Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Kuna kitu hapa ngumu sana kuelewa kwa haraka, labda sababu ya mfumo wa maisha yetu tuliyo zoea na kuamini, Jambo moja najua ni kua kuna watu wenye majina ya wake za watu wapo katika mateso makubwa na ndoa zao na mfumo wetu bado hauruhusu kusema hadharani kwa kigezo cha uvumilivu , unaweza ona ata katika hili jamaa ana mchepuko kitambo kabisa lakin haionekani kama hoja, hoja ni mwanamke kutoka, Hatuwezi amua kwa kutazama hii tu au kumwonea huruma jamaa ,labda hii ndio inayo fanya DUNIA ISIWE NA USAWA?
 
Acha uboya.

Unapokuwa mtanashati kwa mkeo jua kuwa masela watapiga.

Kaa na watu wazima wakushauri maana hali halisi ni kwamba shetani kaivutia bange ndoa yenu
 
Ishawahi nikuta hii aisee sitakaa nisahau japo nilikuwa nashuhudia moves za jamaa toka anaingia! Mpaka demu anabeba viatu vyake anaviingiza ndani! Nikawakurupua kabla hawajaanza sex
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimejikuta nachek kwa sauti kubwa
 
Hana haki ya kulalamika maana na yeye mzinzi. Malipo ni hapa hapa duniani
Mama/mke akiwa mchepukaji baba/mume awe Mtu wa Maombi kuzikemea nguvu za shetani na kuiombea familia baraka na mafanikio. Hali kadhalika, mume akiwe mchepukaji mama awe Mtu wa Maombi hiyo ndio namna ya kusaidia. Lakini hii ya wote kulipiziana na kuchepuka kwa malipizi haiwezi kuwa suluhisho.
 
Ww unafurahia? Kweli nyny wadada unaeza mtu akafa ww unacheka tu
Waache Mkuu. Mkuu pole kwa yaliyokukuta. Kimsingi upendo kwa mkeo uliisha kitambo ninahisi ulibaki kwenye ndoa kwa matakwa ya kiapo tu. Kama una mapenzi japo kwa mbali kwa mwenzio angalia option ya kumsamehe (sio rahisi) hii ni kama bado una hisia za mapenzi kwa mkeo. Na mpeane leave ya kutokuwa pamoja angalau kwa mwaka mmoja. Kama hauna hisia tena na mwenzio ni muda umefika sasa muachane.
 
Tuliolelewa na wazee tumepigwa marufuku kurudi nyumbani bila taarifa madhara yake ni makubwa sana
 
Hii meseji yako naifanyia lamination kabisa naibandika ukutani
 
Pole.sana kaka!! Lakini kama ulivyosema, umefanya naye mambo mengi, na mna watoto wawili ambao ni wadogo, endelea kutumia busara ndugu yangu, Mungu akuongoze!!
Mwanamke aliwe nje uniambie busara . Nyie sijui mnatoaga wapi izi akili .
 
Umenena vyema
 
Acha upumbavu na wewe yaan unaongea upupu tu hapa naludia tena acha ujinga

Sent from my Infinix X682B using JamiiForums mobile app
 
Tulia kijana wangu kaa nae chini muulize sababu ya yeye kudenemka ni nini hasa? Huenda akatoa sababu ambazo wewe ndio chanzo.
 
Ningumu sana kumuacha mwanamke ambaye tayari mmesha zaa nae watoto. Wakuu mtoto nikitu kinachopendwa sana (naamini kwa wengi iko hivi) na mtoto anafaa kulelewa na wazazi wote wawili ( naamini kila mwenye mtoto anatamani kuona hivo) hivo kumuacha mtoto wako alelewe na mtu mwingine inauma sana.

👉Lakini kitendo cha mwanamke kuchepuka kwenda kufanaya mapenzi na wanaume wengine kwa mwanaume aliye muoa ni fedheha kubwa sana . Mm binafsi nlisha mwambia mke wangu kwamba kitu namba moja kitakachofanya nimuache mara moja nikugundua kua anafanya mapenzi na wanaume wengine.
 
Unamatatizo wewe na hutamuacha uyo mwanamke maana sio mda mrefu utampelekea moto tu na ukisha mpelekea moto tu umeshajiloga hutanuacha
Piga chini kenge iyo piga chini jinga ilo yaan mwanamke msaliti kwenye ndoa ni nyoka mkubwa mkubwa sana piga chini mbuzi iyo bwana mdogo

Sent from my Infinix X682B using JamiiForums mobile app
 

Point of correction, waambie ndugu , jamaa na marafiki mnaachana kwa kuwa wote mumetoka nje ya ndoa, huyo mwanamke hajatoka nje ya ndoa peke yake hata wewe pia umesaliti ndoa. Usimtwike zigo lote mwenzako, gawaneni 50:50 maana wote kosa lenu ni moja. Ila mleta uzi bado unanishangaza sana , yani mpaka sasa unajihesabia haki, huuoni uzinzi wako ila unauona uzinzi wa mkeo tu [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…