Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Nimekuwa ndio nimekuja kugundua kuna watu walikuwa wanalipa ada
Kuna jirani watt wake wa5 wote ni st constantine arusha na vyuo ni nje aisee
 
Matajiri wanawasomesha watoto wao kwenye shule za gharama ili waje warithi na kusimamia kampuni zilizoanzishwa na familia; kama wewe unatengeneza kizazi cha kuajiriwa, usiangaike na mashule ambayo chekechea unalipa milioni 12+
 
wakati mwingine,umaskini unasababisha uwe na moyo wa chuki bila sababu.
 
sasa upambane kutafuta za nini kama hutaki zitumike kwa wanao,ukifa mashamba na majumba watanyanga'nywa na baba wadogo,warithishe kitu ambacho hawawezi nyang'anywa.acha uwoga wa maisha...

Watanzania mnapenda sana kupigwa aisee.

Yani nikatoe milioni 4 ili mtoto wangu afundishwe A for Apple? Mwisho wa siku Hesabu sifuri sayansi sifuri ila anajua tu KIINGEREZA cha kubabaisha.


Pesa haitumiki kizembe namna hiyo.. Muweke st kayumba weka usimamizi kama.msingi wa KIINGEREZA mtafutie walimu na programme nzuri za KIINGEREZA ili anapoingia form one masomo ya secondary yasimsumbue.


Acheni utoto nyie...


Kwanza hampo hata smart mngekuwa smart mngewauliza kwanza watoto wenu wanataka kuwa nani ndo muwapeleke kwenye shule inayo toa programme husika. Sio una hangaika kumkaririsha English Medium kumbe mwenzako anataka kuwa kama Konde Boy..

vinginevyo nyie na wanao somesha watoto wao st kayumba wote mpo sawa ila wenzenu wajanja nyie mnapigwa mamilioni wenzenu hawapigwi
 
Watanzania mnapenda sana kupigwa aisee. Yani nikatoe milioni 4 ili mtoto wangu afundishwe A for Apple? Mwisho wa siku Hesabu sifuri sayansi ila anajua tu KIINGEREZA cha kubabaisha.
Si kweli. Hakuna shule inayotoza gharama hizo ukaikuta hata na division three moja
 
Wengi watakuponda, ata waliosoma kwenye hizo shule sijaona wakifanya cha maana, sijawaona wakichimba au kumiliki visima vya mafuta wala gesi
 
Hizi ni kauli za kujaribu kubalance tu mabaya na mazuri. Lakini ukweli unabaki, huwezi kupata elimu bora katika shule ambayo mwalimu hana cha kupoteza
Unachanganya elimu bora na matokeo mazuri kwenye mitihani ya mwisho.

Tanzania hakuna elimu bora on the first place.
 
Ngoja uje upingwe kabuni yangu Primary Kayumba Sec private kwa kua watoto wangu wa kike na Niko busy kidogo na maisha advance boarding Gvt Inshaa Allah..
Na mwanangu std 7 alipata A ,ameenda huko seminary anaburuza akiwaambia ametoka Kayumba hawaamini,haka kadogo Nako nakaandaa na Kingereza kakifika std 6 naanza kukaprooni vzr Ili kaweze kufaulu vzr na kakapambane huko Kwa masista
Lengo ajue tu Kingereza maana huku Kayumba Secondary kama mtoto mzembe hatoboi na kama mzazi uko busy ni changamoto (kunahitaji uangalizi na ushirkiano mkubwa kati ya mzazi ,mwl na mtoto)
 
Ila english medium za siku hizi michosho sana kipindi zinaanza st marys green acres academic etc walimu wengi walikuwa ni wakenya kidogo ilikuwa angalau 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…