Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Faida ya kusajili kama kampuni ni ipi hapo mkuu tupe shule
Atakuja kusema ila nachofahamu ningekuwa nimeisajiri kama Kampuni ningenufaika na fedha ya Uchakavu (Depreciation) kutoka TRA hivyo ningekuwa na punguzo kidogo la Kodi

Maana Kwa biashara yangu ningepata Fedha ya Uchakavu ya almost 37% kama punguzo la Kodi
 

Sio waaminifu kuanzia receptions hadi walinzi hata wamasai siku hizi labda professional companies kama Suma Jkt. Wasipokuibia mapato watawaibia wateja sana.

Kuna trick wanafanya mfano madirisha huwa hayawi locked. Usiku umeme ukikatika walinzi wakishirikiana na vibaka kwa kutumia kama fimbo hivi ndefu ya chuma wanachukua nguo na begi hasa kama vipo karibu na dirisha.

Nyingine ni kuwaambia wateja wakitoka nje waache funguo reception, halafu wanapitia vitu vyao.

Dawa ni kuwa na umeme 24/7 na mfumo thabiti wa CCTV kuizunguka nyumba pande zote, reception na corridors. Unaweza kuwa na mifumo miwili mmoja hata wafanyakazi wote hawaujua ni wewe tu unaojua unakuwa kama taa za kawaida lakini ni camera na mwingine wanaoujua.
 
Nitachukua huo Ushauri wa kufunga camera nyingine ya Siri kama ulivyoshauri.

Uaminifu umekuwa changamoto sana miongoni mwa WaTanzania, watu hawakuonei huruma vile ume- hustle kuweza kujiwekeza
 
Mkuu Hongera sana ila Mbinguni huendi.

Umejenga kiota cha watu Kunyanduana?
 
Faida ya kusajili kama kampuni ni ipi hapo mkuu tupe shule
Kwa kujazia alichosema Grahams

Mfano mteja kaja kwenye lodge akapigwa shoti bafuni akafa au akapata tatizo lolote ambalo mmiliki atatakiwa kufidia, ukiwa huna kampuni mahakama itatumia mpaka nyumba yako ya kulala ili kufidia! Ila ukiwa na kampuni mali zitazokua kwenye risk ni mali za kampuni tu!

2. Kingine ni kwenye kodi, ukiwa na kampuni unaweza usilipe hata shilingi moja provided unatunza gharama mapato na matumizi yako. Tena mda huu anapofanya matengenezo let say ya kumbi ndio mzuri zaidi, gharama zote za ujenzi wa kumbi anaweza wasilisha kama gharama za kampuni na akiwasilisha gharama za mwaka akapatiwa nafuu ya kodi.. angalia hii mifano

A. Assume ana mapato ya 20mil kwa mwaka, bila kampuni tra wataangalia hii 20m kama pato na kukisia jamaa alipe kiasi gani! Hapa anakua hana nguvu ya kucontrol kiasi cha kodi.

B. Chukulia amesajili kampuni na ana mapato ya 20mil kwa mwaka, alafu ndani ya mwaka huo huo akaanza ujenzi wa kumbi na akatumia let say 15mil! Kama alisajili hii kumbi ni mali kampuni basi hii 15mil itaingia kama expense za kampuni... so tra wakija jamaa kupitia mhasibu wake watasema tumepata 20mil lakini tulikua na matumizi ya 15mil ya ujenzi wa kumbi ambayo ni mali ya kampuni hii.. hapo watatoa 20mil - 15mil = 5mil!

Kwa hiyo hii 5mil ambayo ndio faida ndio itatumika katika ku estimate kodi na sio 20mil nzima! Na hapo ni rahisi maana inajulikana kodi ya kampuni ni 30% ya faida!

NB: mimi sio mtaalam wa kodi au mhasibu nimetumia uzoefu na ujuzi wangu mdogo kuhusu makampuni!

Kwa ziada angalia hii video kutoka BRELA:
View: https://youtu.be/DAlo0hOniE4?si=1gD3vPkiHpqUSPxq
 
Umeongea sahihi Mkuu, nimeambiwa Kampuni inasaidia sana kwenye punguzo la Kodi...

Shida ya Nchi hii ni Utitiri wa Kodi

Imagine kabla sijapata hata shilingi 30,000 ya biashara tayari nilikuwa nadaiwa TRA/Halmashauri/Zimamoto n.k
 
Mkuu Hongera sana ila Mbinguni huendi.

Umejenga kiota cha watu Kunyanduana?
Unakumbuka Wazazi wake Yesu walipokwenda ugenini kule kwaajili ya kuhesabiwa na kukosa nyumba za Kulala Wageni hadi kupelekea Walale kwenye Zizi la ng'ombe na Yesu kuzaliwa humo?

Imagine kama hii yangu ingekuwepo nyakati hizo, si wangelala kwangu πŸ€—

Hilo nimechomekea tu Mkuu.... shukrani sana
 
Achana na kamera...weka vitasa vya card ...na software...uhakika zaidi...chumba kikiwa booked unapata notifications online...tumia technology Mzee ...
 
Uzi nzuri Sana ..naomba kuongezea...

Kuhusu wizi tumia technology..nenda jukwaa la IT wakueleze kuhusu vitasa vya card. Na software zake iwe chumba kikipata Tu mgeni unapata notifications hapo hapo...hata kama wa short time.....

Kwingine since wewe ni mpya kwenye biashara nashauri Fanya research ya lodge zilizo kufa au kukosa soko ikiwezekana uzi Kodi upige hela ..

Wengi wanashindwa maintenance Tu...sasa badala ya wewe kutumia hela nyingi kujenga zingine ...jaribu kukodi Kwa mkataba mrefu ..itakusaidia vitu viwili....kwanza utapunguza competition since competition umeinunua...pili utantumia hela ndogo for expansion...

Unaweza amini kkoo kuna hotel inakodishwa Kwa milioni 4 Tu Kwa mwezi wakati ni jengo la ghorofa 8..?

kisa muasisi kafa na watoto wanakula hela yote hawafanyi maintenance..

All in all nakutakia all the best miaka miachache kutoka sasa uwe na lodge hata tano...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…