Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Mkuu issues muhimu kama hii acha ielezwe hata kitabu kizima, siku zote Watanzania ni wavivu kusoma so let us read and analyse.
 
Mkuu mimi ninafikiri tunaongea lugha moja,uzalishaji ni uzalishaji uwe wa bidhaa au huduma.
Labda tusaidiane,mbona kwenye sekta ya Mawasiliano tumeweza?
Mafanikio kwenye sekta ya mawasiliano siyo tiketi ya kufanikiwa moja kwa moja kwenye sekta ya nishati. Jambo muhimu kukumbuka ni kwamba: Mahitaji, Mazingira, Faida na Changamoto baina ya hizi sekta mbili hapa nchini hayafanani kabisa. Hivyo suala zima la mashirika binafsi liangaliwe vizuri na lifanyiwe mjadala mpana.

Lakini mimi naweza kuuliza tu: Unasema sekta ya mawasiliano tumeweza, lakini tukijifananisha na wenzetu wa nchi jirani kama Rwanda na Sudan unadhani kasi yetu inaridhisha ??? Hii ni mada pana ambayo inahitaji tuianzishie uzi wake kabisa siku nyingine. Kwasasa tujikite kwenye hili la nishati.
 
Mbona jibu lipo wazi? Angepata wapi finances zakuujenga kama asingechukua huo wa kibiashara usio na masharti magumu zaidi ya riba?

We ukaombe pesa kwa mtu anayekugomea kujenga mradi hata kwa pesa zako? Wangempa? Mbona hii ipo so direct huhitaji hata kufikiri sana?

Mradi huu wa umeme wa maji hata riba ingekuaje kwa jinsi alivyouweka ulikuwa siyo exclusive ungeweza kujilipa na baadaye kujiendesha vizuri tu na kwa manufaa ya taifa. Hii ni kwasababu ulikuwa planed naukawa linked with other projects kama za viwanda ambavyo ulisikia kila mara akiviongelea vinajengwa na alisisitiza vijengwe pamoja na kuboresha kilimo nadhani ilikuwa ni baada ya kumaliza hizi project kubwa kubwa. Zote hizi zikichangizwa na ujengaji miundombinu ya usafiri ambazo kwa pamoja zingeipeleka production function ya nchi juu sana kwakukutoa formal employments kwa milions of youths ambao wangeinua pato la taifa through spending kupitia salaries zao ambazo ni determined na siyo probable kama wangejiajiri au kuishia kuwa street hawkers ambao kwanza wanauza vitu cheap kutoka mataifa ya nje na hasa China na ku spend kwa basic service kama nauli na hospitali tupo, ambapo dawa zinatoka nje na mafuta ya transport yanatoka nje pia iki imply hasara i.e capital flight, huku local products kama crops zikikosa soko kwakua watu hawana vipato. Besides, kupitia payee zao hao (formally employed youth) tax base ingeongezeka na kupelekea kuongeza uhakika wa mapato ya serikali badala ya kukimbizana na tozo.

Ni kwavile tu watu wanaangalia miradi kwa jicho la faida binafsi lakini taifa lolote lile ili lilete mageuzi ya haraka mambo ya msingi ni energy na infrastructure kama base then ndiyo production inayokuwa subsidized inafuatia baada ya hapo ili kujenga uwezo, kisha baada ya hapo zinakuwa released kuongeza efficiency through competition. Competition huruhusiwa baada ya frame nzima kutokea kuanzia farm gate productions, intermediaries i.e wafanya biashara na wasafirishaji kuji organize mpaka final consumption kwa maana ya market chains; ndipo basi huko mbeleni third phase, ndiyo mambo ya value addition, quality, standardization and specifications zenye linkages both vertical and lateral kuenda kwenye cluster value chains formation hufuata, hatimaye kuwa full developed economy kama za wenzetu; which means base au foundation ikiwa nzuri, kitu ambacho JPM alikuwa ndicho anakijenga, value addition and flows zake through chains and other channels .ie lateral inakuwa ni outcome ya automatic.

Kwa mtizamo wangu; Magufuli alikuwa ana maono mazuri na yenye tija kubwa kwa taifa letu, TATIZO KUBWA SANA, alitumia common sense zaidi na pengine alikosa programmers wazuri either kwakua hawapo wakutosha ama waliokuwa karibu naye walikuwa wababaishaji au alikuwa mbishi asiyependa kusikiliza, sijui sana sababu hapa na speculate tu....Pia nadhani alikosa watu ambao wanaelewa vizuri maono yake ambao wange weza kuyabeba hayo baada yake, leo tusingekuwa na shida ya kuona mwendelezo usio na confusion ndani yake...

Hata hivyo bado kama taifa tunaweza kukubali kukaa na kuelewa hayo maono na kuyapeleka ili sote tufaidike kuliko kila mara kuanza moja kila mara uongozi unapogeuka...
 
Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Acha uvivu, kusoma kwa umakini na kwa urefu kunakufanya usizeeke....Kinachozeeka ni ubongo usiopokea challenge yeyote na huo uzee unakuwa reflected kwenye physical body...
 
Tatizo letu ni poverty, kuna watu walishaona wanaenda kupata pension yao safi kabisa, zilivyokatizwa wakajaa hasira kwakisingizio cha master plan...Nchi hii tunatatizo la selfishness inayoletwa na poor people time preferences...Hakuna masikini anayekubali kuwekeza hata siku moja; they always think of now not tomorrow!
 
This is the most balanced opinion, so far: Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu.
 
Itoshe tu kusema ahsante sana! Umechambua vizuri sana. Naamini wahusika wanapita humu na watafanyia kazi.
 
Sasa Stiglers Gorge (JNHPP) likijengwa kwa haraka haraka, dili za pesa za kuhonga maskini tsheti, kofia na khanga 2025 zitatoka wapi?

Tulia kwanza tuchote pesa za uchaguzi. Mambo ya mabwawa yapo na yataendelea kuwepo.
 
This is the most balanced opinion, so far: Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu.
Karibu, naamini tunajenga nchi yetu kwa faida ya sisi na vizazi vyetu. After all I am done with my personal life, kilichobaki ni kusaidia nchi na watu wake...Sina matamanio mengine yeyote katika maisha yangu zaidi ya hapa nilipofika
 
Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
Sasa na ww tueleze umeme wa maji si rafiki wa mazingira kivip maana mwenzako tumeshamsoma tayari na ww tusaidie sasa mkuu tuelewe vzr.
 
Kwenye aya za mwanzo kabisa za uzi wangu nimezungumzia GOVERNMENT MONOPOLY. Hebu naomba utueleweshe TANESCO's MONOPOLY inasababishaje tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini na tutumiea mbinu ipi kulitatua tatizo.
Kwa sheria za umeme zilizopo only TANESCO ndio anaruhusiwa kuuza na kusambaza umeme kwa wateja (private company hairuhusiwi labda kwa kibari maalum (rushwa), unaweza kuzalisha umeme lakini lazima umuuzie TANESCO kwa bei atakayokupangia yeye ( rushwa tupu)na yeye ndio auze/asambaze kwa watumiaji, waruhusu watu binafsi wafanye hii biashara 100% bila vikwazo vyovyote soko litaamua
 

Mkuu maelezo yako mbona yako wazi kabisa yanaeleweka…hakuhitaji rocket science kutambua hapo ni vita za kiuchumi…

Big corp wanataka kuuza mafuta na gas na mazao yao mengine….leo upunguze mpunga watakuelewa….kujitegemea ni adui mkubwa wa ubepari…

Hv mazingira vs faida itakayopatikana kwenye jamii na serikali kwa ujumla wamezipima…maana mimi ninachojua Kilimanjaro kule mito imekauka sio kwasababu ya mabwawa….watu wanakata miti misituni kutengeneza mikaa na mengineo…na bado wanawasha vibatari vya mafuta ya taa kukwepa gharama za umeme…umeme ni anasa…mtu akitaka kufungua mradi unaotumia umeme inabidi atafakari anafanyaje ili aweze kupunguza gharama ili bidhaa zake ziuzike…
 
Karibu, naamini tunajenga nchi yetu kwa faida ya sisi na vizazi vyetu. After all I am done with my personal life, kilichobaki ni kusaidia nchi na watu wake...Sina matamanio mengine yeyote katika maisha yangu zaidi ya hapa nilipofika
Nashukuru sana mkuu....
 
Binafsi nauunga Sana mkono huu mradi j mzuri mno

Tatizo naloliona hata Kama mradi huu utakamilika sitegemei Bei ya umeme kushuka lakn pia bado kukatika kwa umeme kutabak palepale

Nimejifunza kutoka kwenye gesi tuliaminishwa maneno mengi mzuri lakn mwisho wa siku unaweza kudhan gesi inachimbwa ALABAMA USA inakuja kuuzwa Tanzania

UZALENDO TANZANI INABIDI LIWE SOMO KABISA LA KUFANYIA MTIHANI

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…