Mrejesho baada ya kufika Dar usiku na kuomba mwenyeji anipokee kwa dharura

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,586
Reaction score
8,389
Jana nilikuwa safarini kuja Dar na bahati mbaya mwenyeji wangu niliyekusudia kunipokea simu yake haikupatikana

Kwa kuwa mimi siyo mwenyeji saaana,kupitia hapa jf niliomba kupata msaada wa mtu kujitokeza anipokee maana ningefika usiku sana

Hata hivyo nashukuru sana kwa wenyeji kujitokeza kwenye pm yangu ili wanipokee,jumla ya watu 87 walijitokeza kunipokea bahati mbaya hakuna mwanamke aliyejitokeza kunipokea, nashukuru sana hao 87
Niliwapa watu 11 namba yangu ya simu,watu 7 walinipigia ila wanne walinitext

Nilipofika stendi watu watatu walihakikishia kuwa wapo stendi ya Magufuli ila wawili walikuwa na magari,mmoja yeye alikuwa kwa mguu akiniahidi kwenda kwa daladala Mbagala

Niliposhuka niliondoka na jamaa mmoja aliyejitambulisha Kama M sitamtaja majina yake kwa faragha
Kwenye gari yake walikuwa wanaume watano,mpaka nikaogopa ila wakanihakikishia kuna usalama,nikaingia kwenye gari

Nikakaa siti ya mbele na M tukaanza kuondoka,huku nilimuuliza M Kama hawa jamaa wengine ni member JF akasema hapana

Safari ikaenda Kama saa 3,tukaingia kwenye majengo fulani kwa bahati nikawa nimeona sehemu pameandika Nkuruma hosteli,nikamuuliza M mbona huku ni hosteli,akajibu nataka nishushe hawa wenzangu hapa tuendelee na safari...........

Basi wenzake wakashuka na yeye akashuka huku akiniambia "Nisubiri kidogo" Nikamjibu uwahi nimechoka" Akaondoka akifuata wenzake na wakaingia ndani

Huko ndani alikaa muda mrefu Kama dakika 20 hivi nikamtumia sms "Jamani kulikoni mbona hauji? Nikiona muda ni saa sita kasoro nimechoka na njaa

Baadae Mr M akarejea akaniomba nishuke,nikashuka akanishika mkono wa kushoto akanambia twende cantini pale tupate chakula,tukaondoka tukawa tunapita kwenye korido nikamuuliza hapa ni kama vile chuo,akajibu"Cute ni kweli hapa ni chuo" Nikauliza tena kwani wewe ni mwanachuo?Akajibu kwa upole "Hapana,mi ni mkufunzi" Nikasema"Sawa" Tulipofika,walikuwa wamefunga, nikamwambia" Usijali nitakula kesho mi nioneshe sehemu nipumzike" Akajibu "Basi twende hapa kwangu,nyuma ya hili jengo"Kwani wewe unakaa hapa hapa chuoni akasema "Ndiyo"
Basi tukaenda tulipofika karibu na hilo jengo "Akagonga mlango kijana mdogo hivi akafungua mlango tukaingia ndani,akaniletea soda na mkate nikala kisha akanionesha chumba cha kulala nikaingia kulala huku akiniambia"Cute uwe na amani ,mimi ni mtu salama" Usiku mwema na mimi nikajibu na wewe pia,nikafunga mlango nikaingia kulala
Asubuhi saa 2 hivi alikuja akanigongea mlango tukasalimiana kisha akanipa sabuni nikaoge nijiandae tutoke

Nilipomaliza tulitoka na kwenda parking ya magari,tukapanda gari na kuingia mjini,akanipeleka hotel fulani hivi amazing na kupata chai,supu kuku ya nguvu,Kisha akanipeleka duka lake la vifaa vya umeme,ni duka kubwa,nikampa hongera Mr M kwa duka kubwa sana maeneo ya Sinza

Baadae nikamuomba anipeleke kwa ndugu yangu niliyekuwa nimekusudia kufikia, akanipeleka,wakati tupo njiani akaanza kuniuliza baadhi ya mambo "Cute unajishugulisha na nini,nikamjibu,mimi ni mtumishi wa serikali,afisa mtendaji,nilianzia kazi Moro Kisha Dodoma sasa nipo Bk nimeona niwe karibu na kwetu ila nitatulia nikihamia Mwanza nilikokulia"Akasema kumbe wewe ni mtu mzito wa serikali? Nikamjibu kawaida tu best,akaniuliza "Vipi Kama umeolewa hivi" Nikajibu hapana ila nikiwa naanza kazi Moro nilipatana na kijana mmoja lakini baadae nikaona ana mambo mengi nikaachana tangu hapo nikaachana na mambo ya mahusiano*
Mr M akaendelea na maongezi"Sasa Cute,mimi Nina mchumba ambaye tulikuwa tumekubaliana kuwa tufunge pingu za maisha ila tumekorofishana sana na kufikia kiwango cha kutaka kuvunja mahusiano,binti yule ni mtoto wa tajiri mmoja kule Zanzibar,ananitesa sana"Nikamjibu " Pole ila ongea naye taratibu mambo yenu yatakuwa sawa"

Asante Mr M kwa ukarimu wako,hakika unenionesha upendo wa dhati,nimeondoka Dar narudi zangu kazini nisije nikaondolewa kwenye payroll na huku mwezi wa July mambo ni moto
Mr M Mungu akubariki,hukunitamkia maneno ya kutaka ngono,Kama wanaume wengine,ubarikiwe sana,mwaaaaa nyingi , nakupenda
 
Alright — you asked for it 😈

You're out here juggling cryptocurrency law, environmental impact reports, and English grammar like you're the legal Avenger of Tanzania… but somehow still Googling "How to add Tigopesa to Google Play Store" like it's a Supreme Court case.

You want a Ghibli-style picture of Batistuta in a Santos jersey but can’t decide if your research chapter needs a conceptual framework or just a miracle. One moment you're crafting legal theory, next you're training Osimhen to a 99 rating — bro, are you building a football team and a thesis at the same time?

You're a walking contradiction: part legal scholar, part anime fan, part gamer — with enough curiosity to finish a PhD and still have time to ask, “Can a country get charged for banning Twitter?”

But hey… underneath all that chaos is someone determined, creative, and clearly built different.
So — when’s the Netflix doc dropping: “Law, Goals & Ghibli
 
Eeenheee hadithi njoo utamu kolea.

Hadi unaandika hapa M sio mtu mbaya
Jana nilikuwa safarini kuja Dar na bahati mbaya mwenyeji wangu niliyekusudia kunipokea simu yake haikupatikana

Kwa kuwa mimi siyo mwenyeji saaana,kupitia hapa jf niliomba kupata msaada wa mtu kujitokeza anipokee maana ningefika usiku sana

Hata hivyo nashukuru sana kwa wenyeji kujitokeza kwenye pm yangu ili wanipokee,jumla ya watu 87 walijitokeza kunipokea bahati mbaya hakuna mwanamke aliyejitokeza kunipokea, nashukuru sana hao 87
Niliwapa watu 11 namba yangu ya simu,watu 7 walinipigia ila wanne walinitext

Nilipofika stendi watu watatu walihakikishia kuwa wapo stendi ya Magufuli ila wawili walikuwa na magari,mmoja yeye alikuwa kwa mguu akiniahidi kwenda kwa daladala Mbagala

Niliposhuka niliondoka na jamaa mmoja aliyejitambulisha Kama M sitamtaja majina yake kwa faragha
Kwenye gari yake walikuwa wanaume watano,mpaka nikaogopa ila wakanihakikishia kuna usalama,nikaingia kwenye gari

Nikakaa siti ya mbele na M tukaanza kuondoka,huku nilimuuliza M Kama hawa jamaa wengine ni member JF akasema hapana

Safari ikaenda Kama saa 3,tukaingia kwenye majengo fulani kwa bahati nikawa nimeona sehemu pameandika Nkuruma hosteli,nikamuuliza M mbona huku ni hosteli,akajibu nataka nishushe hawa wenzangu hapa tuendelee na safari...........
Itaendelea
 
Kipochi manyoya kikapaapswa..?
No reforms no election
 
Hahaha
Screenshot_20250604-120208~2.jpg
 
Back
Top Bottom