Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Usidhani kila wakati unatakiwa kufikiria kibiashara la hasha serikali inachochea sekta binafsi ziweze kufanya biashara kwa faida siyo serikali.Reli inatengenezwa ili ichochee sekta za kibiashara.Acha uvivu wa kufikiri
 
Uchumi wa China ulianza kukua kwa kasi miaka ya 1980 baada ya kufunguliwa na kuruhusu sekta binafsi kushamiri chini ya Deng Xiaoping, hii China yenye uchumi mkubwa unayoina leo ni matokeo ya Sekta binafsi kuruhusiwa kuchukua hatamu japo kwa kuendelea kubanwa na sera za kikomunisti. Kwa sasa viwanda na makampuni mengi China yanamilikiwa na watu binafsi au umma kupitia mfumo wa hisa.

Russia ilishatoka kwa kiasi kikubwa kwenye mfumo wa serikali kufanya biashara,ilifanya ubinafsihaji mkubwa wa makampuni ya umma miaka ya 1990 chini ya Boris Yeltsin na imeenda mbali sana kwenye sekta binafsi.

Fahamu pia kuna nchi nyingi zina utajiri mkubwa kiasi kwamba kuna mambo ya kibiashara zinafanya bila dhana ya biashara, Hizo ni pamoja na Russia, Saudi Arabia, Qatar n.k.Hizi ni nchi ambazo zitajenga na kuendesha miradi ya reli, mwendokasi, mashirika ya ndege bila kujali upatikanaji wa faida yoyote, zina huo uwezo, sisi hatuna.

North Korea ni shit hole country haifai hata kuzungumziwa.
 
Serikali inapaswa kujenga reli kisha waiachie sekta binafsi kuendesha treni kama inavyojenga barabara kisha inaachia kampuni za mabasi kusafirisha watu na mizigo.
Usidhani kila wakati unatakiwa kufikiria kibiashara la hasha serikali inachochea sekta binafsi ziweze kufanya biashara kwa faida siyo serikali.Reli inatengenezwa ili ichochee sekta za kibiashara.Acha uvivu wa kufikiri
 
Ccm imetawala hii nchi miaka 60 80% ya watu ni masikini wa kutupwa, hata uwape miaka milioni hakuna kitu watafanya.

kwan wanaofanya wananchi kua maskini ni serikali? socialism mlikataa mkamuona nyerere anaharibu uchumi wakati ilikua ni kwa ajili ya usawa! basi tumeingia capitalism sasa kelele za nn tena ama hujui maaana ya SURVIVAL FOR THE FITTEST? ni wap duniani hakuna maskini?
 
Naona uwezo wako wa kutambua mambo ni wa chini, inatosha.

unachoongea ni upuuzi ndo maaana! biashara ya reli ipo duniani kote mdogo wangu, isitoshe nchi zilizoendelea znategemea reli zaidi lakini malori bado yapo, so unaongea ujinga!
 
Hizi ndizo mojawapo sababu biashara za serikali huwa zinashindwa vibaya sana @Kalamu1

bila serikali hata hilo bundle unalotumia kuongea ujinga usingekua nalo, ni uwekezaji kama huu unaofanya maumivu ya uchumi kupungua kwa wananchi mfano kikwete aliwekeza kujenga mkongo wa taifa unaomilikiwa na serikali hivo kupunguza maumivu ya uchumi, same applies kwenye mambo mengine! kwahio acha kuongea ujinga
 
Masikini wapo sehemu zote Duniani lakini serikali ambayo inatengeneza ama inazalisha 80% ya raia masikini ni serikali ya wapi hiyo, ya kishetani.

Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira watu watoke kwenye umasikini, hiyo survival for the fittest iwe fair, sasa hii serikali ya ccm imeshindwa kwa miaka 60 sasa. Bora apewe Rungwe.
 

naomba kujua elimu yako
 
Mkuu Yoda, nadhani hatuendi popote na mjadala huu endapo kama tutabaki kuzungukia kwenye hizo habari tunazozijuwa kila mara, kama zinavyoelezwa kwa maksudi maalum.
Mimi sijakataa mchango wa sekta binafsi. Ninachokataa ni hiyo dhana potofu ya kunag'ang'ania kwamba "serikali haiwezi".
Maendeleo ya China huwezi kuondoa ushiriki mkubwa wa serikali, eti kwamba yalipatikana tu pale sekta binafsi iliporuhusiwa.

Nimekupa hiyo mifano ya Korea na Soviet kujibu hoja yako ya mashirika binafsi katika utengenezaji na uendelezaji wa silaha, bado unatafuta visababu.
Unaweza kuiita Korea Kaskazini 'shithole', lakini kamwe huwezi kuondoa ukweli kwamba sasa hivi hakuna anayeweza kwenda kuichezea bila kutoka yeye kamasi, na hakuna sekta binafsi iliyowezesha hivyo iwe hivyo.
 
 

yaaani nlikua napita twitter nakutana na hii post nkakukumbuka we bongo lala
 
Yaani mpaka iwe bure kabisa ndo ujue ni huduma kwa jamii?
Mwendokasi ni biashara na si huduma na huduma si lazima iwe bure iwe hata kwa malipo ila yawe kidogo chini ya inayotozwa na sekta binafsi.....Sasa cha kushangaza nauli ya usafiri wa serikali ikawa juu zaidi ya usafiri wa wawekezaji binafsi halafu tuuite kuwa ni huduma!!!!
 
Badala ya kuongelea mchango wa sekta binafsi tunapaswa kufikia mahali kuongolea mchango sekta ya umma( lYani sekta binafsi ndio iwe injini halafu ipewe mchango na sekta ya umma). Tunakosea kusema mchango wa sekta binafsi wakati sekta binafsi ndio inapaswa kuwa 'main'.

Serikali inaweza kufanya biashara yoyote ikiamua, na ina uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu ina uwezo wa kupata pesa kupitia kodi na dola ya kulazimisha mambo, ila haiwezi kufanya biashara YOYOTE kwa ufanisi kama sekta binafsi, hii ni kanunu ya uchumi.
Zipo sababu milioni za kiuchumi kwa nini huwa inakuwa hivyo.

Korea Kaskazini kuwa na makombora ya nuclera na kutochezwa sio kwa sababu ya ufanisi wa sekta ya umma katika biashara. Hakuna biashara yoyote inayofanyika Kiduku anapoenda kuchukua wataalamu wavujisha siri za nuclear "nuclear proliferators" kutoka Iran na kwingineko wamjengee nuclear. Mkuu Kalamu1 Korea ya Kaskazini ni shithole country na " odius dictatorship", ni taifa la kijuha sana linaloendeshwa na psychopaths, huwezi kuwa unarusha makombora hewani kila siku huku watu wako wanakufa njaa na kutumia kinyesi cha binadamu kama mbolea.
Kutamani kuwa kama Korea ya Kaskazini ni wendawazimu au kuwa mtu wa akili ndogo sana.
 
yaaani nlikua napita twitter nakutana na hii post nkakukumbuka we bongo lala
Wewe na huyo taahira mwenzako hamuelewi role ya serikali katika kusaidia kuondoa umasikini.

Kama serikali haijatengeneza mazingira mazuri ya kukufanya wewe shughuli unayofanya ifanikiwe na utokane ama uondokane na umasikini hata ufanyeje haiwezekani.

Kwa nini watu walikua wanamlaumu JPM kwamba amefanya mazingira ya biashara kua magumu? Kwani biashara ilikua haifanyiki?

Ninachokiona ni wewe kua na uelewa mdogo wa haya mambo. Rudi shule uongeze maarifa kisha uje tujadiliane.
 
naomba kujua elimu yako
Elimu yangu hakuna mtu kwenye ukoo wenu anayo ama atakuja kua nayo.

Kama akili huna ya kujua wajibu wa serikali kwenye kupumguza ama kuondoa umasikini, unakopi tweets za waume zako huko Twitter ambao hawana akili kama weww unawezaje kuhoji elimu yangu mimi mtaalam?

Achana na mataahira wenzakowa tweeter, soma hapa kutoka kwa wataalamu wa uchumi kutoka IMF wanasemaje kuhusu serikali kupunguza umasikini


 

Tanzania bila kuwasulubisha wezi wa mali ya umma, miradi yote haitakaa kuja kujiendesha. Watu wasipojua kujituma ili biashara ijiendeshe kwa faida, hilo kosa la nani? Tungejitendea wema, kama tungeweza kujifunza kwanini Tazara, with all its potential, inasuasua hadi hii leo. Shida ni nini? Ili tusirudie makosa kwenye SGR
 
Mbona sioni faida ya TAZARA ambayo ilianza kabla sijazaliwa? Au hata hiyo TAZARA wajukuu wangu ndio wataona faida?
kujua sababu uwezo wa kuchambua mambo ni finyu.Acha mradi umalizie wajukuu zako wataona faida.Miaka 100 ijayo wataona faida yake siyo wewe
 
Hiyo 'para' ya pili ni 'dogma'tu mkuu Yoda iliyozoeleka na inayopendwa kusemwa kama msahafu fulani.

Kwenye 'para' ya kwanza, umenikumbusha jambo ambalo huwa ninalifikiria mara kwa mara: Kwani "Sekta Binafsi" ni kitu gani? Mkulima wa njegere kule Manyara hatuwezi tukamweka kwenye sekta binafsi? Kwa nini? Kama ni uwezo wake, je tukiwaunganisha na wakawa kundi kubwa na uwezo wao ukawa mkubwa, kundi hili hatuwezi tukalitambua kama sekta binafsi?

Nimetumia tu huo mfano wa mkulima, lakini tunaweza kutumia mifano mingi mingine ya aina hiyo.

Bado hatukubaliani kabisa kuhusu uwezo wa serikali kufanya shughuli za kibiashara katika baadhi ya mashirika ikiweka nia ya kuufanikisha.

Kuhusu Korea Kaskazini, naona uamini wako ni ule ule wa kuchotwa akili na propaganda za upotoshaji wa vyombo vya habari na kuufanya wimbo unaoimbwa sehemu zote hadi na watu wenye akili timamu. China pia ilikuwa hivyo hivyo, hadi hapo walipoamua kuunganisha mtindo wao na ule waliokuwa wakiupigia chapuao hao wanaoeneza propaganda duniani.

Korea Kaskazini, usisahau wapo chini ya vikwazo vya kiuchumi, na kila siku wakubwa wanasubiri kusikia nchi hiyo imeangamia! Lakini haijatokea. Waondoe vikwazo basi, ili tuone watakavyodhoofika haraka? Unamwekeaje vikwazo mtu unayejuwa mtindo wake wa siasa ndio utakaommaliza mwenyewe? Ninapoandika haya siyo kwamba nataka Tanzania iwe hivyo, la hasha, ni kuonyesha tu upotoshaji unaofanyika na kuchota akili za watu wengi bila ya kusita na kudadisi kwa kina.
 
Tungejitendea wema, kama tungeweza kujifunza kwanini Tazara, with all its potential, inasuasua hadi hii leo. Shida ni nini? Ili tusirudie makosa kwenye SGR
Mstari mmoja wenye maana nzito kabisa. Badala yake watu wanatafuta majibu kwingine kabisa.
 
Tusipoteze muda na kamati za kutafuta kwa nini mambo ya kijamaa yalishindwa na yanaendelea kushindwa duniani kote. SGR ikikamilika huo mwaka itakaokamilia sekta binafsi ipewe fursa ya kuendesha biashara ya treni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…