Mradi wa mabasi yaendayo kasi (BRT) na Dar es Salaam Rapid Transit (DART)

Ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo haraka - Kimara Mwisho​

Ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo haraka - Kimara Mwisho - wavuti.com

3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da3386758137ac5f112d232c74f5aefdc2c544f18444.jpg

3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da3386750107bcaf013d032c74f5aefdc2c544f18444.jpg

3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da338675f1571cff313d032c74f5aefdc2c544f18444.jpg

3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da338675c107acbf318d332c74f5aefdc2c544f18444.jpg

3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da338675c1378cff619d532c74f5aefdc2c544f18444.jpg
3880ba48b4db12c8e3dca20f61bae367338a5874bf9ff97f226350fb97218501d1da487364b4a6d92da338675b117dc9f811db32c74f5aefdc2c544f18444.jpg
 
Huu mradi kufanikiwa au kutofanikiwa kwake kutategemea na kuweza kujenga uwezo wa kujitegemea in the future. Kama utakuwa mradi wa kusubiri ruzuku ya serikali kila mwezi ndio walipe mishahara ya madereva wanunue mafuta basi hamna kitu hapo mradi utaishia kapuni.
 
Safi sana NDINDA. Vipi lakini mradi utakamilika kwa wakati wake kwa kasi wanauokwenda nayo?

mkuu kutokana na maoni ya watu walio karibu na wanavyoona vifaa na watu wanavyopiga kazi, kuna matumaini kazi inaenda kama ilivyopangwa ila sijui hao tanesco na wengine ambao wanatkaiza kusogeza vitu kama nguzo na mabomba ya maji, mengine sina uhakika mkuu mi huwa naweka tu updates nikiziona:smiling:
 
Kweli mkuu hata mie naona jamaa wanapiga kazi kwelikweli....usisite kutu-update kwa picha mkuu!
 
Haya ni Majibu ya Rais waliyemuita DHAIFU. Ukweli ni kuwa, JK Amefanya makubwa kuliko Awamu zote kwani ametumia fursa ambazo waliotangulia hawakuzipata. Kila kiongozi ana nyota na enzi yake. Nataja baadhi ya mambo ambayo yanaitwa ndoto. Daraja la Maragalasi 80bil, limekamilika kwa zaidi ya 70%, Daraja la Kigamboni 200bil, limeanza kujengwa, Bomba la gesi Mtwara dar for 2700MGW pamoja na kuingiza gesi majumbani mradi umeanza, Mradi wa liganga na mchuchuma ukikamilika 11trillion, umeanza, bara bara za lami 11,000 km nchi nzima awamu tofauti ujenzi unaendelea, Usafiri wa treni dar, october 1, ujenzi reli mpya Tanga, Musoma mkataba umesainiwa, Udom na maendeleo ya vyuo vikuu, Sekondari za kata zimeanza kufaulisha, na kuna listi kubwa ambayo inahusu kilimo, biashara nk. MNYONGE MYONGENI HAKI YAKE MPANI

Usisahau kuwa JK amekuta Tanzania tayari na reserves za kutosha. pamoja na mapungufu yake Mkapa alifanya mambo mengi makubwa hasa kwenye kuubadilisha uchumi wa Tanzania. JK alikuta Tanzania ikiwa na zaidi ya dollar billion tatu kwenye forex. Mkapa hakukuta kitu. Mwinyi ndiyo kabisa alikuwa hata dollar laki tano za kununulia mafuta hazikuwepo.
 
Kuna haja ya kuwa na Ramani rough ambayo itaonyesha mipango kwa miaka angalau 50 ijayo, na kuweka alama mbalimbali ili watu wasiweze kufanya uwekezaji mkubwa. Pia ni vyema sehemu zote ambazo treni zaweza kuatana na barabara kuwe na madaraja pia kuwe na vituo vya kuswitch.
 
Ni kweli, lakini usisahau hali aliyoikuta Jk, Pamoja na huo uchumi kukuwa awamu ya awali. Umeme ulikuwa zero, viwanda vyote viliuzwa na vilikuwa haviingizi kitu, misamaha ya kodi, bara bara za lami km 6000 tu, wanafunzi vyuo vikuu wachache na graduands walikuwa chini ya 1%, Watendaji wengi walikuwa wasomi lakini wezi, mfano tanesco. Hakukuwa na uhuru wa kuongea nk. Wakati mwingine watu wanaotegemewa kabisa hutuangusha. Mengi katika uchumi mkubwa kafanya JK kilichobaki ni "Multiplier effect"
[MENTION][/MENTION]
Usisahau kuwa JK amekuta Tanzania tayari na reserves za kutosha. pamoja na mapungufu yake Mkapa alifanya mambo mengi makubwa hasa kwenye kuubadilisha uchumi wa Tanzania. JK alikuta Tanzania ikiwa na zaidi ya dollar billion tatu kwenye forex. Mkapa hakukuta kitu. Mwinyi ndiyo kabisa alikuwa hata dollar laki tano za kununulia mafuta hazikuwepo.
 
salamu hizi ziwaendee wakenya hasa wale wakazi wa nairobi mana wanajivunia sana kale ka-superhighway kao thika road:A S thumbs_up:
 
Ni kweli, lakini usisahau hali aliyoikuta Jk, Pamoja na huo uchumi kukuwa awamu ya awali. Umeme ulikuwa zero, viwanda vyote viliuzwa na vilikuwa haviingizi kitu, misamaha ya kodi, bara bara za lami km 6000 tu, wanafunzi vyuo vikuu wachache na graduands walikuwa chini ya 1%, Watendaji wengi walikuwa wasomi lakini wezi, mfano tanesco. Hakukuwa na uhuru wa kuongea nk. Wakati mwingine watu wanaotegemewa kabisa hutuangusha. Mengi katika uchumi mkubwa kafanya JK kilichobaki ni "Multiplier effect"

Kuuzwa viwanda ni haki kabisa. Viwanda hivyo vilianzishwa na serikali ya awamu ya kwanza na baadaye viligeuka kuwa ni vichaka vya wezi. Labda nikuulize ni viwanda vipi ambavyo Mkapa aliviuza na unaona kuwa visingeuzwa.

Ni rahisi sana kusahau hali aliyoikuta Tanzania wakati anachukua nchi. Nchi zote wahisani pamoja na Benki Kuu ya Dunia na IMF walisimimisha kabisa kuisaidia Tanzania. Walikuwa wanataka Tanzania ianze kulipa madeni kwanza ndiyo waanze kufikiria namna ya kurudi kuisaidia tena. Mkapa vile vile aliamua kuweka uchumi wa nchi sawa. Shilingi ilipotea na ikawa ina thamani tena mikononi mwa watu. Uchumi ulikuwa na ndipo kukawa na pesa ile ambayo JK aliikuta pale Benki Kuu.

Kuhusu kujenga mabarabara ukumbuke kuwa Mkapa alikuwa ndiye Rais wa kwanza Tanzania kuamua kuwa tunaweza kujenga mabarabara na miundo mbinu mingine kwa kutumia pesa zetu wenyewe bila kuomba misaada au kukopa kila wakati. Ilikuwa haijatokea. Ndipo mradi wa barabara ya kutoka Mwanza hadi Mtwara ulipobuniwa. Vilevile aliweza kutoa maji ziwa Victoria na kuyapeleka mpaka Shinyanga.

Mkapa asingeweza kufanya yote hasa ukizingatia hali aliyoikuta. Alipochukua nchi kulikuwa hata hakuna cha maana cha kuiba. Ufukara na umaskini ulikithiri.

Changamoto za Rais anayekuja ni nyingi. Kubwa kupita zote ni kuhakikisha kuwa anawafagia wezi wote waliopo kila kona ya serikali ya leo na kuhakikisha kuwa uchumi unakua zaidi.
 
Upo sahihi kwa upande mmoja. Kwa upande mwingine JK Kafanya mambo mengi makubwa kuliko wengine wote kwa maana ya uchumi. Nitakupatia orodha na thamani ya miradi. Mmoja wa mfano ni Mradi wa Chuma na MAKAA YA MAWE LUDEWA. Zaidi ya 5Trillioni mwanzo wa mradi na hisa kwa mara ya kwanza tanzania itamiliki 49%. Hakuna Rais Tanzania Amewahi kupata hisa katika mgodi mkubwa ukitoa Mwadui kwa JK Nyerere nadhani alikuwa na hisa kituchul

Tanzania ilikuwa ina hisa za 51% kwenye mgodi wa Mwadui na DeBeers wakachukua 49%. Tanzania iling'ang'ania kuendesha mgodi ule kutokana na wingi wa hisa. Meneja wa mwisho mzungu (Mr. Hunt ) aliondoka Mwadui mwanzoni mwa miaka ya 70 na akachkua Mr. Samwel Rwakatare, na badaye wengne walifuata. Kilicotokea ni kuwa mgodi ulizidi kudorora kiasi cha kwamba walikuwa wantupa mchanga na almasi kwani hawakuweza kununua mashine za kisasa. Mwishoni mgodi ulishndwa kabisa kujiendesha.

Mkapa aliomba De Beers warudi kuuendesha tenma ule mgodi. De Beers waliukuta mgodi ukiwa hoi kwelikweli na wakaiambia serikali na wao watoe pesa kuufufua. Serikali wakawa hawana pesa. De Beers walitoa pesa na hisa za serikali zikapungua thamani kufikia nadhani 25%.

Kuhusu Liganga na Mchuchuma nadhani hali ni karibu hiyo hiyo. Serikali itamiliki 49% ikiwa tu itatoa pesa kununua hisa zake. La sivyo kama serikali itashindwa kutoa hiyo pesa, na watashindwa, basi hisa zake zitapungua kwenda kwenye asilimia ya chini zaidi. Nadhani unaweza kupata taarifa zaidi kutoka NDC.

Mradi wa cuma na makaa ya mawe ni wa miaka mingi sana. Labda sasa kuna kitu kitatokea ijapokuwa bado nina wasiwasi kiasi fulani.
 
Asante kwa kunielimisha kuhusu mwadui. Msimamo wangu, Mhe. Mkapa alikuwa mzuri sana awamu yake ya kwanza. Awamu ya pili, kuna wanaoamini kuwa alilogwa, kwani katika kuuza viwanda, mambo mengi hayakusimamiwe vizuri na huenda yeye alikuwa na nia njema. JK Ana nia njema pia, na kuna mambo kama Mkapa, hatakwepa kwa kuwa tu yeye ni msimamizi mkuu wa serikali. Hisa za Mradi wa Liganga na Mchuchuma zitapatikana kwa mkopo na bahati nzuri, malighafi haitasafirishwa na viwanda vitajengwa nchini. Mradi pia utarudisha fedha mapema ndani ya miaka 10, hivyo kufanya deni la hisa kulipwa na nchi kuanza kunufaika japo kwa muda kidogo. Ukiachilia mbali miradi ya barabara ya JK 11,000Km, Bomba la gesi Mtware dar, Mradi wa Gas visima vipya, Mafuta kampuni ya Brazili, Kufufua TPDC na TIPPER, Kilimo kwanza (nimepita wilaya zote), huezi amini kuna mambo makubwa yanaendelea katika kilimo, Miundo mbinu imesababisha bei ya mahindi kwa mara ya kwanza hadi songea na sumbawanga kuwa shs 500 @kg, Kilimo cha matunda na soko pia, Juisi zinapatikana hadi vijijini [made in Tanzania well done and packed], Though changamoto kuna mazuri ya Mkapa JK Hajayapatia naafasi kama vile Mkurabita, Uwajibikaji kazini, nidhamu ya kazi nk. Nakushukuru kuna niliyojifunza kwako
Tanzania ilikuwa ina hisa za 51% kwenye mgodi wa Mwadui na DeBeers wakachukua 49%. Tanzania iling'ang'ania kuendesha mgodi ule kutokana na wingi wa hisa. Meneja wa mwisho mzungu (Mr. Hunt ) aliondoka Mwadui mwanzoni mwa miaka ya 70 na akachkua Mr. Samwel Rwakatare, na badaye wengne walifuata. Kilicotokea ni kuwa mgodi ulizidi kudorora kiasi cha kwamba walikuwa wantupa mchanga na almasi kwani hawakuweza kununua mashine za kisasa. Mwishoni mgodi ulishndwa kabisa kujiendesha.

Mkapa aliomba De Beers warudi kuuendesha tenma ule mgodi. De Beers waliukuta mgodi ukiwa hoi kwelikweli na wakaiambia serikali na wao watoe pesa kuufufua. Serikali wakawa hawana pesa. De Beers walitoa pesa na hisa za serikali zikapungua thamani kufikia nadhani 25%.

Kuhusu Liganga na Mchuchuma nadhani hali ni karibu hiyo hiyo. Serikali itamiliki 49% ikiwa tu itatoa pesa kununua hisa zake. La sivyo kama serikali itashindwa kutoa hiyo pesa, na watashindwa, basi hisa zake zitapungua kwenda kwenye asilimia ya chini zaidi. Nadhani unaweza kupata taarifa zaidi kutoka NDC.

Mradi wa cuma na makaa ya mawe ni wa miaka mingi sana. Labda sasa kuna kitu kitatokea ijapokuwa bado nina wasiwasi kiasi fulani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom