Wapambanaji wenzangu najiaandaa kuleta mrejesho wa biashara ya madini ya dhahabu msimu wa pili ( Gold business feedback second season). Hii ni baada ya Mimi kujitosa kwenye biashara hii, June twenty twenty nilikuja jukwaani kutaka kufahamu abc za hiyo biashara kutoka kwa experts. Miezi sita baadae yaaani December nilileta mrejesho wa wapi nimefikia. Wapo waliodhani ni promota niliyetumwa kuja kuibia watu. Sasa nikikaribia kukamilisha mwaka juni hii ya twenty twenty one nitaleta mrejesho wa ups and downs na wapi nilipo. Hii ni kutia hamasa miongoni mwa vijana kuona kila utakachodhamilia utakifikia panapo juhudi, nidhamu na kutokata tamaa.