Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Mkuu issues muhimu kama hii acha ielezwe hata kitabu kizima, siku zote Watanzania ni wavivu kusoma so let us read and analyse.
 
Mkuu mimi ninafikiri tunaongea lugha moja,uzalishaji ni uzalishaji uwe wa bidhaa au huduma.
Labda tusaidiane,mbona kwenye sekta ya Mawasiliano tumeweza?
Mafanikio kwenye sekta ya mawasiliano siyo tiketi ya kufanikiwa moja kwa moja kwenye sekta ya nishati. Jambo muhimu kukumbuka ni kwamba: Mahitaji, Mazingira, Faida na Changamoto baina ya hizi sekta mbili hapa nchini hayafanani kabisa. Hivyo suala zima la mashirika binafsi liangaliwe vizuri na lifanyiwe mjadala mpana.

Lakini mimi naweza kuuliza tu: Unasema sekta ya mawasiliano tumeweza, lakini tukijifananisha na wenzetu wa nchi jirani kama Rwanda na Sudan unadhani kasi yetu inaridhisha ??? Hii ni mada pana ambayo inahitaji tuianzishie uzi wake kabisa siku nyingine. Kwasasa tujikite kwenye hili la nishati.
 
Mkuu huku tunakorudi hatutapiga hatua, ni sawa na kukanyaga mafuta mengi wakati gari iko kwenye free gear!
Hiyo power master plan yenyewe mwendazake aliibadilisha akaweka huo mradi..
Mjadala nadhani ungekua kwamba;
※ Kwanini aliamua kufinance hiyo project kwa mikopo ya kibiashara tena ya muda mfupi na riba kubwa. Juzi tumeambiwa marejesho yameshaanza na project haijakamilika ikabidi tutumie mkopo mwingine kulipa huo mkopo kitu ambacho nakiona kama ukichaa!
Mbona jibu lipo wazi? Angepata wapi finances zakuujenga kama asingechukua huo wa kibiashara usio na masharti magumu zaidi ya riba?

We ukaombe pesa kwa mtu anayekugomea kujenga mradi hata kwa pesa zako? Wangempa? Mbona hii ipo so direct huhitaji hata kufikiri sana?

Mradi huu wa umeme wa maji hata riba ingekuaje kwa jinsi alivyouweka ulikuwa siyo exclusive ungeweza kujilipa na baadaye kujiendesha vizuri tu na kwa manufaa ya taifa. Hii ni kwasababu ulikuwa planed naukawa linked with other projects kama za viwanda ambavyo ulisikia kila mara akiviongelea vinajengwa na alisisitiza vijengwe pamoja na kuboresha kilimo nadhani ilikuwa ni baada ya kumaliza hizi project kubwa kubwa. Zote hizi zikichangizwa na ujengaji miundombinu ya usafiri ambazo kwa pamoja zingeipeleka production function ya nchi juu sana kwakukutoa formal employments kwa milions of youths ambao wangeinua pato la taifa through spending kupitia salaries zao ambazo ni determined na siyo probable kama wangejiajiri au kuishia kuwa street hawkers ambao kwanza wanauza vitu cheap kutoka mataifa ya nje na hasa China na ku spend kwa basic service kama nauli na hospitali tupo, ambapo dawa zinatoka nje na mafuta ya transport yanatoka nje pia iki imply hasara i.e capital flight, huku local products kama crops zikikosa soko kwakua watu hawana vipato. Besides, kupitia payee zao hao (formally employed youth) tax base ingeongezeka na kupelekea kuongeza uhakika wa mapato ya serikali badala ya kukimbizana na tozo.

Ni kwavile tu watu wanaangalia miradi kwa jicho la faida binafsi lakini taifa lolote lile ili lilete mageuzi ya haraka mambo ya msingi ni energy na infrastructure kama base then ndiyo production inayokuwa subsidized inafuatia baada ya hapo ili kujenga uwezo, kisha baada ya hapo zinakuwa released kuongeza efficiency through competition. Competition huruhusiwa baada ya frame nzima kutokea kuanzia farm gate productions, intermediaries i.e wafanya biashara na wasafirishaji kuji organize mpaka final consumption kwa maana ya market chains; ndipo basi huko mbeleni third phase, ndiyo mambo ya value addition, quality, standardization and specifications zenye linkages both vertical and lateral kuenda kwenye cluster value chains formation hufuata, hatimaye kuwa full developed economy kama za wenzetu; which means base au foundation ikiwa nzuri, kitu ambacho JPM alikuwa ndicho anakijenga, value addition and flows zake through chains and other channels .ie lateral inakuwa ni outcome ya automatic.

Kwa mtizamo wangu; Magufuli alikuwa ana maono mazuri na yenye tija kubwa kwa taifa letu, TATIZO KUBWA SANA, alitumia common sense zaidi na pengine alikosa programmers wazuri either kwakua hawapo wakutosha ama waliokuwa karibu naye walikuwa wababaishaji au alikuwa mbishi asiyependa kusikiliza, sijui sana sababu hapa na speculate tu....Pia nadhani alikosa watu ambao wanaelewa vizuri maono yake ambao wange weza kuyabeba hayo baada yake, leo tusingekuwa na shida ya kuona mwendelezo usio na confusion ndani yake...

Hata hivyo bado kama taifa tunaweza kukubali kukaa na kuelewa hayo maono na kuyapeleka ili sote tufaidike kuliko kila mara kuanza moja kila mara uongozi unapogeuka...
 
Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Acha uvivu, kusoma kwa umakini na kwa urefu kunakufanya usizeeke....Kinachozeeka ni ubongo usiopokea challenge yeyote na huo uzee unakuwa reflected kwenye physical body...
 
Mtu kama wewe hujui maana ya mazingira. Nenda kasome taarifa ya Three gorges dam ya china. What is Selous? What is that JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala useless master plan? Hiyo waliyojaza umeme wa solar? Miaka yote ya Tanesco ya Ngereja, Muhongo, etc. ulitegemea iandike master plan ya maana?
Tatizo letu ni poverty, kuna watu walishaona wanaenda kupata pension yao safi kabisa, zilivyokatizwa wakajaa hasira kwakisingizio cha master plan...Nchi hii tunatatizo la selfishness inayoletwa na poor people time preferences...Hakuna masikini anayekubali kuwekeza hata siku moja; they always think of now not tomorrow!
 
Mbona jibu lipo wazi? Angepata wapi finances zakuujenga kama asingechukua huo wa kibiashara usio na masharti magumu zaidi ya riba?

We ukaombe pesa kwa mtu anayekugomea kujenga mradi hata kwa pesa zako? Wangempa? Mbona hii ipo so direct huhitaji hata kufikiri sana?

Mradi huu wa umeme wa maji hata riba ingekuaje kwa jinsi alivyouweka ulikuwa siyo exclusive, bali ulikuwa planed na other linked projects kama za viwanda ambavyo ulisikia kila mara akiviongelea vinajengwa na alisisitiza vijengwe pamoja na kilimo , zote hizi zikichangizwa na ujengaji miundombinu ya usafiri ambazo kwa pamoja zingeipeleka production function ya nchi juu sana kwakukutoa formal employments kwa milions of youths ambao wangeinua pato la taifa through spending kupitia salaries zao ambazo ni determined na siyo probable kama wangejiajiri au kuishia kuwa street hawkers ambao kwanza wnauza vitu cheap kutoka mataifa ya nje na hasa China na ku spend kwa basic service kama nauli na hospitali ambapo dawa zinatoka nje na mafuta ya transport yanatoka nje i.e capital flight huku local products kama crops zikikosa soko kwakua watu hawana vipato; kupitia payee zao tax base ingeongezeka na kuongeza uhakika wa mapato ya serikali badala ya kukimbizana na tozo...

Ni kwavile tu watu wanaangalia miradi kwa jicho la faida binafsi lakini taifa lolote lile ili lilete mageuzi ya haraka mambo ya msingi ni energy na infrastructure kama base then ndiyo production inakuwa subsidized infuata ili kujenga uwezo kisha baada ya hapo zinakuwa released kuongeza efficiency through competition baada ya frame nzima kutokea kuanzia farm gate intermediaries mpaka final consumption na huko mbeleni third phase ndiyo mambo ya value addition, quality na linkages both vertical and lateral kuenda kwenye cluster value chain formation; which means basi ikiwa nzuri value addition and flows zake through chains and other channels .ie lateral inakuwa ni outcome ya automatic.

Magufuli alikuwa ana maono TATIZO KUBWA SANA alitumia common sense zaidi na pengine alikosa programmers wazuri either kwakua hawapo wakutosha na waliokuwa karibu naye walikuwa wababaishaji au alikuwa mbishi asiyependa kusikiliza, sijui sana sababu hapa na specukate tu....Pia nadhani alikosa watu ambao wanaelewa vizuri maono yake ambao wangebeba weza kuyabeba hayo baada yake, leo tusingekuwa na shida ya kuona mwendelezo usio na confusion ndani yake...

Hata hivyo bado kama taifa tunaweza kukubali kukaa na kuelewa hayo maono na kuyapeleka ili sote tufaidike kuliko kila mara kuanza moja kila mara uongozi unapogeuka...
This is the most balanced opinion, so far: Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu.
 
Itoshe tu kusema ahsante sana! Umechambua vizuri sana. Naamini wahusika wanapita humu na watafanyia kazi.
 
Sasa Stiglers Gorge (JNHPP) likijengwa kwa haraka haraka, dili za pesa za kuhonga maskini tsheti, kofia na khanga 2025 zitatoka wapi?

Tulia kwanza tuchote pesa za uchaguzi. Mambo ya mabwawa yapo na yataendelea kuwepo.
 
This is the most balanced opinion, so far: Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu.
Karibu, naamini tunajenga nchi yetu kwa faida ya sisi na vizazi vyetu. After all I am done with my personal life, kilichobaki ni kusaidia nchi na watu wake...Sina matamanio mengine yeyote katika maisha yangu zaidi ya hapa nilipofika
 
Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
Sasa na ww tueleze umeme wa maji si rafiki wa mazingira kivip maana mwenzako tumeshamsoma tayari na ww tusaidie sasa mkuu tuelewe vzr.
 
Kwenye aya za mwanzo kabisa za uzi wangu nimezungumzia GOVERNMENT MONOPOLY. Hebu naomba utueleweshe TANESCO's MONOPOLY inasababishaje tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini na tutumiea mbinu ipi kulitatua tatizo.
Kwa sheria za umeme zilizopo only TANESCO ndio anaruhusiwa kuuza na kusambaza umeme kwa wateja (private company hairuhusiwi labda kwa kibari maalum (rushwa), unaweza kuzalisha umeme lakini lazima umuuzie TANESCO kwa bei atakayokupangia yeye ( rushwa tupu)na yeye ndio auze/asambaze kwa watumiaji, waruhusu watu binafsi wafanye hii biashara 100% bila vikwazo vyovyote soko litaamua
 
Wazungu husema hivi "Once is an accident, Twice is a Coincidence, but Thrice is a Pattern".

Hapa namaanisha nini, duniani kote ambako miradi ya namna hii yenye lengo la kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umasikini lazima kuwepo na malalamiko.

Tena nimefuatilia kwa umakini na kufahamu kwamba malalamiko hayo ni lazima yafanane. Mbaya zaidi makundi ya wanaoleta haya malalamiko huwa ni ya watu wa aina ileile, tena huja na sababu zilezile.

Ukifuatilia kwa umakini, utatambua kwamba mfanano wa hawa watu ni mkubwa sana hadi utakubaliana na ule msemo wa kiingereza kwamba "History does not repeat itself, but people do repeat themselves".

Fanya utafiti wako binafsi, utakubaliana na nilichokiandika hapa.

Muda ni mchache, leo hii ntazungumzia nchi tatu ambazo ni Marekani, Ethiopia na Tanzania. Ambako kote katika nyakati tofauti kumekuwa na miradi mikubwa ya kuzalisha umeme wa maji ambao kwa mkono wa serikali, ambayo imelenga kuzalisha umeme wa gharama nafuu kwa wananchi huku miradi hiyo ikiendeshwa na serikali.

Hapa nazungumzia miradi ya The Tennessee valley Hydro-electric Power Projects (TVA), The Grand Ethiopian Rennaisance Dam (GERD) na Julius Nyerere Hydro- Power Project (JHPP).

Nimefuatilia kwa karibu nimeona kwenye hii miradi ya TVA, GERD na JNHPP ni lazima utakutana na majina kama WHITE-ELEPHANTS, DEBT-RIDDEN PROJECTS, UNSUSTAINABLE ENERGY SOURCE, ENVIROMENTAL HAZARDOUS, GOVERNMENT MONOPOLY, UNCOMPETITIVE SOEs na SOCIALIST EMBARKED PROJECT.

Mpaka sasa sijafahamu kwanini tokea kule Marekani, Ethiopia hadi Tanzania mambo yafanane hivi. Imetokea TVA (Once=An Accident), Imetokea GERD (Twice= A Coincidence) na Imetokea Tanzania (Thrice= A Pattern).

Pia sehemu nyinginezo yanaendelea kutoka tu, mpaka najiuliza nini hiki. Labda, huenda ni mawazo yangu hafifu tu, ambapo wazungu husema "A figment of your own imagination"

HEBU TUANGALIE MRADI WA UMEME CHINI YA TENNESSEE VALLEY AUTHORITY

Raisi Franklin Delano Roosevelt alianzisha The Tennessee Valley Authority (TVA) mwaka 1933 ili kuwezesha Marekani izalishe umeme wa bei ndogo ambao utasaidia majimbo kama saba ambayo yanazunguka lile eneo.

Lengo kubwa ni kusaidia kiuchumi ukanda ambao uliachwa nyumba kimandeleo, kutoa ajira kwa vijana na kusukuma uchumi wa viwanda eneo hilo.

Tokea mwaka 1933 mpaka sasa Marekani imefanikiwa kutengeneza mabwawa 50 ambayo yanasaidia kuzalisha umeme wa bei ndogo unaotumika kuendesha viwanda na uchumi wa majimbo karibia saba ya eneo ambalo bonde la Tennessee limepita.

Ila huwezi amini mpaka leo hii mwaka 2022, wanaharakati wa kimazingira wanapinga huu mradi kwa kusema unaleta madhara.

Wakati nasoma shule kuhusu huu mradi, tuliambiwa kwamba ulipigwa vita sana na makampuni binafsi ya umeme, wanasiasa, wanaharakati na wanasheria.

Ambapo walitumia mbinu mbalimbali kufanikisha hujuma dhidi ya huu mradi lakini hawakufanikiwa. Sababu kubwa ni kwamba raia wengi wa Marekani walikuwa ni watu wanaojielewa mno, siyo wajinga wanaopelekeshwa bila kufahamu linaloendelea (Dumbed-Down Citizenry) nchini kwao.

Upinzani haukishia kwenye uanzishwaji wa huu mradi mwaka 1933, mwaka 1936 mmoja wa wamiliki wa hisa kwenye kampuni binafsi la umeme THE ALABAMA POWER COMPANY aitwaye ASHWANDER alipeleka kesi mahakamani kuzuia serikali kuuza umeme kupitia The Tennessee Valley Authority (TVA) akisema kwamba serikali haitakiwi kabisa kuuza umeme hivyo kuna uvunjifu wa katiba ya Marekani.

Unaweza kutafuta kesi ya: Ashwander V Tennessee Valley Authority (1936)

Mahakama ya juu ya Marekani ilikataa na kusema uzalishaji huu wa umeme siyo wa faida tu, bali ulilenga kutoa huduma kwa kukuza uchumi wa eneo ambalo lilikuwa nyuma kimaendeleo na kuimarisha ulinzi wa nchi kwasababu viwanda vya silaha vilikuwepo eneo hilo.

Hivyo mabwanyeye wakapigwa chini na serikali inauza umeme kwa raia mpaka leo hii. Ikumbukwe inayofanya hivi ni serikali ya Kibeberu ya ulimwengu wa kwanza na siyo serikali ya Kijamaa ya ulimwengu wa tatu.

Wamarekani zaidi ya milioni 9 wanapata huduma ya umeme nafuu kutoka kwenye miradi 29 ya umeme wa maji kutoka Tennessee Valley Authority (TVA).

Kubwa zaidi ni kwamba huduma ya umeme kwenye majimbo hayo yanayopitiwa na bonde la Tennessee ni moja kati ya umeme wenye gharama nchini Marekani, kama siyo ndiyo wenye gharama nafuu zaidi kwenye nchi hiyo.

Kitakachoshangaza watu werevu ni kwamba PROPAGANDA CHAFU na UZANDIKI dhidi ya mradi huu hazijaisha tokea mwaka 1936. Raisi Dwight Eisenhower alishawahi kuutukana huu mradi kwa kuuita maneno kama "Ujamaa nyemelevu" (Creeping Socialism), ilhali mamilioni ya Wamarekani ni wanufaika.

Maneno kama haya hayatakiwi kabisa kutoka kwenye kinywa cha mkuu wa nchi mwenye lengo la kuwakwamua kiuchumi raia wa kawaida, kwasababu faida za mradi ni dhahiri kwa watu wote.

Lengo la Raisi Eisenhower lilikuwa siyo kupinga UJAMAA bali ni kubinafsisha (TVA), lakini akakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wazalendo wa kimarekani na mwishowe akawa mpole.

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba waliompinga ni wenzake kutoka REPUBLICAN PARTY ambao husifika kwa kuchukia UJAMAA hasa pale ambapo serikali yenyewe hufanya biashara. Nini kilipelekea Raisi na jopo la wataalamu wake kupingwa hivi ???

Sasa kubwa na baya zaidi dhidi ya mradi huu ni lile la mwaka 2013, ambapo Raisi Barrack Obama aliandaa muswada ili kubinafsisha The Tennessee Valley Authority (TVA) kwa watu binafsi.

Moja ya sababu kubwa ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ni kwamba mamlaka ya Tennessee Valley (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni mzigo kwa serikali.

Walikuwa na hoja nzito sana maana ukweli ni kwamba mamlaka hiyo (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni takribani dola za kimarekani bilioni 25.

Lakini hili halikuwa sababu ya kusema kwamba serikali ibinafsishe shirika hili la kiserikali na kuwaumiza raia wapatao milioni 9 kwa kupanda kwa gharama za umeme.

Sababu ya pili ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ili kufanikisha ubinafsishwaji wa The Tennessee Valley Authority (TVA) ni ile ambayo hata kwetu huku inatusumbua ya kutunza mazingira.

TVA mbali na miradi 29 ya umeme wa maji, imeongeza pia miradi 12 ya umeme wa makaa ya mawe, miradi 3 ya umeme wa nyuklia, miradi 15 ya umeme wa gesi na mradi 1 wa umeme wa upepo.

Inasemekana TVA inahitaji dola za kimarekani bilioni 25 ili kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababisha na huu mradi hasa kutoka kwenye vinu vya makaa ya mawe. Hivyo ili serikali isiingie kwenye hizi gharama zisizo za msingi, basi ni kheri ibinafsishe tu shirika hili.

Kuna nchi fulani hivi viongozi wake, wasomi na wafanyabiashara wanapenda kuzungumza kauli kama hizi za Raisi Barrack Obama na Dwight Eisenhower, bila shaka ndugu msomaji utakuwa unaifahamu.

Hivyo njia rahisi kwa Serikali ya Raisi Obama, kukwepa deni kubwa la TVA na gharama za marekebisho, wakaona ni bora wauze hii SOE (State Owned Enterprise).

Ila ukweli mchungu ni kwamba wangefanya hivyo ina maana gharama za umeme kwa wananchi wa Marekani zaidi ya milioni 9 ingepanda sana na wangeathiri biashara nyingi na maisha ya raia wa kawaida.

Mbali na madhaifu yake mengi, Marekani ni taifa ambalo raia wake wengi wanajielewa mno.

Wahafidhina wa chama cha REPUBLICAN hasa wawakilishi kutoka majimbo hayo, pamoja na watu binafsi walipinga kwa nguvu mswada ambao ungefanikisha ubinafsishwaji wa kiholela wa hii mamlaka ambayo lengo lake kuu ni kutoa huduma kwa raia na kuimarisha ulinzi wa nchi.

HEBU TURUDI NCHINI TANZANIA SASA, TUANGALIE TANESCO NA JNHPP

Bunge la Marekani lilichofanya ni kukataa mamalaka isiuzwe na kuiwekea ukomo wa deni, ambayo mamlaka haitakiwi kuvuka, ambapo ukomo ni dola za kimarekani bilioni 30.

Hivyo madeni hayapo tu kwenye shirika letu la TANESCO lakini hata TVA wana madeni tena yanakera. Sisemi haya kusema TANESCO inafanya vizuri, la hasha kuna mambo mengi ya ajabu yanafanyika.

Lakini naamini wakijipanga vizuri na kupunguza siasa tunaweza kufika sehemu nzuri sana. Mbona TVA wafananya vizuri na bado ni shirika la serikali ???

Jambo jingine ambalo nalisikia sana nchini Tanzania ni hilo la kusema umeme wa maji siyo endelev. Mimi siyo mtaalamu lakini naweza kufahamu wapi nadanganywa, kiukweli hili linanipa ukakasi mkubwa sana.

Mradi wa TVA umeanza mwaka 1933 na upo hadi leo hii, utasemaje kwamba umeme wa maji siyo endelevu jamani ???

Unaweza kumtukana Raisi Magufuli kwamba ni mjinga, lakini kumbuka huu mpango wa JNHPP umekuwepo tokea enzi za Mzee Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, ina maana hawa wote na wataalamu wao walikuwa ni wajinga kabisa wasitambue kwamba Hydro-Electric Power is not sustainable source of energy ??? Aidha ni kweli sisi watanzania ni watu wajinga sana pamoja na viongozi wetu, AU kuna kitu kinachoendelea nyuma ya pazia sisi raia wa kawaida hatukioni.

Jambo kubwa zaidi la kujiuliza hapa: Ni kwamba kama mradi wa TVA ambao manufaa yake yanaonekana kwa mamilioni ya wananchi wa Marekani unapigwa vita kali hivi, tena hadi na viongozi wa serikali wakiwemo maraisi, sisi huku kwetu Tanzania tusipingwe kweli ???

Mwaka jana miezi ya mwishoni nilikuwa nafuatilia wanaharakati mitandaoni, nikasikia baadhi wakisema mamilioni ya miti yamekatwa na uharibifu mkubwa wa mazingira umefanyika kwenye mradi wa JNHPP ndiyo maana mvua zimegoma Tanzania.

Lakini, wengine wanasema kwamba JNHPP ni tembo mweupe (A White Elephant Project). Majibu ya Waziri Makamba, yamakuwa yakibadilika-badilika. Lakini naamini, ukweli tutaufahamu tu.

Wanaharakati wetu wangepinga huu mradi (JNHPP) peke yake sisi tungeelewa labda na binafsi ningesema hebu tujifanyie tathmini. Lakini hakuna mradi wowote mkubwa ambao umewahi kufanyika nchini Tanzania bila kupata upinzani mkubwa:

Uwe ni mradi wa msaada, uwekezaji au mkopo. Nasema hili kwa UJASIRI WOTE, kama upo naomba nitajiwe ili nijifunze.

Ukifuatilia kinachoendelea kwa wanasiasa wetu kuna sababu nyingi sana zinazoletwa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Wengi wetu ni UJINGA, WOGA, BENDERA FUATA UPEPO lakini kubwa ni ULAJI TU wa watu wachache ambao wamevaa ngozi ya kutunza mazingira, kulinda katiba, matumizi ya mbinu za kisasa za kisayansi na kibiashara kuendesha sekta ya nishati nchini. Lakini ni hivi: UKWELI UKO KAMA MIMBA, HUWEZI KUUFICHA MILELE. Tutafamu tu...

NAMALIZIA NA ETHIOPIA, MRADI WA THE GRAND ETHIOPIAN RENNAISANCE DAM

Ingekuwa Tanzania ndiyo nchi pekee ndiyo inayopigwa vita kwa kuanzisha mradi kama huu ningesema, basi tujifanyie tathmini kidogo.

Ila hadi kule kwa ndugu zetu Ethiopia yametokea machafuko makubwa sana kupinga uanzishwaji wa The Grand Ethiopia Rennaisance Dam (GERD) ambalo litakuwa msaada mkubwa sana kwa mamilioni ya wahabeshi nchini humo.

Upinzani umekuwa mkubwa imefika kipindi kwamba Raisi wa Marekani Donald Trump akaweka bayana kabisa kwamba Misri inaweza kulipua bwana hilo" Egypt might blow up the dam".

WIKILEAKS wanasema kwamba, mradi huu ukimalika hautaisaidia Ethiopia peke yake kuzalisha umeme wa bei ndogo, bali utazalishwa umeme mwingi (Megawatts 5,250) ambao utauzwa hadi nchi jirani kama Sudan na serikali ya Sadani inafahamu hili vizuri kabisa.

Sasa ukifuatilia kwa umakini, kuna wanasiasa wakubwa ambao walisema wazi kwamba mradi wa GERD, hauna manufaa na ni tembo mweupe ( A WHITE ELEPHANT). Moja kati ya watu waliowahi kusema hivi ni Raisi Isaias Afwerki wa Eritrea.

Lakini mradi huu ukikamilika, umeme wa gharama nafuu utafika hadi nchini kwake. Watanzania tujiulize kitu hapa: Kama umeme wa maji siyo wa muda mrefu (Not Sustainable), hivi iweje serikali ya Uchina itupe zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1, ambazo ni sawa na trilioni mbili za kitanzania au zaidi kwenye mradi ?

Asasi za kiraia (NGOs) nazo haziko nyuma katika kutuonesha madhara ya mradi huu wa GERD. NGO maarufu iitwayo INTERNATIONAL RIVERS kutoka California, nchini Marekani iliandaa ripoti kubwa kabisa kuonesha madhara ya mradi huo kwenye mazingira. Wakaenda mbali zaidi na kusema kwamba bwana hili linaweza kuchangia mabadiliko ya hali ya nchi.

Ikumbukwe hawa ndugu zetu wamezungumza sana juu ya miradi ya umeme wa maji nchini Tanzania na Ethiopia.

MWISHO KABISA: MAONI YA WANAZUONI KUHUSU SIASA ZA UMEME NA MABWAWA

Kama umefuatilia siasa za Afrika kwa muda mrefu, utatambua kwamba huu mchezo haujaanza na Tanzania wala Ethiopia. Prof Mike Muller ambaye ni mhandisi kutoka chuo cha Witswatersrand Afrika Kusini, amawahi kuandika na kusema siasa za kupinga miradi mikubwa ya umeme wa maji zilianza mapema nchini Misri kipindi cha Gamal Abdi Nasser ambapo alitaka kujenga bwawa la Aswan (ASWAH HIGH DAM) ambalo lingezalisha MegaWatts 2,100.

Prof Asit K. Biswas amtaalamu wa maji na mazingira, ambaye ndiye anaongoza kwa kufanyiwa rejea za kitaalamu linapokuja suala za mazingira na maji, akishirikiana na Prof Cecilia Tortajada waliandika chapisho ambalo limesema kwamba mradi wa BWAWA LA ASWAN una madhara makubwa kwenye mazingira.

Lakini ukweli ni kwamba wataalamu mradi huo ulipokamilika mwaka 1970, ulikidhi nusu ya mahitaji ya umeme nchini Misri.

Ikimbukwe kwamba siasa za ASWAN HIGH DAM ziliwahi kupelekea Misri ivamiwe kijeshi na Uingereza, Ufaransa na Israeli. Nasser alisema alitaifisha Mfereji wa Suez kwasababu maji yake ni muhimu kwa ujenzi wa bwawa la Aswan.

Nasser aliomba msaada kwa serikali ya Raisi Eisenhower ili kujenga bwana la Aswan, lakini Eisenhower aligoma.

Raisi Kennedy alikosoa sana haya maamuzi ya kuvuruga miradi ya Afrika akisema hivi "When we abruptly abandoned the Aswan Dam in Egypt, the Russians went ahead to finance it. While we starve the Development loan Fund, the Sino-Soviet bloc has already passed us in economic assistance to selected key areas" Hili ndilo lilitokea bwawa lilijengwa na Warusi.

Maajabu barani Afrika huwa hayaishi kabisa: Kinachotushangaza wengi wetu leo hii ni kwamba Misri ambao miaka ya nyumba walionewa katika kujengwa bwawa la Aswan (ASWAN HIGH DAM), leo hii wao nao wakishirikiana na mataifa makubwa nje, wanaharakati na asasi kubwa za kiraia, wanafanya hujuma kubwa sana dhidi ya mradi wa GERD nchini Ethiopia.

NB 1: Siasa kama hizi, zilionekana pia kule nchini GHANA kipindi cha marehemu Nkhrumah ambapo alikuwa anataka kujenga bwawa la AKASOMBO (The Akasombo Dam) ili kuzalisha umeme.

Uliundwa mtandao mkubwa sana wa watu ndani na nje ya nchi ili kumzuia. Muda ni mchache sana siwezi kuzungumza kilichotokea.

NB 2: Fanya utafiti wako kuhusu miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kupitia maji (TVA, GERD, JNHPP) pia hata ASWAN HIGH DAM na AKASOMBO DAM utatambua kwamba siasa zake zinafanana.

Wahusika ni walewale, wakitumia mbinu zilezile, sema tu huja wakiwa wamevaa vingago (Masks) tofauti-tofati. Kiufupi hizi siasa zinachezwa sana kitaalamu na wengi wetu tunafuata upepo bila kufanya tafiti binafsi.

Mimi siyo mtaalamu sana wa haya mambo, hivyo naomba wale wajuvi wanisaidie zaidi kuelewa. Nitafurahi kurekebishwa na kuelekezwa pale ambapo nimepotoka na kutofahamu kinachoendelea.

CC: JokaKuu , Nguruvi3 , UmkhontoweSizwe , TUJITEGEMEE

Mkuu maelezo yako mbona yako wazi kabisa yanaeleweka…hakuhitaji rocket science kutambua hapo ni vita za kiuchumi…

Big corp wanataka kuuza mafuta na gas na mazao yao mengine….leo upunguze mpunga watakuelewa….kujitegemea ni adui mkubwa wa ubepari…

Hv mazingira vs faida itakayopatikana kwenye jamii na serikali kwa ujumla wamezipima…maana mimi ninachojua Kilimanjaro kule mito imekauka sio kwasababu ya mabwawa….watu wanakata miti misituni kutengeneza mikaa na mengineo…na bado wanawasha vibatari vya mafuta ya taa kukwepa gharama za umeme…umeme ni anasa…mtu akitaka kufungua mradi unaotumia umeme inabidi atafakari anafanyaje ili aweze kupunguza gharama ili bidhaa zake ziuzike…
 
Karibu, naamini tunajenga nchi yetu kwa faida ya sisi na vizazi vyetu. After all I am done with my personal life, kilichobaki ni kusaidia nchi na watu wake...Sina matamanio mengine yeyote katika maisha yangu zaidi ya hapa nilipofika
Nashukuru sana mkuu....
 
Binafsi nauunga Sana mkono huu mradi j mzuri mno

Tatizo naloliona hata Kama mradi huu utakamilika sitegemei Bei ya umeme kushuka lakn pia bado kukatika kwa umeme kutabak palepale

Nimejifunza kutoka kwenye gesi tuliaminishwa maneno mengi mzuri lakn mwisho wa siku unaweza kudhan gesi inachimbwa ALABAMA USA inakuja kuuzwa Tanzania

UZALENDO TANZANI INABIDI LIWE SOMO KABISA LA KUFANYIA MTIHANI

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom