Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Karibu sana kwenye biashara ya Uchimbaji.

Ukiwa na bahati huwezi kukosa millioni millioni, muhimu Kwa miezi ya awali uwe na funds za kukuwezesha ku-run biashara walau miezi 6 hadi 12 bila kutegemea fedha ya duarani.
Mkuu nina lengo nihamie kwenye biashara ya madini unanishauri niwekeze kwenye eneo lipi mtaji kwangu sio tatizo
 
Asante mkuu wa elimu nzuri ya kiuchumi hususani kwa vijana, hata mimi nina mpango huo wa kujenga nyumba ya kulala wageni nimekuja kugundua hiii ni biashara inayolipa kwa haraka kuliko nyumba za kupanga
vipi chief kuhusu vitanda umeweka vya ukubwa gani pia ulijenga jiko, chumba cha kufulia pamja na reception kubwa kwa ajili ya wateja kuweza kupumzika, kupata maji, chai pamoja na kupiga stori mbili tatu nje ya vyumbani?
 
Shukrani Mkuu 🙏

Kuhusu Ukubwa wa Vitanda, nimeweka vya 5*6 na magodo ya inchi 12

Sehemu ya Chai, Reception na Kufulia zipo bila kusahau parking.

Kwa tathmini niliyoifanya, nyumba za Kupangisha hazilipi kama zilivyo za Wageni.

Kama umetia nia ya kuwekeza huku, usisite pambana uje ukamilishe ndoto yako.

Gharama za ardhi zisingekuwa kubwa DSM, ningeweka nia ya kujenga nyingine ya walau Vyumba 20 hivi.

Maana Mwaka 2027 tutakuwa na Wageni wengi sana kwaajili ya mashindano ya AFCON
 
Jaribu njia ya kwenda Chamazi mkuu kidogo bei zitakuwa vizuri maana uwanja wa Azam naona ni mmoja wa uwanja utaotumika, naona Tanroad wamechafua sana majengo pembezoni mwa barabara kuwa wayaondoe ikiwemo bar zote maaruf za chamazi nahisi kabla ya mwaka huo Chamazi itakuwa na njia mbilimbili ikibidi hata mwendokasi maana upana wanaotanua ni mkubwa kidogo.
 
Umesema sahihi Mkuu

Na bei za viwanja njia ile haijachangamka sana kama huku City centre, hopeful ukiwa na milioni 18-25 hivi unaweza kupata Kiwanja kizuri pembezoni mwa barabara.

Naona pia hata biashara za Baa pamoja na Vyakula itakuwa hot sana kipindi hicho
 
Karibu sana boss naimani utanipako ajira namimi nitambe mjini[emoji28]
 
Absolutely yes, Lodge inalipa
 
Mkuu naomba jina la hii lodge nitakuwa Mbeya kikazi kuanzia mwezi wa 6
 
Hapa panaitwa KUOKOKA NI LAZIMA Njombe hyo 😀😀😀
 
Asante Mkuu, ila Benki zinasumbua sana kwenye kutoa Mikopo Kwa biashara mpya.

Kuna haja Wizara ya Fedha/Benki Kuu wakalegeza masharti kwenye hizo Taasisi za Kibenki

Vinginevyo ndoto za Wajasirimali wengi zinakufa
Wanakuonea huruma ya kukufisirisi mkopaji.mkopo kwa biashara ambayo haina mwaka siwezi kopesha .Kwa sababu kuna dynqmics unakuwa hujazijua za hiyo biashara.
 
Wanakuonea huruma ya kukufisirisi mkopaji.mkopo kwa biashara ambayo haina mwaka siwezi kopesha .Kwa sababu kuna dynqmics unakuwa hujazijua za hiyo biashara.
Umesema sahihi Mkuu, lakini si Kuna hati za nyumba/viwanja wangepokea kama dhamana ili walau kusaidia Wajasiriamali wanaochipukia
 
Umesema sahihi Mkuu, lakini si Kuna hati za nyumba/viwanja wangepokea kama dhamana ili walau kusaidia Wajasiriamali wanaochipukia
Kuuza dhamana siyo lengo la kwanza la mkopeshaji ;sababu kuna usumbufu wa kuiuza dhamana.Mabenk wanataka kujiridhisha na uwezo wako wa kuingiza mapato.Waone angalau mtiririko wa kipato chako cha muda mrefu kutoka kwenye hiyo biashara,ndiyo wajue watakavyo kukakata.vinginevyo uweke dhamana halafu ukope nusu ya thamani ya dhamana ya soko.ili ukishindwa wauze kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…