Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Kuna gold detectors za aina nyingi huku ila nataka kujua ipi ni nzuri na je nikileta ntauza?

Zipo za Mjerumani nzuri sana zingine mpaka 15m
 
Aisee
 
UK
Dili lipo mkuu au unazijua nzuri
Aaah sawa, ngoja basi nikitulia nitakueleza kwa ufahamu trend ya utafutaji wa dhahabu ili pamoja na wadau wengine tufanye tathmini ya pamoja kama biashara ya vipimo kwa sasa itafaa au haitafaa.
 
Kuna gold detectors za aina nyingi huku ila nataka kujua ipi ni nzuri na je nikileta ntauza?

Zipo za Mjerumani nzuri sana zingine mpaka 15m

Nitakujibu kwa majibu marefu kidogo, kuwa mvumilivu, tiririka nami.

Majibu haya ni kwa mujibu wa my personal experience (nimezaliwa na kukulia katika moj ya maeneo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania)
Hivyo kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo katika hoja zangu kulingana na hali ilivyo katika maeneo yenye madini nchini.

Tutazame kwanza mabadiliko ya trends za teknolojia za kupata dhahabu na nyakati zake.

1. Kuokota dhahabu maeneo mbalimbali (kwenye surface land) hasa ya maeneo ya mitoni, n.k :

Hizi ni zama za zamani sana, hasa kabla ya uhuru na kabla ya kuja watu weupe barani Afrika. Kama umeshawahi kusikia kwamba zamani dhahabu zilikua zinatumika kama "kete" za kuchezea bao. It was that simple, that abundant.

2. Kuchimba ili kupata "mchanga wa dhahabu" na kuosha ili kuipata dhahabu yenyewe (kusekesa/kuchekecha, kupiga kalai):

Hapa kilichokua kinatafutwa ni "mchanga wa dhahabu", na hatimaye unaoshwa kwa njia nilizotaja hapo juu ili kupata madini ya dhahabu. Ni njia ambayo inahitaji maji na kinachopatikana hapa tunaweza kusema ni "pure gold".

3. Kuchimba mashimo marefu (long bases) ili kutafuta MIAMBA inayoambatana na dhahabu:

Katika njia hii miamba hiyo hulainishwa (kuwa mawe madogo madogo), kutwangwa (kupata unga unga) na hatimaye "kukamatishwa" kwa kutumia Mercury ili kupata dhahabu. Mercury inafanya selective extraction ya gold kutoka kwenye unga (Ore) inayojumuisha metali nyingine.
Baada ya kazi ya Mercury, yale mabaki ("baada ya dhahabu" kuwa extracted) yalikua ama yakitupwa, au kutunzwa kwa ajili ya kurudia zoezi la extraction ya Mercury wakati ujao yatakapokua mengi zaidi. Logic hapa ni kwamba Mercury haifanyi extraction ya 100%. Katika point namba 5 tutaanzia hapa kwenye haya MABAKI au MARUDIO au MASAINENTI.

4. Kutumia "vipimio" (Gold detectors) kupata dhahabu:

Hii hasa ni kwa ajili ya kupata dhahabu zilizo kwenye surface (hazikuonekana kwa macho na kuokotwa hapo zamani), zile za kwenye "mchanga wa dhahabu" na kwa uchache kwenye "miamba yenye dhahabu".
Kwa huku kwetu, teknolojia hii imeanza kuchipukia mwaka 2000, imekuja ku peak miaka ya 2005-2010. Kuanzia miaka ya 2010 kuja juu vipimio vilianza kupungua kutokana na uhaba wa "aina ya dhahabu" ambazo vinagundua. Hivyo wenye vipimio walianza kwenda maeneo ya mbali (kutoka huku niliko) ili kutafuta dhahabu zinazoweza kutambuliwa na hivi vipimio. Mfano Mpanda, Maeneo ya nchi ya Msumbiji, Zambia n.k
Ila kwa ujumla ni kwamba kwa sasa kumiliki kipimio imekua kama ni old fashioned way ya kutafuta dhahabu, siku za kulala njaa zinakua ni nyingi sana. Kwa maneno mengine hapa nakuambia kwamba kuwa makini sana kama kweli utaamua kuleta hivyo vifaa. Hali yake ndivyo ilivyo.
Mifano ya "aina" za vipimio (gold detectors) iliyokua maarufu ni kama vile GP, SD, XT, GMT, Fisher, n.k

5. Ujio wa "Leaching plants" pamoja na "Elution" ili KUOZESHA "marudio" (Rejea point namba 3 hapo juu) na hatimaye kupata kupata dhahabu:

Yale mabaki au marudio baada ya shughuli ya Mercury, hapa yanaozeshwa kwa kutumia kemikali kadhaa kwenye mtambo wa uchenjuaji dhahabu na hatimaye kuchomwa ili kuipata dhahabu yenyewe.
Kutokana na hili, the more marudio unazalisha, the more likely kwamba utachenjua mara nyingi na hivyo utapata dhahabu kwa wingi zaidi.
Maana yake sasa, utahitaji maeneo mengi yenye miamba ya dhahabu, utahitaji mitambo mingi ya kusaga mawe (yanaitwa makarasha, yaani crushers) kutengeneza "marudio" mengi zaidi.
Kwa sasa teknolojia hii ya kumiliki "makarasha" ndio ina peak sana kwa "huku kwetu".

6. CIP & CIL Major plants:

Hii ni advanced level ya njia namba 5 hapo juu, inakua na ufanisi mkubwa zaidi katika kuozesha, inachukua large volumes ya marudio at a time na pia ina extract more gold.

Hata hivyo inahitaji mtaji mkubwa na miundombinu thabiti (hasa umeme) ili kuiendesha. Kwahiyo hizi bado ni chache sana.

Unaweza ukaona kuwa katika scenario zote 6 hapo juu (of course kuna zaidi) utaona dhahabu ni ileile, ila kinachobadilika ni TEKNOLOJIA inayotumika kuipata.

Hivyo nakusihi ufanye maamuzi juu ya biashara hiyo kulingana na uhalisia wa mambo yalivyo.

NB: Hii inahusu zaidi wachimbaji wadogo na angalau kidogo wachimbaji wa kati.

Andiko langu si msimamo wa sekta ya madini ya nchi nzima, ila angalau kwa 80% liamini na uliafuate.

Ukitaka nieleze fursa "za kibiashara" zilizopo katika sekta ya madini na mnyororo wake wa thamani, nitafanya mambo mawili yafuatayo:-

A. Nitakuomba unipe muda
B. Nitakueleza kinagaubaga.

Uwe na siku njema.
 

Nashukuru sana Mkuu kwa kutiririka na kupata mda wa kunielewesha
Nimerudia rudia kusoma na ni madini haswa umemwaga hapa kama dhahabu yenyewe

Nilikuwa nina haja sana ya kujua undani wa hii biashara na sasa nimepata mwanga mzuri

Asante sana
 
Hakika wewe umetema pointi za maana na zinazoonyesha uhalisia wa biashara tofauti na wengi wetu hupenda kusikia stori za vijiweni, maake kama faida ingekuwa kubwa sana tunavyoaminishwa basi wengi wangefanya.
 
Mkuu mimi nanunua dhahabu. Mara nyingi inakuja dhahabu IL yopembuliwa, ila Kuna wakati yanakuja mawe nayadhamini mwenye nayo anasaga kisha ananiuzia dhahabu. Hivyo kuwa na karasha imepanua wigo mwingine wa miradi yangu maana mwezi October nitatoa mlima. Nilikuwa nasagia kwa jamaa kabla sijachonga, jamaa juzi kachenjua mlima kapata kilo na gm miambili. Hivyo marudio yanalipa vizuri ila uwe na mtaji na usimamie kwa karibu zaidi.
 
Mkuu IBRA wa PILI usimbishie Narubongo kuwa faida ya dhahabu ni 2000 hadi 3000 kwa gram. Mkuu iko ivii, inategemea na maeneo. Kwa sababu ya ushindani wa kibiashara unakuta sehemu watu wanainunua dhahabu kwa bei ya juu kuzidi hata bei elekezi ya serikali. Hivyo huambulia faida kiduchu au kupata hasara. Yapo maeneo wanunuzi wa dhahabu wanapata faida maradufu sababu wanaelewana na wananunua dhahabu kwa bei elekezi. Mfano Mimi juzi nilikuwa sokoni nikiwa na 93g nilipoyeyusha ikatoka 91g. Polini nimetumia mil. 7.5, narudi na mil 9.2. Hapo hata Kama nimekaa wiki mbili bado inalipa mnoo.
 
Pambana mkuu, in'shallah utafika
 
Pori unalochukulia lipo wapi? Na soko lipo wapi?
 


Mkuu asante kwa maelezo ya uhakika. Najua kuhusu leaching plants pamoja na elution plants ila sijawahi kusikia kuhusu hizo CIP & CIL Major plants. Naomba utolee maelezo zaidi hizo kama hutojali. Fursa na changamoto zake, mtaji wa kuanzia nk.

Aidha kati ya kuwekeza kwenye plants na kwenye uuzaji wa machinery na madawa ya uchenjuanji ni wapi kuna fursa zaidi na lesser risky?
 
Wakuu mcrounmj na gspain naamini mtanipa mwanga zaidi maana mpo Chunya mahala ambapo nataka nifanye uwekezaji.

Kwa uzoefu wenu hasa Makongolosi kati ya 'Leaching plant and elution plant' na uuzaji wa mining machinery na madawa ya uchenjuaji wapi kuna fursa zaidi na lesser risky hasa Makongolosi?

Mkuu Mwanamaji kasema sasa kuna teknolojia ya CIP & CIL Major plants. Imefika Chunya hii? Kama ndiyo mnaonaje comparing to Elution plant katika maeneo ya hapo? Last time nipo hayo maeneo sikuisikia hii.

Najua kuna fursa ya maabara za madini as well, hiyo nayo vp?

Nahitaji kujua zaidi soko, changamoto, mtaji wa kuanzia nk. Any input is greatly appreciated.
 
Mkuu hizo CIP na CIL major plants ni "bigger versions" za hizi normal Leaching plants.

Kinachoongezeka ni ukubwa wa mzigo unachenjuliwa at a time na ufanisi wa zoezi la uchenjuaji.

Katika kuongeza ufanisi wa uchenjuaji, inajumuisha kuongeza jotoridi la kinachochenjuliwa. Sasa hii warming of Ore inakula umeme si mchezo.

Na kwa ujumla kwa sababu intake yake ni kubwa, basi inahitaji malighafi nyingi sana (mawe au mchanga) ili hii plant iendeshwe kwa tija.
Sitaki kwenda kwenye details za nini kinatokea na hata tukapata CIP (Carbon in pulp) na CIL (Carbon in leach) processes, ila kwa juu juu hizi ni namna mbili "activated Carbon" inawekwa ili kukamata dhahabu kutoka kwenye material inayoozeshwa.

Kwa Chunya nafahamu kuna jamaa anaitwa Aidan Msigwa (Mdimmi) anayo hii plant.

Makadirio ya uwekezaji wake, haiwezi kupungua 1B.
(Kama nakosea wadau watakuja ku correct).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…