Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Kwenye hizi english medium wazazi wengi wanasomesha kwa vipato vya ofisini nje ya hapo ni chaalii
Ambapo wakishastaafu kama hawakuwekeza vizuri basi maisha yanabaki kuwa ya kawaida tu
Kama ni connections peleka international schools na wa huko wote wanajiweza
 
Safi yote heri
 
Mi mtoto wangu atasoma shule bora zisizo karirisha kufaulu.

Huwezi kuta hizi shule za International zikitoa ranking baina ya wanafunzi
Ranking kwa wanafunzi haina maana kabisa
Hivi wanategemea darasa zima wote watakuwa wa kwanza 😄
 
Connections inatakiwa iwe mutual broh
Ukijikakamua kupeleka huko iwe kwa ajili ya elimu bora sio connections za kujipendekeza sabb huko no body gives a f#@&^
 
Hizi ni stori tu kama una Hela uchumi wa uhakika peleka mtoto English medium kama huna peleka kayumba lakini hizi habar kwamba mtoto akisoma kayumba anakuwa strong sijui anakuwa na uwezo zaidi na kwamba anaesoma Medium anakuwa nyolonyolo sjui hajui hesabu hizo ni stori za vijiweni sawa na kusema tajiri akifa hazikwi angani atazikwa ardhini na maskini
 
Story za vijiweni kweli.
 
Connections inatakiwa iwe mutual broh
Ukijikakamua kupeleka huko iwe kwa ajili ya elimu bora sio connections za kujipendekeza sabb huko no body gives a f#@&^
Mkuu usidharau ishu ya connections! Tuna mifano hai kitaa. Ebu fuatilia stori ya Makonda ndio utajua maana ya connections Bro!
 
It’s a shame kwamba wanaochangia mada humu ni wanaume!!! Tangu lini mwanaume akawa na uchungu na watoto? Mostly wanawake ndo wanatamani watoto wao wasome shule nzuri wapate exposure ya kujipambania. Shule anaenda kusoma hayo mengine unamfundisha wewe nyumbani. Sadly hao wanawake wenye uchungu na watoto ndo wameruhusu ‘jamii’ iwa label as servants of the house wanatulia nyumbani wanasubiri mwanaume akatafute alete watoto watasoma shule anayotaka baba.

From my experience the last time, Baba mtu alimtoa mtoto wake english medium akampeleka kayumba. Mwanamke anakuja kustuka mwaka unaofuata mume anasomesha
mtoto wa dada ake st Mary’s, wa mchepuko yuko english medium na ameanza kumjengea huyo mwanamke nyumba. Sasa najiuliza, mtoto wake kamkosea nini hadi amfanyie hivyo? Wanaume wengine mmepewa mamlaka ya kuongoza familia but you are dumb!
 
Mimi mwenyewe nimesoma hizo english mediums kwahio naongea kitu nakijua
Kwanza wazazi wachache unakuta wana bizz kubwa kama kina bakhresa etc
Inawezekana umeishia wapi! Kuna T.O mmoja wa hivi karibuni kutoka Kanda ya Ziwa. Anatoka familia ya kimaskini sana hadi alikuwa anaahirisha masomo akapige vibarua. Baada ya kuwa T.O. form four, akapewa ofa ya kusoma Feza Boys. Sasa hivi kamaliza form six na sio tena yule wa kupiga vibarua! Connections zipo hadi Ulaya Bro!
 
Hapo tupo pamoja ila hilo toto chafu la kishua bila shaka kwa sasa lina maisha safi 😁😁. Maana ukitokea familia nzuri halafu kichwani akili ikiwepo, kutoboa ni must
Yuko mbali sana kimaisha sababu Advance alikuja kutulia na kuachana na ujinga akapiga PCM one ya 4. Chuo alisomea nje. Mara ya mwisho nilikutana nae ana kampuni yake na kuna kazi alikuwa anafanya na Tigo. Mimi nimetoka poor family ila kusoma na watoto wa kishua imenisaidia sana... imenitoa tongotongo nyingi tofauti na ningesomea kijijini kwetu. Mimi pia sasa hivi ni wa kishua self-made
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…