Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Ukiwa na Kampuni na mfano hii biashara ya Lodge ikawa ni sehemu ya hiyo Kampuni itahesabika kama ni sehemu ya Mtaji wako.

Kwahiyo unavyokuwa unalipa Kodi kule TRA Kwa Mwaka, utajikuta unafunga mahesabu na Deni maana bado hela uliyo wekeza bado haijarudi...

Kwahiyo kama ni Kodi, utaanza kulipa mwaka 4 Kwa mujibu wa hesabu zangu hapo juu za PBP baada ya kwamba mwaka wa 4 utaanza kufunga hesabu na +ve Net Present Value (NPV).

Lakini Kwa sasa utajikuta bado una loss hence Investment Capital yangu bado haijawa recovered
 
Biashara ya Uchimbaji ina changamoto nyingi sana hasa Kwa small scale Mining.

Nilijaribu wakati fulani, lakini Kila nikifanya tathmini mwisho wa mwaka naona napata hasara tu za vibarua na materials

Hivyo nili- quit

Shukrani Kwa mchango wako Chanya, nitafanyia kazi hili.

Barikiwa 🙏🙏🙏
 
Haya ndiyo mambo tunahitahi humu kwakuwa ni mafunzo kwa sisi wajasiliamali, hongera sana
Shukrani Mkuu, tunaendelea kupata uzoefu na kujifunza wote hapa.

Kuna vitu nilikuwa sivijui but kuna watu wamevieleza hadi nimepata mwanga.

Tusiache kujaribu na kufanya Tena hata kama utaanguka mara kadhaa
 
Safi mkuu! Hongera, toa location tuje kukuunga mkono, swali la kizushi huna unoko wa kutaka vyeti vya ndoa hapo kwako mkuu?.
Masharti yangu ni ya kawaida tu, isipokuwa nimeandika Watu wa Jinsia Moja hawapaswi Kulala Chumba Kimoja.

Hii ni kutokana na maadili

Cheti cha Ndoa sijaweka katazo, maana Kuna Uchumba mwingine watu wanakaa hata miaka 10 ndiyo wanakuja kuoana 🤗
 
Umenihamasisha Nina viapartment vyangu vya chumba sebule choo na jiko zaidi ya kumi nimevipanga sehemu Kwa saša vina wapangaji .
Ni wastaarabu nacharge laki 2 Kwa unit Kwa mwezi.
Kwa sasa eneo limechangamka nafikiria kubadili niondoe wapangaji wa mwezi nifanye biashara ya lodge.
ITS good idea lodge zinalipa ukiwa na usimamizi mzuri na eneo lililochangamka na nyumba haichakai
 
Vifanyie ukarabati Mkubwa then vifanye Lodge.

Kama utaweza kuweka sofa, Meza, Tv sebuleni na kule chumbani ukaweka kitanda/godoro na kifriji kidogo then ukafunga Wi-Fi utakuwa na uhakika wa kutoza 50k na zaidi.

Niliwahi Kulala Lodge ya hivyo nililipa shilingi 70,000 Kwa usiku Mmoja japo Kuna Vyumba vingine vya 120,000

Kama umesema Kuna Mzunguko wa watu, lazima Mradi ukulipe 💪
 

Nimekupata mkuu mawazo yako mazuri sana .
Kuna mada nimeziona kuhusu Airbnb nazo nazisoma Kwa kina kujifunza .
Kuna jamaa nimeona kabadili nyumba zake za kupanga kuwa lodge na anapata wateja . Nyumba zangu nzuri kulipo Kwa huyo mshkaji wangu
 
Kuna mada nimeziona kuhusu Airbnb nazo nazisoma Kwa kina kujifunza .
Kuna jamaa nimeona kabadili nyumba zake za kupanga kuwa lodge na anapata wateja . Nyumba zangu nzuri kulipo Kwa huyo mshkaji wangu
AiBnB ni nzuri kwa mikoa mikubwa hasa ukiwalenga wataliii. Unaweza kupangisha kuanzia dollar 20 kwa chumba hadi dollar 500 kwa siku kutokana na nyumba yako iko wapi na viwango vyake.

Pia unaweza kupangisha kwa muda flani hivi tu. Mfano unaweza ukahama kwa siku mbili tatu, weekend, wiki moja, mbili ukapangisha halafu ukarudi ukakaa mwenyewe kukaa au ukaishi na mteja as host family.

Ukishapata review nyingi za kutosha inakuwa rahisi. Kupata pesa nzuri, na wateja wengi. Nyumba inabidi iwe na viwango.

Hosteli nayo ni biashara nzuri, Unaweza ukapangisha hadi vijana hadi 100 au zaidi. Ila inahitaji usimamizi wa karibu.
 

ivi watanzania type yako kumbe bado wapo!!

mi naona humu yamejamaa mambumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…