Mradi wa usambazaji maji uliojengwa na China wanufaisha maisha katika mji mkuu wa Angola

Mradi wa usambazaji maji uliojengwa na China wanufaisha maisha katika mji mkuu wa Angola

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VNan2jlvpci1OQQ1.png


Katika eneo la ujenzi wa Mradi wa Usambazaji Maji wa Quilonga unaotekelezwa na Shirika la Ujenzi wa Nishati la China (PowerChina) mashariki mwa Luanda, mji mkuu wa Angola, wafanyakazi wanashughulika na kazi zao kwa utaratibu mzuri.

Figueira Kalunga, fundi wa usimamizi wa usalama, anazunguka eneo hilo, akikagua kwa uangalifu kofia za wafanyakazi, nyenzo na vifaa vingine vya kujilinda.

Kalunga ameshiriki kwenye miradi kadhaa ya PowerChina tangu mwaka 2017, akianza kama fundi wa kukarabati chuma. "Ninajivunia kuwa sehemu ya mradi huu ambao unanufaisha maisha ya watu. Sio tu kwamba unatoa nafasi za ajira kwa Waangola wengi, bali pia utanufaisha idadi kubwa ya wakazi mara tu utakapokamilika," alisema.

Luanda imekumbwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu kutokana na ukame, vifaa chakavu, na uwezo duni wa kutibu maji na usambazaji.

Antonio Fernandes Rodrigues Belsa da Costa, katibu mwenye jukumu la kusimamia maji katika Wizara ya Nishati na Maji ya Angola, alisema katika eneo la mradi kwamba mji mkuu bado unakabiliwa na pengo la upatikanaji wa maji la hadi asilimia 50, huku baadhi ya maeneo yakipata maji mara moja tu kila baada ya siku mbili au tatu.

Kwa mujibu wa meneja wa mradi huo Zhang Qiang, Mradi wa Usambazaji Maji wa Quilonga una kituo cha kusukuma maji chenye uwezo wa kusukuma maji kila siku kwa mita za ujazo 570,000, bomba la maji lenye urefu wa kilomita 12.5, mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa kila siku wa mita za ujazo 500,000, na vituo vitano vya usambazaji.

Ujenzi unaendelea kama ulivyopangwa, na mara tu mradi utakapokamilika, utapunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa maji uliopo mashariki mwa Luanda, alisema Zhang.

Zhang Peng, mhandisi mkuu, alisema kituo cha kusukuma maji kilichopo kwenye kingo za Mto Kwanza, kinakabiliwa na changamoto za ujenzi kutokana na ardhi ya kinamasi na misingi ya kina kirefu.

"Kupitia ufumbuzi bunifu wa uhandisi, tumeweka msingi imara wa muundo mkuu," alisema.

Zaidi ya ujenzi, timu ya mradi imefanya kazi ili kupunguza tofauti za kanuni na viwango vya kiufundi kati ya China na Angola. Pia wamekuza mawasiliano ya kitamaduni kwa kuandaa shughuli mbalimbali, kutoa mafunzo ya lugha, na kuajiri wahandisi wazawa wenye uzoefu wa masomo nchini China, jambo ambalo limesaidia kukuza maelewano na ushirikiano kati ya wafanyakazi.



Helmano Adriano, msimamizi wa manispaa ya Bom Jesus, ambako mradi huo unapatikana, alisifu juhudi za kujitolea za Shirika la PowerChina kwa jumii za wenyeji kupitia miradi ya ustawi wa umma, kama vile kujenga mifumo ya maji ya kunywa, kuweka gridi za umeme, na kusaidia mipango ya jamii, ambayo inanufaisha moja kwa moja maelfu ya wakazi.

"Mradi wa Usambazaji Maji wa Quilonga utaboresha kwa kiasi kikubwa usambazaji maji katika mji mkuu na kimsingi kuziba pengo. Tuna imani kwamba utakapokamilika mwaka 2026, utapunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa maji wa Luanda," alisema Belsa da Costa.
 
Back
Top Bottom