mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Kwa mujibu wa takwimu za chumbani kwako sio?Tanzania kwa East tu tumepitwa na congo na Rwanda kwa gesi nyingi
Rwanda Wana gesi...congo piaTanzania kwa East tu tumepitwa na congo na Rwanda kwa gesi nyingi
Kwani unajua hata maana ya LNG?Yaani tuuze gesi nchi za ulaya wakati hapo mttwara kwenyewe hawatumii gesi
Umeishia darasa la ngapi ndugu?Gesi gani? Tanzania haichimbi gesi, gesi inachimbwa na makampuni na ndio wanaamua wamuuzie nani na kwa gharama gani
Nchi zote ulizozitaja sio Tanzania. Hata Algeria ni Africa ila wanatumia vizuri resources zao
Watanzania tuna akili nyingi sana. Tulip uone matokeo ndo useme
uzi wako ni mzuri sana na wenye kutia matumaini hasa kwa sisi watanzania tuliokwisha poteza matumainiAmani iwe nanyi wadau,
Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.
Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.
Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi
Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi
Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.
Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.
Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi
Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana
Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.
Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?
Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.
Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!
Muwe na siku njema!
View attachment 2128208
Kwani unajua hata maana ya LNG?
Ninukuu katika aya yako ya mwisho, ati, '.....Umasikini itakuwa Historia Tanzania',Amani iwe nanyi wadau,
Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!
Muwe na siku njema!
takwimu zako sio sahihi ndugu, kwenye swala la gas tanzania tuna lita nyingi sana za ujazo, yaan kitakwimu tunaweza tukawa juu sana kiduniaTanzania kwa East tu tumepitwa na congo na Rwanda kwa gesi nyingi
Hakika! Naona nuru kubwa mbeleniNaunga mkono hoja, Mama Samia aendelee na kasi hii hii bado kitambo tutafika.
Nani kakwambia Lindi Kuna LNG plant?Ninukuu katika aya yako ya mwisho, ati, '.....Umasikini itakuwa Historia Tanzania',
Ninasubiri takwimu za kutokomeza umasikini kwa kutumia LNG Plant hapo Lindi.
LNG inamilikiwa na Makampuni makubwa ambayo yaliisha ingia Mikataba na Serikali.
Mgao wa Serikali ni ASILIMIA ngapi ili tuweze kuzungumzia kutokomeza Umasikini?
Huyu msafisha kabuli wa chato pale achana nae tutakwimu zako sio sahihi ndugu, kwenye swala la gas tanzania tuna lita nyingi sana za ujazo, yaan kitakwimu tunaweza tukawa juu sana kidunia
Basi kwa kutulia! Mada nzito sana hii kwakoHapana sifahamu
Tupe ushahidi wa Hiyo miswada kusainiwaTutacheza vipi vizuri wakati mikataba ishasainiwa?
Usiongelee yaliyopita tuongelee sasa kwenda mbeleuzi wako ni mzuri sana na wenye kutia matumaini hasa kwa sisi watanzania tuliokwisha poteza matumaini
Ila tambua ya kuwa hii sio fursa ya kipekee kwa nchi yetu
tumekuwa na fursa nyingi sana tangu enzi za mwalimu lakini chakuskitisha tumeshindwa kutumia hata moja
lord; nina imani wewe ni mtanzania kama nilivyo mimi na watanzania wengine, nina iman unaijua hii nchi vizur utajiri tulionao
swali la kujiuliza tumenufaika vipi na raslimari tulizo nazo?
madini, bahari, bandari, mawziwa, mito mikubwa, mbuga za wanyama, kilimo, mifugo nk! raslimar zote hizo kwa ujumla zinafanana na iyo gas ukizijumlisha?
lakin cha ajabu mpaka leo hii bado tunalia umaskini