia ya kufanya hivyo.

LAPSSET ulikuwa ni mradi mkubwa ukihusisha Bandari ya Lamu, Ujenzi wa miundo mbinu kama SGR na barabara, viwanja vya ndege, 'Resort Cities' n.k. katika ukanda wote wa Kaskazini mwa nchi ya Kenya. Bandari ilipangwa kuwa na ghati 32.

Baada ya kuona mwitikio wa washirika haupo, na hakuna mwekezaji yeyote aliyeonyesha nia juu ya mradi huo, serikali ikaamua yenyewe ianze na ujenzi wa ghati tatu za mwanzo huku ikiendelea kuwavutia wawekezaji. Ghati ya Kwanza imekamilika na inazinduliwa Novemba 7, (nadhani). Hili wazo la kuwa Bandari ya kusambazia mizigo kwenda bandari ndogo ndogo kama Dar es Salaam limepata nguvu sana hivi karibuni baada ya kushindwa kuifanya Bandari hiyo kuwa bandari ya kupitishia mizigo ya Ethiopia, Sudan Kusini Uganda na DRC; hili ndilo lilikuwa wazo kuu mwanzoni mwa kuubuni mradi huo, toka siku nyingi (1975) na kuja kukaziwa kwenye dira yao ya maendeleo ya 2030.
Ili bandari iweze kufanya kazi hizo inahitaji pawepo na miundombinu, barabara, reli nakadhalika, mambo ambayo hadi sasa hayapo. Kwa hiyo wazo la 'Transshipment Hub' likawadondokea kama Sir Isaac Newton alivyodondokewa (hapana, sio yeye, nimemsahau jina - miongo mingi imepita baada ya mambo haya kuyakumbuka vizuri).

Haya,sasa tumelizwa na Bagamoyo yetu?
Kwanza ni lazima tukumbuke pia kwamba, huenda hata sisi wazo la Bagamoyo tulilidaka tu, halikuwa wazo letu la asili! Ni nani asiyeikumbuka Bandari ya Mwambani Tanga... iliishia wapi?

Ni nani anayeweza kusema hapa kwamba SGR yetu hatukudandia kwenye mawazo ya wengine, tena hao hao tunaolia nao!

Je, Bandari ya Lamu kuwa "Transshipment Hub" ni tatizo kubwa kwetu? Hili ndilo ninalotaka kujua toka kwa wajuvi wa mambo haya. Je, Bandari ya Bagamoyo haiwezi ikajengwa kwa sababu ya uwepo wa Lamu? Na kumbuka, miradi hii sio bandari tu - kuna viwanda na makorokoro mengi mengine.

Djibouti wamejenga bandari zao kubwa tu na za kimkakati bila kujali uwepo wa hiyo "Transshipment Hub" ya Salasalah iliyopo hapo Oman.

Nasi tukisema, potelea mbali, tunajenga "Hub" yetu hapa Bagamoyo kwa sababu jiografia inaturuhusu vizuri zaidi, kuna yeyote atakayetuzuia, si ni biashara bwana? Mnunuzi atatafuta penye nafuu au sio?

Tuache kulialia sana jameni. Tanzania yetu hii ina kila kitu cha kutuwezesha kwenda mbele.
Hawa wenzetu huko Kaskazini ukisikia kelele zao nyingiiii, ujue wanalia na maumivu kimyakimya.

Wkifungua tu kamradi fulani kama SGR toka Mombasa kwenda Nairobi utadhani wamemaliza kila kitu. Ndege yao ilipoanza safari kwenda New York ukiwasoma utadhani hakuna ndege zingine zinazokwenda huko, huku Ethiopia wana miaka!

Ukiwakamata na udanganyifu wao katika mambo ya biashara, kama zile biskuti za sukari iliyoingizwa bila ushuru watakulalamikia kama wewe ndio mhalifu!

Lakini nitashangaa sana Rais Magufuli akiwa amehadaiwa kuihujumu nchi anayoiongoza kwa sababu za urafiki tu. Nitamshangaa saaana. Ni kwa kweli hata sitaki kabisa kuamini hilo kuwa linawezekana.

Impressive. Very. Nimejifunza mambo kadhaa pia
 
Naunga mkono hoja

Zitto rudi jukwaani hapa ujibu maswali ya watu

Hakuna hoja za kujibu katika hizo. Serikali na Rais walifanya ulaghai kwa kutumia propaganda kuchora picha hasi ya Mradi ule.

Suala la TAX HOLIDAY ni suala la KISHERIA. Eneo lolote ambalo ni SEZ lina tax holiday kisheria. Mradi huu upo chini ya EPZA na Sheria ya EPZA imeweka vivutio vya Kodi kisheria. Sio suala jipya wala sio suala la kujadili. Rais na Kakoko walidanganya Umma
 
Sijui mheshimiwa Zitto alipandwa shetani gani kichwani; wakati mwingine siasa nyingi ni saratani ya ubongo!
 
Sijui mheshimiwa Zitto alipandwa shetani gani; kichwani; wakati mwingine siasa nyingi ni saratani ya ubongo!

Mwalimu Kichuguu na wewe huwa unapotosha sana wakati mwingine hasa unapokuwa unajibu hoja za Zitto kwa mfano hapa hujajibu hoja hata moja ya Zitto zaidi ya "rhetoric" na pia umeshambulia credibility ya Zitto kuwa anapotosha badala ya wewe kuweka hoja zako au kilicho kweli.

Nakumbuka katika mada aliyowahi kuweka Zitto hapa kuhusu makubaliano ya Serikali yetu na Barrick, Zitto alisema kuwa Serikali imesamehe Trillion 424 ambazo ilithibitika kwa uchunguzi wa wataalamu wetu malrofesa wabobezi Mruma na Osoro kuwa ACACIA walituibia kwa muda mrefu walioperate nchini, ukang'ang'ania kuwa hilo siyo kweli, ukasema mkataba hausemi hivyo LEO hii imethibitika kuwa Serikali imesamehe Trilion 424 ila imekubali kupokea shilingi Trilion 0. 7 (Billion 700) zitakazolipwa ndani ya awamu saba. Sasa hapo nani alikuwa mkweli, Zitto au wewe?

Mwalimu tunategemea makubwa kutoka kwako badala ya hizi cheapshots kwa Zitto
 
Fatma Karume, Ansbert Ngurumo, Maria Sarungi na Kigogo2014 njooni mumuunge mkono mwenzenu.
 
@="ruaharuaha, Hizi zote ni porojo tu... zikiwa na lengo lile lile la kutaka kuwahadaa watu!

Ile hoja kwamba serikali HAITAKUSANYA KODI mbona haijaelezwa hapo?! Au bado serikali haitakusanya kodi?! Manake watu hapa walikuwa wanatoa povu kwamba serikali haitapata chochote kwa sababu hata kodi hawataruhusiwa kukusanya!!

And since Day 1, nimekuwa nikisema hapa kwamba HUO NI UONGO... wanachotaka ni kwamba, baadae Watanzania wakiona kodi zinakusanywa, watu waseme kama si Magufuli, pasingekuwa na kodi yoyote!!!

Hiyo 33 years lease ni porojo tu ambayo hata my young brother from another mother Malcom Lumumba amefafanua vizuri tu! Na hata kama wakitoa 33 years, wataongeza tu kwa sababu ndivyo sheria ya ardhi inavyosema unless transfer of the project ifanyike kabla ya huo muda, jambo ambalo sioni uwezekano wake hasa ukizingatia, suala la project transfer halihusishi Industrial Complex!

Kwamba the government will be free to develop other ports nayo ni porojo nyingine! Tangia uhuru tume-develop bandari ngapi zaidi ya kuziua bandari za Lindi, Kilwa, na Tanga iliyo ICU?!

Tangia zamani, I mean wakati wa JK kulikuwa na mpango wa kui-develop Bandari ya Mtwara ili kuhudumia oil tankers!!

Nini kingemfanya Mchina agome kuendeleza tankers terminal wakati anajua kabisa Bandari ya Bagamoyo haitatumika kwa ajili ya usafirishaji wa gas??!!!

Kabla JK hajaondoka, tayari kulikuwa na mpango wa kuendeleza Bandari ya Tanga ili kuhudumia mafuta ya Uganda ingawaje Magufuli na mashabiki wake anataka kuaminisha watu kwamba Bomba la Mafuta kutoka Uganda to Tanga is his doing wakati ni uongo mtupu!!!!

Kwahiyo leo hii bandari hizo zikiendelezwa ndo mseme kwa ajili ya Magufuli kuwakazia Wachina?!
 
Tena kibaya zaidi ambacho wanasahau ni kwamba mwekezaji anapewa Derivative Right hivyo ardhi haiwi yake, kwenye hati ya umiliki ardhi jina linatokea ni la Export Processing Zones Authority (EPZA) ambaye yeye ndiyo atawapa Uchina na Oman wafanyie biashara (Joint Venture).

Sheria za nchi yetu haziruhusu mtu kumiliki ardhi, sembuse mgeni!
Nikipata muda, nataka kujifunza zaidi hilo suala!!
 
@="Missile of the Nation,
Nitajibu mada hii baadaye nikipumzika kutoka shamba; Mheshimiwa Zito anatumia maoni ya mhariri wa gazeti la Citizen kujenga hoja yake wakati hata mhariri mwenyewe amesema "Kenya banks on" yaani kwa kiswahili rahisi ni kuwa Kenya inacheza karata yake kwenye mradi huo. Kucheza karata ni patapotea, hakuna maana ya kushinda. Hata walipoanza kujenga SGR kuimarisha Northern corridor walisema vivyo hivyo, lakini sasa hivi wanasema SGR ni white elephant. Kuchambua mikataba ni jambo la muhimu sana kuliko kukurupuka kwa vile jirani kafanya jambo kama hilo.Mradi wa Bagamayo ni mzuri tu iwapo una mkataba mzuri, siyo uruhus badnari ijengwe halafu seriklali isiwe na mamlaka ya kuingia ndani au kupanua bandari nyinge.. Wakati Lamu inajwengwa, Mheshimiwa Zito angetuletea mkataba wa Lamu halafu akachambua uzuri wake huku alkiulinganisha na wa Bagamoyo; siyo ngonjera tu.

Kuhusu mkataba wa Barrick, ACACIA na Tanzania, ni mpuuzi tu asiyejua maana ya Shillingi trilioni 400 ndiye anayeweza kuamini namba hiyo; Acacia ilikuwa na thamani isiyozidi $2bn yaani kama TSh 4.6 trilioni tu; ilinunuliwa na Barrick wa $1.2b. Hata kama kulikuwa na malimbikizo na interest, hayawezi kufikia kiasi hicho cha trilioni 400. Sijasoma tamko la serikali kusamehe kiasi hicho huenda ni kwa sababu walijua hakikuwepo. Bajeti ya serikali yenyewe mwaka huu ilikuwa trilioni 33.tu, halafu watu walete ngonjera nyingine kuidai ACACIA deni la trilioni 400; upuuzi tu.

Hayo makubaliano ya serikali kulipwa arears za kiasi hicho kwa miaka saba yalikuwamo kwenye mkataba ule labda kama wewe hukuusoma, siyo kuwa serikali imekiri leo. kama husumoa post zangu kuhusu mjadala ule zitafute. Zamani kidogo rais Mkapa aliingiza msamiati wa uvivu wa kusoma, jambo ambalo niliona kuwa alikuwa anatukana raia, lakini kweli inadibi tuwe tunasoma mambo na kuyaelewa badala ya kurukia yale tunayoambiwa bila kuona ukjweli wake.
 
Rejea Post # 14 ya uzi huu. Fungua hiyo clip na uitazame mwanzo mwisho. Kwa ufupi, hoja zako zote zimejibiwa kwenye clip hiyo.
Come on TUJITEGEME... tumefahamiana muda mrefu sana hapa JF, and I know you're smart than this ingawaje nawe ni Muunga Mkono Juhudi!!

Hivi kabisa ulitarajia Mkurugenzi wa Bandari aongee tofauti na anachoongea Rais wa nchi, tena under Magufuli Administration?! Google tafuta huyo Mkurugenzi aliongea wakati gani kama hujaona it's just few days baada ya Mr. President kuwa ameongea... did you expect him to sabotage what Mr. President said?!

Anyway, you may ignore that, na kuangalia upande mwingine! Hivi alichoongea huyo Mkurugenzi kina tofauti gani na ambacho kilikuwa presented na akina Profesa Mruma pale Ikulu kuhusu dhahabu iliyopo kwenye makinikia?!!

Wakati ile siku wakishabikia matani kwa matani ya dhahabu iliyopo kwenye yale makontena, ambayo hapo kabla JPM alisema inaweza kujaa kwenye malori ya tani 7, pale pale nili-doubt takwimu za akina Mruma, na nilisema:-
Hili la ripoti ya leo I still reserve my comment kwa sababu naona kuna mambo kama hayajakaa sawa!!!

I repeat, kuna mambo hayajakaa sawa na ninatamani sana kuiona full report!!!

Sikumsikiliza JPM lakini kwa kuangalia highlights nilizoona hapa JF; kama yaliyosemwa kwenye ripoti ni sahihi basi tafsiri yake Tanzania ndie largest gold producer duniani!!!

Hata Australia hawatufikii!!!

Please, mwenye full report atuwekee ili tuichambue critically!!!
Huyo alitumwa directly na Magufuli, na matokeo yake tumeyaona... ile dhahabu ambayo tuliambiwa kodi yake bila penalty, ni Shilingi Trilioni 108 kwa miaka 17, meaning about 6.4 Trillion kwa mwaka!!!

Sasa hivi kwa jinsi haya mambo yanavyoendelea, unaweza kuiamini ile ripoti ya Mruma?! Sasa ikiwa Academician tu anadiriki kusema uongo tena akiwa kwenye viunga vya Ikulu, seuze huyo Mkurugenzi wa Bandari?!

Na kuna mtu hapo juu ame-highlight the so called makubaliano mapya (not sure kama ni kweli)! Sasa kama ni kweli, hayo aliyosema Mkurugenzi mbona hayapo?!
 
Kuna Meli gani kubwa duniani kwa sasa ambayo haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar?

Sikiliza hiyo video, kina cha bandari ya Dar Ni kikubwa zaidi na kinao uwezo wa kuhudumia meli ya ukubwa wowote duniani

Maelezo mazuri sana JK angesign mkataba tungeingia kwenye mtego
 
Siku moja nilikaa kitako na waziri mstaafu aliyeshiriki juu ya mradi huu nikamuuliza kwamba hiki anachozungumza rais juu ya mradi huu ni cha kweli? Akasema si kweli.

Ukweli ni kuwa mradi huu ulihusu nchi Tatu,

Tanzania- Ardhi
China - Utaalamu na Ufundi
Arabuni - Mtaji

Akapinga hoja ama sababu aliyoitaji rais kuwa amekataa mradi huu kwakuwa TRA wamezuiwa kusimamia kodi.

Waziri akasema ni kweli kwenye mradi kama huo TRA hawawezi kusimamia kwakuwa si chombo kinachowajibika kwa wabia wote, Bali makubaliano yalikuwa ni kuunda chombo maalumu cha kimapato toka pande zote ambacho kitasimamia mapato, na TRA itahusika kwenye ukaguzi wa gawio letu tu ambalo litakuwa katika mfuko maalumu.

Aina ya Mradi huu ni bandari ya Dubai inayolisha Afrika, na hata wasanifu walikwenda Dubai kupata uzoefu...

Hoja ya miaka mkataba wa 99 badala ile ya pendekezo la TZ la miaka 33 kisha kufanya marejeo, ilikuwa ya msingi na inajadilika lakini sio ya kuvunja mradi.

Kwa nadharia hii inaonyesha sisi kama taifa tumefeli juu ya mkakati wa kikanda wa wa kiuchumi wa kupambana na watani wetu wa jadi Kenya na Rwanda. Hapa ndipo hoja ya kubadili muundo wa idara yetu ya Usalama wa Taifa inapopata mashiko.

Tunakimbizana na ndege ambazo sio biashara ya kinchi yenye mafaa kwa dunia ya leo
 
@="Kichuguu,

Mwalimu unahimiza watu kusoma lakini wakati huo unapinga Tafiti za kisomi

Utafiti hupingwa kwa utafiti mbadala siyo maoni ya jumla jumla

Kama Maprofesa wetu nguli Mruma na Osoro wamefanya utafiti wa kisomi na kukuta tumeibiwa Trilion 424 na ripoti yao ikasomwa mbele ya Taifa zima na mbele ya mheshimiwa rais wewe ni nani hata uje useme kuwa finding hiyo ni upuuzi mtupu?.
Haya hebu tuambie basi kama siyo Trilion 424 tulizoibiwa na ACACIA tumeibiwa kiasi gani?

Utafiti hupingwa kwa utafiti siyo blah blah
 
Nitajibu mada hii baadaye nikipumzika kutoka shamba; Mheshimiwa Zito anatumia maoni ya mhariri wa gazeti la Citizen kujenga hoja yake wakati hata mhariri mwenyewe amesema "Kenya banks on" yaani kwa kiswahili rahisi ni kuwa Kenya inacheza karata yake kwenye mradi huo. Kucheza karata ni patapotea, hakuna maana ya kushinda. Hata walipoanza kujenga SGR kuimarisha Northern corridor walisema vivyo hivyo, lakini sasa hivi wanasema SGR ni white elephant. Kuchambua mikataba ni jambo la muhimu sana kuliko kukurupuka kwa vile jirani kafanya jambo kama hilo.Mradi wa Bagamayo ni mzuri tu iwapo una mkataba mzuri, siyo uruhus badnari ijengwe halafu seriklali isiwe na mamlaka ya kuingia ndani au kupanua bandari nyinge.. Wakati Lamu inajwengwa, Mheshimiwa Zito angetuletea mkataba wa Lamu halafu akachambua uzuri wake huku alkiulinganisha na wa Bagamoyo; siyo ngonjera tu.
Man, let's be honest! Hivi unaamini kabisa kabisa kwamba Mchina alitaka akishajenga hiyo bandari basi serikali isitie pua yake pale?! Do you?!

Mimi katika utafiti wangu kwenye masuala ya BOT, sijawahi kusikia popote duniani kwamba kuna mikataba ya aina hiyo!! Ambacho labda angefanya Mchina (based on our research), almost kile kile kinachofanyika kwenye FDI zingine ambazo sio BOT.

Kwa mfano... Tax Holiday! Hili lipo sio kwa Mchina tu na Bandari ya Bagamoyo bali hata kwenye miradi ya aina nyingine!

Pili, VAT and/or any other Tax Exemption kwa vifaa vitakavyotumuika kujenga bandari na industrial complex! Hili nalo halitokani na Mchina na Bandari ya Bagamoyo bali ni mambo yanayofanyika duniani kote including na sisi wenyewe!!

Tatu, Income Tax Exemption...!! Kama nilivyosema mara kadhaa, kodi is always mali ya serikali bila kujali itakusanywa na nani, na kwahiyo ambacho angepata Mchina ni kama kile anachopata leo hii Mamlaka ya Bandari; yaani tozo mbalimbali lakini kodi on imports, exports na zingine zinaenda kwa TRA!!

Hapa Mchina angefanya jaribio la kusamehewa income tax lakini sio kwamba eti kodi ingechukuliwa na Mchina!

Kwamba eti Mchina alitaka tusiendeleze bandari!! Bandari zipi?! Ya Lindi au ya Kilwa?! Au zile za Ziwa Tanganyika, Victoria na Nyasa?!

Kama ni Bandari ya Tanga, mbona basi kabla JK hajatoka kulikuwa na mpango wa kuendeleza Bandari ya Tanga ili ku-cater mafuta ya Tanga?!

Au Bandari ya Mtwara?! Kama ni Bandari ya Mtwara mbona tangia awamu ya wakati lilipokuja suala la gas Bandari ya Mtwara ilianza kuendelezwa ili ku-cater meli za kusafirisha gas?!

Au wanataka kutuambia walikuwa na mpango wa kuziendeleza hizo bandari kama bandari za kawaida kama ilivyo ya Dar?! Kama ndivyo, ina maana CCM hii hii iliyoziua Bandari za Lindi na Kilwa huku wakiiacha ya Tanga ikiwa ICU leo ndo wangeziendeleza hizo bandari baada ya kuona Mchina anajenga Bandari ya Bagamoyo?!

Au uendelezaji wa Bandari ya Dar es salaam?! Kama ndivyo, mbona mpango wa uendelezaji wa hizi berth za sasa ulikuwepo tangia zamani?! Au walitaka kuibadili Dar port kuwa kama Durban Port ingawaje hawakuweza kufanya hivyo over the past 50 years?!

Btw, hivi hiyo Bandari ya Dar es salaam unaendeleza hadi wapi ikiwa hadi sasa tayari 90% ya Kurasini imeshavunjwa?! Au walitaka kuendeleza bila kuwa na eneo for container terminal?! Au ndo wanataka kutuambia the government was prepared kuibomoa Tarafa mzima ya Chang'ombe?!

If YES, taabu yote hiyo ya nini?! Why should we keep abolishing residential areas wakati Bagamoyo pako tupu?!

Sina shaka hata kidogo kwamba wewe hauwezi kuwa miongoni mwa wale wanaoamini mradi ulitakiwa uende Bagamoyo kwavile JK anapendelea kwake!!
 
LOoo! Chige Bhwanah. Unanikumbusha yale makinikia na malori ya tani sabasaba ya dhahabu tupu!

Na mara Paa! SGR ikaenda kwa waturuki! Hivi kweli tunajua sababu zilizosababisha badiliko hilo la ghafla? Huyu Kikwete na watu wake wote walikuwa hawalitakii mema taifa hili?

Heshima sana mkuu Chige.

Hili la kusema uongo ni tatizo kubwa. Na kweli, lengo ni hilo hilo ulilotaja. Sifa.

Pengine siku moja itatokea watu wajue ukweli. Sasa hapo hata kama atakuwa amejijengea 'legacy' ya kuyajenga yote hayo yeye, watu watamdharau kwa ubabaishaji aliolifanyia taifa kwa kujitafutia sifa binafsi.
Hahaahaaa!! Bila kusahau kauli nyingine ya Magu kwamba Watanzania tukijua dhahabu iliyojaa mle, basi tungelia; matokeo yake badala ya kulia, wanaishia kukubali 700B badala ya 425 Trillion walizoamisha watu!!!
 
Man, let's be honest! Hivi unaamini kabisa kabisa kwamba Mchina alitaka akishajenga hiyo bandari basi serikali isitie pua yake pale?! Do you?!

Mimi katika utafiti wangu kwenye masuala ya BOT, sijawahi kusikia popote duniani kwamba kuna mikataba ya aina hiyo!! Ambacho labda angefanya Mchina (based on our research), almost kile kile kinachofanyika kwenye FDI zingine ambazo sio BOT.

Kwa mfano... Tax Holiday! Hili lipo sio kwa Mchina tu na Bandari ya Bagamoyo bali hata kwenye miradi ya aina nyingine!

Pili, VAT and/or any other Tax Exemption kwa vifaa vitakavyotumuika kujenga bandari na industrial complex!

Tatu, Income Tax Exemption...!! Kama nilivyosema mara kadhaa, kodi is always mali ya serikali, na kwahiyo ambacho angepata Mchina ni kama kile anachopata leo hii Mamlaka ya Bandari; yaani tozo mbalimbali lakini kodi on imports and exports inaenda kwa TRA!! Hapa Mchina angefanya jaribio la kusamehewa income tax lakini sio kwamba eti serikali isikusanye kodi!

Kwamba eti Mchina alitaka tusiendeleze bandari!! Bandari ipi?! Ya Lindi au ya Kilwa?! Au zile za Ziwa Tanganyika, Victoria na Nyasa?!

Kama ni Bandari ya Tanga, mbona basi kabla JK hajatoka kulikuwa na mpango wa kuendeleza Bandari ya Tanga ili ku-cater mafuta ya Tanga?!

Au Bandari ya Mtwara?! Kama ni Bandari ya Mtwara mbona tangia awamu ya wakati lilipokuja suala la gas Bandari ya Mtwara ilianza kuendelezwa ili ku-cater meli za kusafirisha gas?!

Au wanataka kutuambia walikuwa na mpango wa kuziendeleza hizo bandari kama bandari za kawaida kama ilivyo ya Dar?! Kama ndivyo, ina maana CCM hii hii iliyoziua Bandari za Lindi na Kilwa huku wakiiacha ya Tanga ikiwa ICU leo ndo wangeziendeleza hizo bandari baada ya kuona Mchina anajenga Bandari ya Bagamoyo?!

Au uendelezaji wa Bandari ya Dar es salaam?! Kama ndivyo, mbona mpango wa uendelezaji wa hizi berth za sasa ulikuwepo tangia zamani?! Au walitaka kuibadili Dar port kuwa kama Durban Port ingawaje hawakuweza kufanya hivyo over the past 50 years?!

Btw, hivi hiyo Bandari ya Dar es salaam unaendeleza hadi wapi ikiwa hadi sasa tayari 90% ya Kurasini imeshavunjwa?! Au walitaka kuendeleza bila kuwa na eneo for container terminal?! Au ndo wanataka kutuambia the government was prepared kuibomoa Tarafa mzima ya Chang'ombe?!

If YES, taabu yote hiyo ya nini?! Why should we keep abolishing residential areas wakati Bagamoyo pako tupu?!

Sina shaka hata kidogo kwamba wewe hauwezi kuwa miongoni mwa wale wanaoamini mradi ulitakiwa uende Bagamoyo kwavile JK anapendelea kwake!!
Well argued. Watu wengi wameacha kufikiri na kuchambua na kubakia na kuunga mkono kila anachotamka Rais hata kama kimekosa mantiki.
 
Back
Top Bottom