miss pablo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2018
- 5,411
- 11,025
Wachagga hiyo hakuna. Tunakusema sana[emoji23]Marehemu hasemwi vibaya ujue na waafrika tukifariki tunageuka mizimu. Shauri yako [emoji16][emoji16][emoji16]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wachagga hiyo hakuna. Tunakusema sana[emoji23]Marehemu hasemwi vibaya ujue na waafrika tukifariki tunageuka mizimu. Shauri yako [emoji16][emoji16][emoji16]
Kwenye hizi english medium wazazi wengi wanasomesha kwa vipato vya ofisini nje ya hapo ni chaaliiTatizo la kusoma st kayumba unakuwa huna strong connections unless ziwe zile special schools. Yaani utajikuta unamaliza lakini marafiki zako wengi watakuwa katika positions ambazo hazimsaidii mtu kati yenu kuondoka katika poverty circle
Yaani circle nzima ya marafiki si ajabu ukakuta huna contact ya kukuambia kuna nchi flani ulata ina fursa flani
Safi yote heriMiezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"
Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane
Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.
Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:
1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.
2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.
Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa
1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.
2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.
Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)
Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..
Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.
Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.
MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.
1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.
2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.
Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.
Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.
Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Ranking kwa wanafunzi haina maana kabisaMi mtoto wangu atasoma shule bora zisizo karirisha kufaulu.
Huwezi kuta hizi shule za International zikitoa ranking baina ya wanafunzi
Connections inatakiwa iwe mutual brohMkuu watu hawaelewi, hao wanaowaona laini ndio wana connections na akili za kuishi soft life zaidi. Imagine mtu kasoma na watoto wa mawaziri, diplomats, businessmen yaani circle nzima ipo loaded. Ndio ulinganishe na mtu kasoma na watoto wa wakulima na wafugaji
Halafu humu watu wanajitoa akili, yaani unawatumia kina Nyerere, Mkapa au Pinda leo hii kama successful stories na wakati dunia yao na yetu ni mbingu na ardhi..
Kiukweli hata kama primary ntawasomesha shule za kawaida ila kuanzia o level acha wakapambane na kutengeneza future connections na exposure
Kuna wengine wanasomeshewa na makampuni wanasomeshewa na wanayofanyia kazi Ila hawasemi kwa watu waonekane wanazo.Nimekuwa ndio nimekuja kugundua kuna watu walikuwa wanalipa ada
Kuna jirani watt wake wa5 wote ni st constantine arusha na vyuo ni nje aisee
Ninaye muongelea huyo ni mfanyabiasharaKuna wengine wanasomeshewa na makampuni wanasomeshewa na wanayofanyia kazi Ila hawasemi kwa watu waonekane wanazo.
Kabla ya kumsema tunaweka chumvi mdomoni ili tusigeuke jiwe.Marehemu hasemwi [emoji16]
Sizitaki mbichi hiziHuu uzi umenikumbusha ule wimbo wa;
"Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,...!"
Story za vijiweni kweli.Hizi ni stori tu kama una Hela uchumi wa uhakika peleka mtoto English medium kama huna peleka kayumba lakini hizi habar kwamba mtoto akisoma kayumba anakuwa strong sijui anakuwa na uwezo zaidi na kwamba anaesoma Medium anakuwa nyolonyolo sjui hajui hesabu hizo ni stori za vijiweni sawa na kusema tajiri akifa hazikwi angani atazikwa ardhini na maskini
Mkuu usidharau ishu ya connections! Tuna mifano hai kitaa. Ebu fuatilia stori ya Makonda ndio utajua maana ya connections Bro!Connections inatakiwa iwe mutual broh
Ukijikakamua kupeleka huko iwe kwa ajili ya elimu bora sio connections za kujipendekeza sabb huko no body gives a f#@&^
Ahahahahaha!!!Sizitaki mbichi hizi
Mimi mwenyewe nimesoma hizo english mediums kwahio naongea kitu nakijuaMkuu usidharau ishu ya connections! Tuna mifano hai kitaa. Ebu fuatilia stori ya Makonda ndio utajua maana ya connections Bro!
Inawezekana umeishia wapi! Kuna T.O mmoja wa hivi karibuni kutoka Kanda ya Ziwa. Anatoka familia ya kimaskini sana hadi alikuwa anaahirisha masomo akapige vibarua. Baada ya kuwa T.O. form four, akapewa ofa ya kusoma Feza Boys. Sasa hivi kamaliza form six na sio tena yule wa kupiga vibarua! Connections zipo hadi Ulaya Bro!Mimi mwenyewe nimesoma hizo english mediums kwahio naongea kitu nakijua
Kwanza wazazi wachache unakuta wana bizz kubwa kama kina bakhresa etc
Yuko mbali sana kimaisha sababu Advance alikuja kutulia na kuachana na ujinga akapiga PCM one ya 4. Chuo alisomea nje. Mara ya mwisho nilikutana nae ana kampuni yake na kuna kazi alikuwa anafanya na Tigo. Mimi nimetoka poor family ila kusoma na watoto wa kishua imenisaidia sana... imenitoa tongotongo nyingi tofauti na ningesomea kijijini kwetu. Mimi pia sasa hivi ni wa kishua self-madeHapo tupo pamoja ila hilo toto chafu la kishua bila shaka kwa sasa lina maisha safi 😁😁. Maana ukitokea familia nzuri halafu kichwani akili ikiwepo, kutoboa ni must
Ndiyo.Kwa hiyo huko siku hizi wapo watoto wa viongozi wakubwa na wafanyabiashara wakubwa?