Mrejesho kuhusu kupima DNA za watoto wangu

Mrejesho kuhusu kupima DNA za watoto wangu

Hiyo ni roho ya ubinafsi, na inaweza fanya mtoto kuwa mnyonge hata kupunguza upendo, katika maisha ya dunia hii hakuna ajuae kesho.. unachoweza kukitaa leo kumbe kesho kimeandaliwa kuwa kama daraja kwako... Siwezi mpima mtoto DNA .. mtoto anapotungwa mimba hakuna alichopanga anazaliwa tu hana makosa awe wako au sio wako
Endeleeni kuzaa hovyo hovyo mkutarajia huruma ya kulelewa watoto wenu wa vichochoroni sasa hivi watu wameshtuka hela yenyewe ngumu.
 
kukwepa watoto wa mitaani
hata kama siyo wako, watakuambia ni wako
Huyu alijichanganya tu sijui alikua hajui haya au uliona ame WIN na yeye kumbe mawakili walikua wanamchora tu..
 
kukwepa watoto wa mitaani
hata kama siyo wako, watakuambia ni wako
Hii imani potofu mtaendelea kule mabustard mpaka mkome.

Kwenye science hakuna kitu kama hicho.

Watoto maelfu wako mitaani na hawajapimwa DNA
 
Mimi namwambia ukweli
Haya mambo sio ya kuchokonoa na kujitapa
Oooh hooooo
Wale maelfu wako mitaani ni baada ya kupima DNA??

Wanaume wameshtuka. Mambo ya kusakiziana mimba yatafika mwisho.
 
Kuna kipindi mkemia mkuu wa serikali alisema asilimia kubwa ya wanaopima watoto wanakua sio wao ila wanaambiwa ni wao ili kupunguza watoto wa mtaani.
Na hii ina kama kaukweli yaani kwenye report yao wanakuambia wengi waliopima watoto sio wao mwisho wa siku kila anaenda wanampa majibu kuwa ni wao ili kukupa imani mtoto asiteseke na ndoa isiharibike na ndo maana majibu hawakupi kwa sababu unaweza ukaenda ku confirm Kenya ukakut tofauti.
NIMESHAWAHI KUPIMA NITAKUJA KWA USHUHUDA NGOJA MWEZI MTUKUFU UISHE
 
Hiyo ni roho ya ubinafsi, na inaweza fanya mtoto kuwa mnyonge hata kupunguza upendo, katika maisha ya dunia hii hakuna ajuae kesho.. unachoweza kukitaa leo kumbe kesho kimeandaliwa kuwa kama daraja kwako... Siwezi mpima mtoto DNA .. mtoto anapotungwa mimba hakuna alichopanga anazaliwa tu hana makosa awe wako au sio wako
Mbususu zisipokuchanganya you are one of the greatest thinkers of our times. Ukiweza tu kuzishinda mbususu basi, tutakusoma vizazi na vizazi huko mbele ya safari [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Miezi kadhaa imepita niliandika uzi humu nikasema nitaenda kupima DNA watoto wangu.

Nilipatiwa muongozo kwenye ule uzi na baadhi ya wanasheria/mawakili waliomo humu ikabidi kumjulisha wakili wangu akasema inawezekana na ni rahisi sana.

Nashukuru nimekuta mabao yote ni yangu, I felt like Messi for a while, hahahahahaaa.

Naendelea kuwashauri wanaume wenzangu kuzingatia kupima DNA za watoto wenu, kulea mtoto asie wako watakuja kukuletea shida ukubwani.

Ciao
Siku ukibahatika kwenda nje hususan Ulaya au Marekani nenda na vinasaba vya wanao (nywele, kucha, mate...) ukapimie DNA huko. Ikitoka kuwa ni wako wote ndo kaa ujipongeze. Kwa hapa Bongo yawezekana ukawa umepigwa!
Screenshot_20230416_214924_Chrome.jpg
 
unaonekana ni mtu mwenye asili ya ubinafsi rohoni mwako, wewe kulelea mtoto ambao si wako waona shida na je wakwako utakapokufa nani awalele na hizo shida ulizosema nani atazibeba utakapokuwa haupo

Hivi unajua shida kiasi gani uliowap wazazi wako toka ukiwa mdogo mpaka leo hii

World wouldn't be a better place if we had people like you .....
Acha kuhalalisha upumbavu kama ningetaka kulea mtoto asiye wa kwangu ningeenda vituo vya mayatima nikachukua mmoja nikalea.
Yaani nikuoe uniletee dharau ya kufanya uchafu wa uzinzi na bado unauleta nyumbani kwangu alafu nikuache eti nisonekane mbinafisi?

Mwana mke yeyote anaye enda kubebeshwa mimba na mwanaume mwingine hali ya kuwa ameolewa na mme wake ana uwezo wa kuzalisha huyo ni mwana mke mpumbavu na hana akili.

Na wanawake wote walio fanya upuuzi huo mwenyezi mungu ameahidi kuwapa adhabu kali sana na yenye kudhalilisha.
 
KAMA HUJUI HATA MAJIBU YA DNA WAMEKUPA YA UONGO...
Ni kama sikuhiz matokeo ya UKIMWI ukienda kichwa kichwa una presha wakikukuta una ngoma wanakuambia HUNA UKIMWI urudi baada ya miezi 3...
Boss unaingilia miongozo ya afya, mambo ya afya hayachezewi hivyo sawa mkuu. Kukuambia urudi baada ya miezi 3 ni kwasababu incubation period ya ukimwi ni miezi 3 kabla ya hapo kwavipimo huwezi kuuconfirm. Ya mtaani yaache mtaani, wakikucheleweshea kukuanzishia dose kama una ukimwi kweli utaishi kwahali mbaya hata ukianza dose baadae. Afya sio siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes... nilijua hilo kabla, wakili aliesimamia ni zaidi ya ndugu kwangu, kama na huyo kanidanganya basi kweli hivi viumbe nimeandikiwa kuvilea
Suala siyo wakili wako. Suala ni huko kwa Mkemia mkuu. Wakili wako akipewa matokeo ndiyo siyo atafanya nini?

Lea hao watoto wawe ni wako ama la!

Mimi mtoto akizaliwa kwangu sitakaa niwe na mashaka hata kama nikigundua siyo wangu. Nitachukulia kama sadaka natoa kwa kulea mtoto wa mtaani lakini kamwe sitamfukuza wala kumtelekeza....na hatakaa ajue labda mamake amwambie.
 
Sharti la mtanzania kamili anayeongea kiswahili ni kufanana na mtoto wako.
Kichwa ,mwili, masikio, macho au tembea au sauti. Ukikosa hivo wewe tunakutenga kwanini mpaka upime DNA. Kwenda zako mwana mpitevu wewe. Ulitegemea uambiwe si wako.
 
Mbususu zisipokuchanganya you are one of the greatest thinkers of our times. Ukiweza tu kuzishinda mbususu basi, tutakusoma vizazi na vizazi huko mbele ya safari [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
🙏🙏🙏🙏 Mungu anisaidie kwakeli, maana mwili dhaifu, ila roho i radhi..
 
Mkuu nisikudanganye, Mtoto ukishahisi kutoka ndani ya moyo wako sio wako basi sio wako.
Mkuu hisia ni hisia ila siukweli, naunahisi juu ya matendo ya mama yao ila siwatoto. Tutumie hekima na akili kama wanaume, sio hisia. Kwahisia mwanamke aweza kukudhania unacheat ila wewe wala hufanyi hivyo. Tujitofautishe natukubali makosa kama hisia zako ni zauongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aah me namshukuru demu wangu mana tumbo lake lina photocopy machine, hizo DNA nasikiaga tu ila hongera mkuu kwa kuhakiki.
 
Kuna muda sisi wenye taaluma yetu ya udaktari tunaamua kutumia busara tunataka Tanzania iwe sehemu salama ya kuishi😁😁😁
 
Mie wakwangu ni wangu. uthibitisho niliofanya ni kuchunguza vitabia vyao. wote wana vitabia ambavyo utotoni nilikuwa nayo na maumbile nadra. Mfano naweza kukunja kidole kwa namna mtu mwingine inakuwa ngumu. Vidogo nikaviambia vikunje vikaweza Daa!
 
Back
Top Bottom