Mrejesho! Nilimpa mwanaume mtaji akaniacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine

Mrejesho! Nilimpa mwanaume mtaji akaniacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
MREJESHO; NILIMPA MWANAUME MTAJI AKANAICHA NA KWENDA KUOA MWANAMKE MWINGINE!

Kila kitu kilikua kizuri, tulipanga kuhusu kuoana. Wakati namaliza chuo nilikua na pesa yangu kama milioni tatu hivi, hizi ni pesa ambazo Baba yangu aliniwekea kwenye akaunti tangu nasoma, alipofariki basi sikuzitumia kwani nilikua na Boom. Tulipomaliza chuo mimi na mpenzi wangu tulikubaliana tuzae mtoto kwanza ili yeye aanze Biashara na tukishafanikiwa basi tutaoana.

Kweli nilibeba mimba, mama alikasirika lakini sikujali kwani nilikua na mwanaume na tunapendana sana. nilimpa ile pesa akanza Biashara, alikua anafanya Biashara ya vitunguu, anazunguka minadani. Mwanzo alikua akinipa pesa niweke mimi, lakini ghafla alibadilika, akawa anabaki nazo, nikimuuliza anakasirika na kuniambia kuwa nataka kumpenda kichwani.

Tukaanza kugombana, mwanzo nilikua karibu na Mama yake, tukaw akila tukigombana nampigia simu namuambia ananiambia ataongea naye. mara ghafla Mama yake alinigeuka, akawa hataki kuongea tena na mimi na ikafikia kipindi akniambia kuwa wanachotaka ni mtoto wao lakini hawanitaki tena wkani nina mdomo sana hivyo nitamtawala mtoto wao.

Niliona kama utani, lakini mwaka jana mwezi wa nne alikuja na kunirudishia milioni tatu zangu. Akaniambia hanitaki tena anaenda kuoa kuna mwanamke kachaguliwa na ndugu zake. Kumbe alishakusanya mtaji, ana pesa akaamua kuniacha. Niliumia sana, nikalia kwani mimi nilianza kukusoma mwanzoni lakini kwa namna tulivyokua tunapendana nilijua kuwa mwanaume wangu ni tofauti.

Nilikuja kwako nakumbuka ukaniambia, nina maamuzi mawili, kuchukua milioni tatu nitafute chakwangu nifanikiwe, au niisuse nianze kulia na kumuomba Mungu amlaani huyo mwanaume ambaye alishakua mume wa mtu. Ushauri wako ulikua mchungu, haukunifariji lakini ulinifungua macho. Nilijikuta napata ujasiri, nakumbuka uliniambia muone mwanao kama Baraka na si laana.

“Unapoachana na mtu mnagawana vitu viwili, kwanza ni LAANA na pili ni BARAKA, laana inakuja pale ambapo hukubali kuachika, kila siku unamfuatilia, unakua na hasira na unataaka kulipa kisasi kila dakika. Inakua ni laana kwakua unasimamisha mambo yako na kumfuatilia yeye, ni ngumu kufanya kitu chochote cha maendeleo, ni ngumu kupata mwanaume wa kukuoa kwani kila dakika utakua na hasira.

Ningumu kuwa hata na marafiki, badala ya kuonekana kama msichana utaonekana na kutambulika kama “Dada aliyeachwa!” BARAKA inakuja pale ambapo unakubaliana na ukweli, unasema kaniacha, kanichukulia pesa zangu lakini nina uhai na nina afya. Unachukua milioni tatu, unaanza kuzifanyia kazi, unaacha kumfuatilia, kama hahudumii mtoto unaacha kuhangaika naye, akikuona una furaha bila yeye hapa utaona anaanza kuchanganyikiwa.

Anakua na kisirani, hasira, sasa yeye anakua amechagua LAANA, furaha kwake inakua ngumu hata mambo yake yanakua magumu. Lakini kama asipochagua kukufuatilia basi naye atachukua Baraka na laana mtaiacha wote. Hivyo chagua na njoo kwa mrejesho.”

Kaka nilchagua Baraka, ilikua ngummu lakini sikua na namna, nikaacha kumfuatilia na ile milioni 3 nikaanza kuikopesha kwa watu, baadaye nikaanza kuagiza vyombo vya mtumba nikawa nauza online, katika kuuza ndipo nimekutaana na mwanaume ambaye sasa hivi ndiyo mume wangu. Nina furana na amani, na kama ulivyosema Kaka, ukichagua BARAKA yeye anaweza kuchagua LAANA.

Iko hivi, mwanzo hakua anahanagika na mimi, lakini aliposikia naoelwa alikuja na kujifanya kajutia, bado ananipenda na mambo kibao. Alikua hahudumii mtoto akajifanya anataka kuhudumia, nilimuambia twende ustawi wa jamii ili tukapangiwe na kama ni matumizi apeleke huko, hakutaka, akamtafuta mchumba wangu na kuanza kumuambia mambo mabaya kuhusu mimi, sijui nilimsaliti, mimi ni Malaya awe makini na mimi.

Mchumba wangu alimsikiliza akamjibu “Kuwa mwanaume basi ukiachwa achika acha kujiliza kama ndiyo unaona siku zako kwa mara ya kwanza” alimblock, kaka kweli uliyosema sasa hivi nasikia na mke kamrudisha nyumbani yaani baada ya mimi kuolewa tu ni kama wakawa hawapatani, nilijua kwakua mwanamke alinipigia kuniomba niongee na mume wake na kama alinikosea basi nimsamehe kwani hayuko sawa kabisa, ni kama kachanganyikiwa. Nilimjibu tu tuliachana hajanikosea nilishasamehe ndiyo maana nina amani, sikutaka kuongea naye wala kuhangaika naye tena ana sasa hata sijui anaishije.

Nakushukuru sana Kaka, ulinifanya nikachagua Baraka, nashukuru kwani Kitabu chako kilinisaida kupitia kipindi kigumu sana cha maisha yangu, nashukuru sana, ushauri wako siku zote ni mgumu lakini unasaadia, nashukuru sana kwa kitabbu Kaka!

NB: Umeachwa na una maumivu, hujui namna ya kumsahau X wako, soma Kitabu changu cha “HAKUNA KUACHWA ACHWA” Sehemu ya 3 nimezungumzia namna ya kumsahua X wako na kuwa sawa kabla ya kuanza mahusiano mapya.
 
mwenzenu nimeangukia kinuu kwenye tamasha moja apa jijinii
FB_IMG_1725037419632.jpg
 
Back
Top Bottom