Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Tenesse Valley Authority (TVA) haikuwa mahususi kwa ajili ya kuzalisha umeme bali kuinua uchumi wa maeneo yanayoizunguka kupitia usafiri wa majini, uwekezaji wa viwanda vya mbolea,mipango mji na pia kupambana na mafuriko.Hii ni tofauti sana na bwawa la Stiglerz ambalo uharibifu mkubwa wa mazingira unafanyika kuzalisha umeme ambao ungeweza kuzalishwa na kuzidi kwa gesi na vyanzo vingine vya nishati mbadala.
 
Marekani, Misri na kwingine kokote walipojenga mabwawa makubwa ya umeme uharibifu wa mazingira umekuwepo, huwezi kujenga bwawa kubwa la umeme bila kuharibu mazingira.
Mkuu, mimi siyo mtaalamu. Nachotaka kueleweshwa ni kwamba kwanini sehemu nyingine duniani kama Marekani na Misri madhara kwenye mazingira yasiwepo, lakini yawepo tu nchini Tanzania. Naomba unidadavulie zaidi nipate kufahamu.......
 
Unapofanya miradi mikubwa ya nchi hutakiwi kuangalia gharama nafuu kwa wananchi, kuna mambo mengine mengi mtambuka ya muhumu yanayopaswa kutazamwa kwa kina.
Management ya uchumi inatakiwa ifanyike katika level ya macro sio micro.

Gesi ingesimamiwa vizuri ingezalisha umeme mwingi kuliko wa Stiglers hata kama ungekuwa wa bei juu kidogo, gesi ingezalisha maelfu ya ajira za moja kwa moja na laki za ajira indrect, gesi ingefungua uchumi wa kusini eneo ambalo liko nyuma sana kimaendeleo, gesi ingeleta kodi kwenye uchumi wa nchi. Umeme wa Stiglers zaidi ya porojo za kuwa wa bei nafuu hautukapa hizi faida nyingine za moja kwa moja kwa uhakika.
 
Umetangulia kujihami kuwa hauna maarifa ya kutosha eneo la mazingira kijiografia,sasa ni hivi...

☆Miradi ya H.E.P sio rafiki kwa mazingira ktk dunia ya sasa hususani nchi za tropic na semi-arid state.

☆Pili,fahamu kuwa hali ya hewa ya USA na hizi nchi zetu za Africa zilizo karibu na equator ni tofauti sana hasa ktk masuala ya water tap and conservation as per global warming effects.

☆FYI...miradi ya HEP kwa nchi zetu kimazingira na sustainability hasara ni kubwa kuliko faida,ivyo basi SIO SAHIHI KUCHUKUA MIFANO YA USA NA KUIAPPLY AFRIKA MAANA NYAKATI NA MAZINGIRA NI TOFAUTI SANA. Naungana na wataalamu wanaopinga miradi hii kwa Africa.

Ata ivyo wanaopinga hawakuacha kutoa solution mbadala,yaani umeme wa upepo ambao ni cheaper na more efficient.
 

Nashukuru sana mtaalam, lakini ningeomba unifahamishe zaidi. Kwanini sehemu za Afrika kama Misri walisema kuna madhara lakini faida zimekuwa ni kubwa zaidi kuliko hizo hasara ??? Lakini pia niulize, hivi kila mradi wa umeme uliopo hapa barani Afrika umechangia kwa kiasi gani kuharibu mazingira AS PER GLOBAL WARMING EFFECTS ???
 
Kama kuna jambo la kumshukuru E.Lowassa ni jinsi alivyosimamia na kuiwekea ngumu Egypt iliyotumika mkataba wa 1929 na kutaka tuchimbe visima ili wao wapate maji ya kumwagilia
Nguruvi3, asante kwa comment nzuri sana na ambazo zinakubaliana na maoni ya baadhi yetu kuwa shida ya maamuzi muhimu katika Taifa letu ni siasa kutangulia utaalam.
Halafu ningependa kukufahamisha kuwa nchi zote za Africa ambazo Nile imepitia au zina maziwa ambayo ni Nile-feeders, zinachezewa mchezo mbaya sana na Egypt. Mwanasiasa yeyote atakayetaka kutumia maji ya Nile kwa wingi, kama kumwagilia na/au kufua umeme, Egypt iko tayari kuhakikisha anafanyiwa zengewe la kummaliza kisiasa au hata kuuwawa. La kwanza ndilo lililomkuta Lowasa. Lakini lilifanyika kisiri sana kupitia siasa na watu waliokuwa wamelipwa. Sasa hivi wameweza kupenyeza vizuri mno ndani ya siasa zetu, dhubutu atoke mwanasiasa ajaribu ku-support miradi kama iliyokuwa inapendekezwa na Lowassa, hata kwa kutamka nia tu, hatamaliza mwaka. Ili kuua miradi kama hiyo huku kwetu huwa wanajifanya wanatoa ufadhili na fedha za miradi ya kuchimba visima vya maji. Iko kama tunaambiwa, "nyie kiuchumi hamtakiwi kupiga hatua kutuzidi sisi, tulieni kwanza sisi tusonge mbele halafu tutawambia wapi muelekee" Na sisi kupitia siasa zetu tumekubali.
 
Umeisoma sheria iliyoanzisha hii mamlaka ???
 
Unafahamu dhumuni la kuwa na SOEs ndani ya nchi ???
 
Ungefafanua huo uharibifu wa mazingira ni upi ambao gas hauufanyi ila maji ya umeme ndiyo inafanya....Hapa umezungusha tu maneno hujaweka facts
 
Ila wakumbuke siyo miungu wao, ipo weak point yao huwa equation zao huwa zinakataa...God has never left this world to rule by itself...Historia ni mwl mzuri; Egypt iliyotikisa enzi za Yesu leo ipo wapi? Roma iliyotikisa enzi za mafarisayo leo iko wapi...Africa ndiyo ilianza kuebselea kabla ya hizo sehemu zingine na mzunguko unakaribia kutufikia
 

Nashukuru kwa mchango wako mzito mkuu Nguruvi. Umezungumzia mambo mengi sana na kuna baadhi ya sehemu nadhani hatujaelewana vizuri. Lakini haya tuyaache tujikite kwenye hoja ya msingi kabisa: UMEME WA MAJI. Tukiacha siasa za matumbo, kufuata upepo na propaganda, umeme wa maji unatoa suluhisho la muda mrefu na salama kwa mazingira.

Jambo jingine muhimu, makosa aliyofanya Raisi Magufuli kuhusu huu mradi hayageuzi huu mradi kuwa haramu:Masuala kama fedha za huu mradi, kutelekeza miradi mingine muhimu ya umeme kama ule wa gesi na siasa za kukomoana. Hoja hii tumeizungumza hadi kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ambapo tulisema makosa ya ndugu Jakaya hayageuzi huu mradi kuwa haramu. Siasa za kusema kwamba umeme wa maji hautumiki dunia ya leo wengi tunazishangaa kidogo. Tungeelewa labda pale watu wanasema kwamba ujenzi wa JNHPP ni hatari kwasababu umefanywa ndani ya hifadhi. Lakini siyo kutuambia kwamba umeme wa maji ni hatari kwa dunia ya sasa. Hapa tuwaeleweje labda ???

Lakini pili, nilitoa mfano wa TVA kuonesha kwamba kuna mabwawa ya umeme zaidi ya 20 lakini hayaleti madhara kwenye mazingira kama tunavyoambiwa. Wanaharakati wanachopinga pale ni uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe. Upande mwingine ile ni SOE hivyo ina madeni ambayo serikali imeona kuwa ni mzigo, hivyo wanataka kubinafsisha. Mwisho kabisa, ukifuatilia vizuri utafahamu kwamba huu mradi ulianza kupingwa na makampuni binafsi kwasababu yalisema TVA itakuwa ni GOVERNMENT MONOPOLY. Mbona hili liko wazi ???

Lakini tatu, nimesoma chapisho ambalo lilisema kwamba ASWAN HIGH DAM ni janga la kimazingira. Nikaenda zaidi kuweka hadi waandishi, ila mwishoni inaonekana kwamba matokeo yake ule mradi ni mazuri kiuchumi hadi kimazingira. Aliyeyasema haya naye ni mtaalamu ambaye alifanya utafiti wake na nimemuweka hapa. Mambo kama haya yamekuwepo sana hapa Afrika, binafsi siyazungumzii kwasababu nataka kunyoosha kidole kwa wazungu la hasha. Wewe umekuwepo hapa Tanzania kwa muda mrefu, unafahamu dhahiri maneno ya wataalamu naupinzani kutoka nje yamekuwepo tokea tunaanza kufanya miradi kama TAZARA. Sasa hapa utasemaje nawalaumu watu wa nje ilhali huo ndiyo ukweli ???
 


Mkuu hongera Sana Kwa uchambuzi wa kina ulioufanya. Nimejifunza mambo mengi mno.

Ubinafsi ndio tatizo letu kuu
 
Hao wanaopinga huo mradi ni wapumbavu na wanatoa hoja za kipumbavu na nyepesi sana!

Huo mradi umechukua kaeneo kadogo sana ukilinganisha na maelfu kwa malaki ya eka zinazoendelea kupandwa miti kila siku hapa nchini.

Nenda kule iringa na mikoa mingine uone watu wanavyootesha miti kama hawana akili nzuri. Sasa hako kaeneo kadogo kujenga bwawa litakalo tuletea manufaa makubwa kama taifa utasemaje kana haribu mazingira?

Hao wana harakati uchwara wamejifungia ofisini kwenye viyoyozi hawajui chochote zaidi ya porojo tu
 
Gesi imeshauzwa
 
Mqkamba kawekwa hapo Kama mtego huonmradi ukifeli ndio utampoteza makmba kwemy siasa

Mam mjanja kamuweka ili amalize kisiasa huyu makamba
 

Mkulu, Nina hamu sana kujua madhara ya miradi ya HEP kwa mazingira.

Lingine ni kuwa, kama kule jangwani Misri wanatumia Aswan dam with very little effect of evaporation. What about the place where there is a double maxima rainfall!!?
 
Umesikia wapi kua ni mikopo ya muda mfupi?can you provide proof ya haya uyasemayo? au ni maneneo tu ya kuskia aka Umbea?
Mradi hauna ht miaka miaka ht miaka mi3 (construction ilianza 2019)....kwamba walikopa mkopo wa miaka miwili au?imekua personal loan hio au ndo umbumbu wenu?
Acheni kuleta mambo ya vijeweni or story za kuskia zisizokua na evidence humu ndani, msituchukulie wote ma poyoyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…