Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Yaani tuuze gesi nchi za ulaya wakati hapo mttwara kwenyewe hawatumii gesi
 
Tanzania kwa East tu tumepitwa na congo na Rwanda kwa gesi nyingi
 
Naunga mkono hoja, Mama Samia aendelee na kasi hii hii bado kitambo tutafika.
 
Kitu gani kinakufanya uamini Tanzania tuna akili sana tofauti na Waafrika wengine Manelezu ?!
Nchi zote ulizozitaja sio Tanzania. Hata Algeria ni Africa ila wanatumia vizuri resources zao

Watanzania tuna akili nyingi sana. Tulip uone matokeo ndo useme
 
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
View attachment 2128208
uzi wako ni mzuri sana na wenye kutia matumaini hasa kwa sisi watanzania tuliokwisha poteza matumaini

Ila tambua ya kuwa hii sio fursa ya kipekee kwa nchi yetu

tumekuwa na fursa nyingi sana tangu enzi za mwalimu lakini chakuskitisha tumeshindwa kutumia hata moja

lord; nina imani wewe ni mtanzania kama nilivyo mimi na watanzania wengine, nina iman unaijua hii nchi vizur utajiri tulionao

swali la kujiuliza tumenufaika vipi na raslimari tulizo nazo?

madini, bahari, bandari, mawziwa, mito mikubwa, mbuga za wanyama, kilimo, mifugo nk! raslimar zote hizo kwa ujumla zinafanana na iyo gas ukizijumlisha?

lakin cha ajabu mpaka leo hii bado tunalia umaskini
 
Gas yenyewe akina 'sultani mang'ung'o' walishaiuza kwa vipande vya fedha kwa wale pua ndefu.
 
Amani iwe nanyi wadau,

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
Ninukuu katika aya yako ya mwisho, ati, '.....Umasikini itakuwa Historia Tanzania',
Ninasubiri takwimu za kutokomeza umasikini kwa kutumia LNG Plant hapo Lindi.
LNG inamilikiwa na Makampuni makubwa ambayo yaliisha ingia Mikataba na Serikali.
Mgao wa Serikali ni ASILIMIA ngapi ili tuweze kuzungumzia kutokomeza Umasikini?
 
Tanzania kwa East tu tumepitwa na congo na Rwanda kwa gesi nyingi
takwimu zako sio sahihi ndugu, kwenye swala la gas tanzania tuna lita nyingi sana za ujazo, yaan kitakwimu tunaweza tukawa juu sana kidunia
 
Ninukuu katika aya yako ya mwisho, ati, '.....Umasikini itakuwa Historia Tanzania',
Ninasubiri takwimu za kutokomeza umasikini kwa kutumia LNG Plant hapo Lindi.
LNG inamilikiwa na Makampuni makubwa ambayo yaliisha ingia Mikataba na Serikali.
Mgao wa Serikali ni ASILIMIA ngapi ili tuweze kuzungumzia kutokomeza Umasikini?
Nani kakwambia Lindi Kuna LNG plant?
 
takwimu zako sio sahihi ndugu, kwenye swala la gas tanzania tuna lita nyingi sana za ujazo, yaan kitakwimu tunaweza tukawa juu sana kidunia
Huyu msafisha kabuli wa chato pale achana nae tu
 
Tutacheza vipi vizuri wakati mikataba ishasainiwa?
 
uzi wako ni mzuri sana na wenye kutia matumaini hasa kwa sisi watanzania tuliokwisha poteza matumaini

Ila tambua ya kuwa hii sio fursa ya kipekee kwa nchi yetu

tumekuwa na fursa nyingi sana tangu enzi za mwalimu lakini chakuskitisha tumeshindwa kutumia hata moja

lord; nina imani wewe ni mtanzania kama nilivyo mimi na watanzania wengine, nina iman unaijua hii nchi vizur utajiri tulionao

swali la kujiuliza tumenufaika vipi na raslimari tulizo nazo?

madini, bahari, bandari, mawziwa, mito mikubwa, mbuga za wanyama, kilimo, mifugo nk! raslimar zote hizo kwa ujumla zinafanana na iyo gas ukizijumlisha?

lakin cha ajabu mpaka leo hii bado tunalia umaskini
Usiongelee yaliyopita tuongelee sasa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom