Mrejesho baada ya kufika Dar usiku na kuomba mwenyeji anipokee kwa dharura

Mrejesho baada ya kufika Dar usiku na kuomba mwenyeji anipokee kwa dharura

Nacheka kama mazuri eti wa 88πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£ ila JF
Wahuni sio watu aisee anaweza akawa kakosea kuhesabu idadi inaweza ikawa kubwa zaidi subiri mrejesho mwingine hawa wadogo wa kataa ndoa wanataka kuokota embe kwenye miti ya mikaratusi.
 
Jana nilikuwa safarini kuja Dar na bahati mbaya mwenyeji wangu niliyekusudia kunipokea simu yake haikupatikana

Kwa kuwa mimi siyo mwenyeji saaana,kupitia hapa jf niliomba kupata msaada wa mtu kujitokeza anipokee maana ningefika usiku sana

Hata hivyo nashukuru sana kwa wenyeji kujitokeza kwenye pm yangu ili wanipokee,jumla ya watu 87 walijitokeza kunipokea bahati mbaya hakuna mwanamke aliyejitokeza kunipokea, nashukuru sana hao 87
Niliwapa watu 11 namba yangu ya simu,watu 7 walinipigia ila wanne walinitext

Nilipofika stendi watu watatu walihakikishia kuwa wapo stendi ya Magufuli ila wawili walikuwa na magari,mmoja yeye alikuwa kwa mguu akiniahidi kwenda kwa daladala Mbagala

Niliposhuka niliondoka na jamaa mmoja aliyejitambulisha Kama M sitamtaja majina yake kwa faragha
Kwenye gari yake walikuwa wanaume watano,mpaka nikaogopa ila wakanihakikishia kuna usalama,nikaingia kwenye gari

Nikakaa siti ya mbele na M tukaanza kuondoka,huku nilimuuliza M Kama hawa jamaa wengine ni member JF akasema hapana

Safari ikaenda Kama saa 3,tukaingia kwenye majengo fulani kwa bahati nikawa nimeona sehemu pameandika Nkuruma hosteli,nikamuuliza M mbona huku ni hosteli,akajibu nataka nishushe hawa wenzangu hapa tuendelee na safari...........
Itaendelea

"Hata hivyo nashukuru sana kwa wenyeji kujitokeza kwenye pm yangu ili wanipokee,jumla ya watu 87 walijitokeza kunipokea bahati mbaya hakuna mwanamke aliyejitokeza kunipokea, nashukuru sana hao 87
Niliwapa watu 11 namba yangu ya simu,watu 7 walinipigia ila wanne walinitext."
 
Back
Top Bottom